MADHARA YA KUSHINDWA KUPITISHA MKOJO.


image


Posti hii inahusu zaidi madhara ya kushindwa kupitisha mkojo, ni madhara makubwa yanayotokea kwa mtu iwapo akishindwa kupitisha mkojo.


Madhara yanayoweza kutokea iwapo mtu hakutibiwa tatizo la kushindwa kupitisha mkojo.

1.Maambukizi kwenye kibofu Cha mkojo.

Tukumbuke kuwa mkojo unachujwa kutoka sehemu mbalimbali za mwili kwa hiyo mara nyingi mkojo huwa na wadudu na wadudu hao inabidi watolewe nje na wakibaki ndani wanaanza kushambulia sehemu mbalimbali za kibofu Cha mkojo na hatimaye kuleta maambukizi, kwa hiyo hali hii ya kushindwa kupitisha mkojo inabidi ishughulikiwe mara Moja kwa sababu inaweza kuleta maambukizi makubwa kwenye kibofu Cha mkojo na hatimaye kuleta maambukizi ambayo ni makubwa zaidi na hayakutarajiwa.

 

2. Kuharibika kwa figo.

Tunajua kazi za figo kwenye mwili wa binadamu ni kubwa mno kwa hiyo figo likiharibika matatizo mengi utokea kwenye sehemu mbalimbali za mwili wa binadamu, kwa hiyo figo likiharibika mkojo utashindwa kutengenezwa na damu utashindwa kuchuja na mwisho wake mtu asipotibiwa haraka anaweza kupoteza maisha, kwa hiyo tunapaswa kutibu tatizo hili mapema iwezekanavyo Ili kuweza kuepuka madhara makubwa zaidi ambayo yanaweza kujitokeza na tukashindwa kuyatibu kwa hiyo tutibu tatizo dogo Ili tuepuke kuwepo kwa tatizo kubwa baadae.

 

3. Kupungua kwa nguvu ya misuli ya kwenye kibofu Cha mkojo.

Hali hii utokea pale ambapo kibofu Cha mkojo kikijaa kinatuna na kusababisha madhara makubwa kwenye misuli ambayo nayo ulegea iwapo tatizo hili kama halijatibiwa mapema linawza kufanya kibofu Cha mkojo kulegea na hatimaye  kufanya mkojo ukawa unapita bila taarifa kwa hiyo Tunapaswa kuwa makini katika kutibu ugonjwa huu  maana usipotibiwa unaweza kuleta kitu kingine tofauti.

 

4. Kuwepo kwa UTI.

Ugonjwa wa kushindwa kupitisha mkojo kutoka kwenye kibofu unaweza kusababisha UTI kwa mgonjwa hii ni kwa sababu ya maambukizi kwenye kibofu Cha mkojo na wadudu ambao wapo ndani ya mkojo kwa hiyo tunapaswa kutibu tatizo hili iwezekanavyo Ili tuweze kuepuka na janga hili la Ugonjwa wa UTI ambao ni hatari katika maisha ya watu walio wengi.



Sponsored Posts


  ðŸ‘‰    1 Mafunzo ya php       ðŸ‘‰    2 Magonjwa na afya       ðŸ‘‰    3 Hadiythi za alif lela u lela       ðŸ‘‰    4 Maktaba ya vitabu       ðŸ‘‰    5 Jifunze fiqh       ðŸ‘‰    6 Madrasa kiganjani    


Je! una maswali, mapendekezo ama maoni? tuma ujumbe wa meseji SMS hapo chini ili kuunganishwa na muhusika au bofya hapa

SMS SMS



Post Nyingine


image Namna ya kuzuia maambukizi kwenye tumbo na utumbo mdogo
Posti hii inahusu zaidi namna ya kuzuia maambukizi kwenye tumbo na utumbo mdogo, hizi ni njia ambazo zinapaswa kufuatwa ili kutokomeza kabisa maambukizi kwenye tumbo na utumbo mdogo. Soma Zaidi...

image Dalili na ishara za jipu la Jino
Jipu la jino ni mfuko wa usaha unaosababishwa na maambukizi ya bakteria. Soma Zaidi...

image Huduma ya Kwanza kwa aliyepatwa na presha ya kupanda
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu huduma ya Kwanza kwa mtu aliyepatwa na presha ya kupanda Soma Zaidi...

image Njia za kuzuia damu isiendelee kuvuja
Posti hii inahusu zaidi njia za kuzuia damu isiendelee kuvuja, ni njia ambazo utumika ikiwa kuna damu inavuja kwenye sehemu yoyote ya mwili,kwa hiyo tunaweza kutumia njia hizi ili kuepuka kuendelea kuvuja kwa damu. Soma Zaidi...

image Fahamu kuhusu Ugonjwa wa Dengue
Posti hii inahusu zaidi ugonjwa wa Dengue, ni ugonjwa unaosababishwa na virusi ila unasambazwa na mbu kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine mbu anayasambaza Ugonjwa huu kwa kitaalamu huitwa Aedes mosquito . Soma Zaidi...

image Jinsi ya kuepuka minyoo
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu njia za kuiepuka minyoo Soma Zaidi...

image Maandalizi ya mama mjamzito kwa ajili ya kujifungulia.
Postii inafundisha maandalizi ya mama kwa ajili ya kujifungulia hii Ni muhimu Sana kwa wale ambao hawajawahi kujingua Ni mara yao ya kwanza wanatakiwa kujua na kuelewa vifaa na mahitaji kujifungulia na kwa wale wanaohudhuria clinic huwa wanafundisha. Soma Zaidi...

image Faida za Uzazi wa mpango
Posti hii inazungumzia Faida za Uzazi wa mpango kwa watoto, mama, wanandoa, na jamii au JUMUIYA. Soma Zaidi...

image Madhara ya kutotibu Maambukizi kwenye mifupa.
Posti hii inahusu zaidi madhara ya kutotibu Maambukizi kwenye mifupa,ni madhara ambayo utokea endapo Maambukizi kwenye mifupa yasipotibiwa kwa mda wake. Soma Zaidi...

image Dawa mbadala za vidonda vya tumbo
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu dawa mbadala za vidonda vya tumbo Soma Zaidi...