image

Madhara kwa wasiofanya mazoezi

Posti hii inahusu zaidi madhara mbalimbali ambayo yanaweza kutokea kwa watu wasiofanya mazoezi, mazoezi ni kama tiba kwa namna Moja au nyingine ila Kuna madhara ambayo yanaweza kutokea kwa wale ambao hawafanyi mazoezi.

Madhara kwa wasiofanya mazoezi.

1. Kuwepo kwa magonjwa mbalimbali ya kuambukizwa.

Kwa sababu ya kutofanya mazoezi Kuna hatari ya kuwepo kwa magonjwa mbalimbali yasiyoambukizwa magonjwa hayo ni pamoja na saratani mbalimbali, mshutuko wa moyo na kisukari hayo ni baadhi ya magonjwa ambayo yanaweza kutokea kwa watu ambao hawafanyi mazoezi.

 

2. Kuwepo kwa Uzito mkubwa na unene wa kupitiliza.

Kwa sababu ya kuwepo kwa mafuta kwenye mwili Kuna hatari ya kuwepo kwa uzito mkubwa na uliopitiliza  kwa sababu kila kitu kinachoingia mwilini ukaa humo humo na hakitoki mwilini hali inayosababisha kuwepo kwa uzito mkubwa na unene wa kupitiliza.

 

3. Pia kutofanya mazoezi usababisha kuwepo kwa presha .

Kwa sababu ya kuwepo kwa kiwango kikubwa cha mafuta kwenye mwili usababisha mishipa kuziba na upelekea kuwepo kwa presha kw watu ambao hawafanyi mazoezi.

 

4. Pia kwa wale wasiofanya mazoezi wanaweza kuwa na matatizo katika upumuaji.

Kwa sababu ya kuwepo kwa mazoezi usaidia vile vile kuweka kifua kwenye hali nzuri na pia mapafu yanakuwa na uwezo wa kupitisha hewa Vizuri kabisa bila shida yoyote, ila kwa wale wasiofanya mazoezi ni vizuri kabisa kufahamu kwamba wanaweza kupata matatizo mbalimbali katika upumuaji.

 

5.vile vile kwa wale wasiofanya mazoezi wanaweza kupata matatizo ya kuwepo kwa cholesterol kwenye mwili kwa sababu cholesterol usababishwa na kuwepo kwa kiwango cha mafuta mwilini kwa hiyo kwa wale wanaofanya mazoezi hawawezi au ni vigumu kupata tatizo hili kwa hiyo ni vizuri kabisa kufanya mazoezi Ili kuepukana na tatizo la kuwepo kwa cholesterol mwilini.

 

6. Pia kwa wale wasiofanya mazoezi Wana uwezekano wa kupata na maradhi ya mara Kwa mara kama vile mafua, kikohozi vi homa homa vya kila wakati na magonjwa madogo madogo kwa hiyo ni vizuri kabisa kufanya mazoezi Ili kujiepusha na matatizo mbalimbali kwenye mwili.

 

7. Pia kwa wale wasiofanya mazoezi miili yao huwa mizito na pia mifsuli pamoja na mifupa huwa laini kwa hiyo ni vizuri kabisa kufanya mazoezi Ili kuweza kujiepusha na hali ya kuwepo kwa ulaini kwenye mifupa na misuli 

 

8 . Kwa wale wasiofanya mazoezi jitahidi walau kutafuta kitu chochote cha kukufanyaa utoe jasho kwa sababu mazoezi ni dawa na pia mazoezi ni kinga ni vizuri kabisa kufanya mazoezi.





           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 1893


Sponsored links
👉1 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)     👉2 Kitau cha Fiqh     👉3 kitabu cha Simulizi     👉4 Kitabu cha Afya     👉5 Madrasa kiganjani    

Post zifazofanana:-

Fahamu mtindo mzuri wa maisha
Postei hizi inahusu zaidi mtindo mzuri wa maisha, yaani mtu ale ki vipi au afanyeni nini ili kuweza kuboresha afya yake. Soma Zaidi...

kitabu cha afya
Soma Zaidi...

Kitabu Cha Afya na Lishe
Kupata kitabu hiki download faili la PDF hapo chini na usome bila ya internet. Soma Zaidi...

DONDOO 100 ZA AFYA
Pata dondoo 100 za Afya Soma Zaidi...

Kujiandaa kwa ajili ya kumuona daktari
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu baadhi ya mambo ya kujiandaa kwa ajili ya kumuona daktari Soma Zaidi...

DARASA LA AFYA NA AFYA YA UZAZI
Jifunze mengi kuhusu Afya, kuwa nasi kwenye makala hii hadi mwisho. Soma Zaidi...

AFYA NA MAGONJWA
Pata elimu juu ya afya hapa ukiwa na vitabu vyetu bila ya malipo yoyote Soma Zaidi...

MARADHI YASABABISHWAYO NA HALI ZA MAISHA
Pata elimu juu ya afya hapa ukiwa na vitabu vyetu bila ya malipo yoyote Soma Zaidi...

Dondoo za afya 1-20
Somo Hili linakwenda kukuletea dondoo mbalimbali za afya Soma Zaidi...

Umuhimu wa kuvaa nguo za upasuaji.
Posti hii inahusu zaidi umuhimu wa nguo za upasuaji, tunajua wazi kuwa, wakati wa upasuaji tunapaswa kusafisha chumba na mazingira yake lengo ni kuhakikisha kuwa tunazuia wadudu wasisambae au kuingia kwenye mwili wa binadamu. Soma Zaidi...

Umoja wa mataifa unazungumziaje afya
Somo Hili linakwenda kukueleza kuhusu Mambo ya kiafya yanayozungumzwa na umoja wa mataifa Soma Zaidi...

darasa la afya
Soma Zaidi...