Madhara ya kutotibu maambukizi chini ya kitovu

Posti hii inahusu zaidi madhara ya kutotibu maambukizi chini ya kitovu ni madhara ambayo yanaweza kutokea kwa mgonjwa pale ambapo matibabu yanapokuwa hayatolewi kwa mgonjwa wa maumivu chini ya kitovu.

Madhara ya kutotibu maambukizi chini ya kitovu.

1. Kwanza kabisa mirija ya uzazi inajaa maji.

Kwa sababu ya kuendelea kuwepo kwa maambukizi bila ya matibabu yoyote Kuna hatari ya kujaa maji mirija ya uzazi na maji hayo utoa harufu mbaya na pia maji yakiwa mengi uzuia yao kutembea na hivyo ni rahisi kwa Mama kupata ugumba au mimba kushindwa kushika.

 

2. Pia kuendelea kuwepo kwa maambukizi chini ya kitovu usababisha ongezeko kubwa la maambukizi hali ambayo usababisha kutokukomaa kwa mayai kwenye mfuko wa kizazi ambao kwa kitaalamu huitwa ovaries.

 

3. Kuvimba kwa Kuta za mji wa mimba na mini ya uzazi, kwa kawaida kama Kuna maambukizi ambayo yanafikia kiasi cha kuharibu mji wa mimba na Kuta za uzazi Moja kwa Moja uingilia urutubishaji na pia kama Kuna mimba ni rahisi kutoka.

 

4. Pia maambukizi yanaweza kuhathiri pia  kibofu cha mkojo hali hii utokea pale maambukizi yakisha sambaa kutoka sehemu Moja kwenda nyingine na kusababisha madhara makubwa kwenye kibofu cha mkojo.

 

5. Kwa hiyo tunaona wazi kuwa madhara na matatizo ya kuwepo kwa maambukizi chini ya kibofu cha mkojo usababisha madhara mbalimbali pamoja na ugumba na kuharibu kibofu cha mkojo kwa hiyo ni vizuri kabisa kutibu tatizo Ili kuweza kupunguza madhara yatokanayo kwa sababu ya kuwepo kwa maambukizi chini ya kitovu.



Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2022/07/04/Monday - 05:44:17 pm     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 782


Download our Apps
👉1 Kitabu cha Afya     👉2 Kitau cha Fiqh     👉3 kitabu cha Simulizi     👉4 Madrasa kiganjani    

Post zifazofanana:-