MABAKA YANAYOWASHA CHINI YA MATITI.


image


Posti hii inahusu zaidi mabaka yanayowasha chini ya matiti, ni ugonjwa ambao uwapata wanawake walio wengi na wengine hawajapata jibu Sababu zake ni zipi na pengine uchukua hatua za kutumia miti shamba wakidai juwa hospitalini nugonjwa huu hautibiwa, ila ni sababu za kawaida zinazosababisha ugonjwa huu na pia unatibika vizuri sana.


Tatizo la mabaka yanayowasha chini ya matiti.

1. Tatizo hili kwa kawaida linaweza kumpata mwana mke yeyote yule hasa hasa uwapata wanawake walio wanene , wanawake wenye Ugonjwa wa kisukari, wanawake wenye matiti makubwa, wanawake wanaofanya mazoezi sana na pia wale wenye pilika  pilika nyingi.

 

2.Ugonjwa huu utokea pale ambapo kuna misuguano kutoka sehemu mbili za matiti zinazoangaliana , baada ya sehemu hizo kubwa na msuguano kwa sababu ya shughuli mbalimbali au wakati wa mazoezi na hewa kwenye sehemu hiyo uwa kidogo hali ambayo Usababisha kuwepo kwa michubuko.

 

3.Kwa sababu ya michubuko ambayo huwa kwenye sehemu za matiti Usababisha wadudu kama vile bakteria na virusi kuweza kuingia kwenye michubuko hiyo kwa hiyo mama anaanza kuwasha na kujikuna hali ambayo Usababisha michubuka chini ya matiti.

 

4. Na kwa wakati mwingine kama kuna unyevunyevu kwenye matiti ukachanganyikana na wadudu hao hali inaweza kwa ngumu zaidi na kusababisha kujikuna sana , tatizo hili huwa kubwa zaidi hasa kwa wanawake wale wanaoshinda kwenye shughuli za kutumia nguvu na hawaogi hali huwa ngumu kwa sababu unaweza kukuta matiti yamechubuka sana.

 

5. Kwa hiyo baada ya kujua tatizo hili wanawake wote hasa kama ni wanene au wembamba ni vizuri kusafisha kwenye sehemu za matiti kwa maji safi na sabuni ili kuepuka na tatizo hili kwa sababu chanzo hiki ni kutofanya usafi na pia wanawake wenye Ugonjwa wa kisukari wawe makini sana kwa sababu walipatwa na tatizo hili ni vigumu kupona haraka kama wale wasio juwa na kisukari.

 

6.Pia ikumbukwe kwamba kwa akina Mama wanaopiga mazoezi kila siku au kufanya kazi zenye nguvu kama vile kulima kwa mda mrefu wanapaswa kuiga kila siku walau kwa mara moja na kunywa maji mengi ili kuepuka tatizo hili la kuwashwa kwenye matiti.

 

7.Pia kama imetokea mtu akapata na Ugonjwa huu anapaswa kutumia dawa kutegemea na kisababishi kama waliosababisha ni bakteria Mgonjwa anapaswa kutumia dawa ambazo ni antibiotics kama vile benzathine penicillin, erythromycin, oral penicillin kwa ajili ya kuondoa Maambukizi.

 

8.Pia Mgonjwa anaweza kutumia dawa iwapo  kisababishi ni fungusi anaweza kutumia dawa zinazotibu fungasi kama vile cream zinazotibu fungasi na pia katika matumizi ya dawa hizi hazipaswi kutumiwa kiholela zinatumiwa kwa ushauri wa wataalamu wa afya kwa sababu mtu unaweza kutumia dawa huku una Ugonjwa mwingine hali ambayo inaweza kusababisha matatizo mengine makubwa.

 

9. Vile vile kwa wale wenye imani potofu juu ya ugonjwa huu waache kwa sababu watu baada ya kupata tatizo kama hili hawakubali kwenda hospitalini na kuanza kutumia miti shamba ambayo uchukua mda mrefu kutibu tatizo na tatizo linaendelea kuongezeka kila siku hali ikiwa mbaya ndipo wanakumbuka hospitali na unakuta wadudu wanakuwa wameingia mpaka ndani na kusababisha madhara makubwa.

 

10.Kwa hiyo akina Mama huu ni ugonjwa wa kawaida tu na unatibika ukipata tatizo nenda moja kwa moja hospitali ili uweze kupata matibabu kwa sababu Ugonjwa huu umewapa eatu wengi wametibiwa na wamepona na wanaendelea vizuri na maisha.



Sponsored Posts


  ðŸ‘‰    1 Hadiythi za alif lela u lela       ðŸ‘‰    2 Jifunze fiqh       ðŸ‘‰    3 Madrasa kiganjani       ðŸ‘‰    4 Mafunzo ya html kwa kiswahili       ðŸ‘‰    5 Magonjwa na afya       ðŸ‘‰    6 Mafunzo ya php    


Je! una maswali, mapendekezo ama maoni? tuma ujumbe wa meseji SMS hapo chini ili kuunganishwa na muhusika au bofya hapa

SMS SMS



Post Nyingine


image Huduma ya kanza kwa mgonjwa mwenye jeraha la kawaida kwenye ubongo
Posti hii inahusu zaidi huduma ya kwanza ya mgonjwa mwenye jeraha la kawaida kwenye ubongo, ni Tiba ambayo utolewa kulingana na dalili za jeraha la kawaida kwenye ubongo kama ifuayavyo. Soma Zaidi...

image Kazi za madini ya Shaba mwilini.
Post hii inahusu zaidi madini ya Shaba mwilini,ni madini ambayo ufanya kazi mbalimbali mwilini, kama ifuatavyo Soma Zaidi...

image Nini chanzo cha malaria
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu chanzo cha ugonjwa wa malaria Soma Zaidi...

image Njia za kuzuia Ugonjwa wa tauni.
Posti hii inahusu zaidi njia mbalimbali ambazo zinaweza kutumika ili kuweza kuepuka Ugonjwa wa raundi. Soma Zaidi...

image Minyoo Ni nini
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu maana ya minyoo Soma Zaidi...

image Zijue sababu za kupungukiwa damu mwilini
Posti hii inahusu zaidi tatizo la kupungukiwa damu mwilini, ni ugonjwa unaotokana sana hasa kwa watoto wadogo chini ya miaka mitano ingawa na kwa watu wazima. Soma Zaidi...

image Ugonjwa wa Dondakoo na namna unavyoweza kuenea
Posti hii inahusu zaidi ugonjwa wa Dondakoo na namna unavyoweza kuenea kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mtu mwingine. Soma Zaidi...

image Huduma ya Kwanza kwa mtu aliyeng'atwa na nyoka
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu huduma ya Kwanza kwa mtu aliyeng'atwa na nyoka Soma Zaidi...

image Dalili za ugonjwa wa ngiri
Posti hii inahusu zaidi Dalili ambazo mgonjwa wa ngiri anaweza kuzipata, kwa hiyo baada ya kusoma na kuelewa dalili hizi mgonjwa anapaswa kuwahi hospitali mapema kwa ajili ya kupata matibabu. Soma Zaidi...

image Ugonjwa wa kisukari
Ugonjwa wa kisukari hurejelea kundi la magonjwa yanayoathiri jinsi mwili wako unavyotumia sukari kwenye damu (glucose). Glucose ni muhimu kwa afya yako kwa sababu ni chanzo muhimu cha nishati kwa seli zinazounda misuli na tishu zako. Pia ndio chanzo kikuu cha mafuta kwenye ubongo wako. Ikiwa una Kisukari, haijalishi ni aina gani, inamaanisha kuwa una sukari nyingi kwenye damu yako, ingawa sababu zinaweza kutofautiana. Glucose nyingi inaweza kusababisha matatizo Soma Zaidi...