MADHARA YA RIBA KWENYE JAMII


image


Haya ni madhara ya riba katika jamii. Ni kwa namna gani jamii inadhurika kutokana na riba?


8. Tatizo la Riba
Riba ni kupata chochote kile cha ziada kutoka katika mkopo au mtaji bila kushiriki katika faida au hasara. Mwenyezi Mungu anatufahamisha katika Qur’an:

 


Wale wanaokula riba hawasimami ila kama anavyosimama yule ambaye shetani kamzuga kwa kumsawaa; haya ni kwa sababu wamesema, Biashara ni kama riba, hali Mwenyezi Mungu amehalalisha biashara na kuiharamisha riba.(2:275)

 

Mwenyezi Mungu huyafutia (baraka mali ya) riba; na kuyatia baraka (mali iliyotolewa) sadaka (2:2 76).
Madhara ya riba katika jamii

 


(i)Riba inachafua nafsi ya Tajiri na uchumi wake. Tajiri ambaye hayuko tayari kukukopesha mali yake pasi na riba, kamwe hawezi kutoa mali yake bure kuwasaidia wanyonge na wenye dhiki. Tajiri asiye tayari kutoa mali yake kuwasaidia wenziwe wenye dhiki na shida katika jamii huwa mchoyo, bahili, mpupiaji mali, asiyetosheka na utajiri alionao, mfujaji, muonevu na dhalimu. Tajiri mwenye moyo wa namna hii hata kama atajiita Muislamu hawezi kamwe kuchunga mipaka ya halali na haramu katika kuchuma!

 


(ii)Riba inamkandamiza Mnyonge mwenye dhiki. Wanyonge na wenye dhiki katika jamii inayoendesha uchumi wake katika misingi ya riba, hawapati msaada wowote wa bure kutoka kwa matajiri kwa kiasi ambacho wengi wa wale wasiojiweza kabisa kujitosheleza kwa mahitaji muhimu ya maisha yao kwa namna duni sana - wengi hujipatia chakula chao kutoka katika mapipa ya taka (watoto wa mtaani), wengi hujisitiri kwa masalio yaliyookotezwa hapa na pale na wengi makazi yao ni stesheni na sokoni. Hawa, kisaikolojia, hujiona ni watu duni wasio na maana yoyote katika jamii na huwaona matajiri na watu wenye uwezo kuwa ndio wenye maana. Na hapa ndipo inapojengeka chuki baina ya wasionacho kuwachukia walio nacho.

 


(iii) Riba inaharibu uchumi wa jamii na maendeleo yake. Riba na msingi wake wa unyonyaji imma ikitozwa na tajiri mmoja au kikundi cha matajiri, imefanywa msingi wa uchumi wa taifa au wa kimataifa. Kwa bahati mbaya kutokana na mazoea tuliyonayo juu ya vyombo vya uchumi vya kitaifa na kimataifa vinavyoendeshwa katika misingi ya Riba kama vile mabenki ya taifa na shirika la Bima la Kimataifa, baadhi ya watu wamediriki kuhalalisha Riba ya mabenki na Bima. Kuhalalisha huku kwa riba ya mabenki na Bima aidha kumetokana na uzoefu wa uchumi haramu katika jamii zetu au umetokana na kushindwa kuona ubaya wa riba kitaifa au kimataifa.
Waislamu hatuna budi kukumbuka kuwa alichokiharamisha Allah (s.w) kinakuwa ni haramu katika wingi wake na katika uchache wake. Tukichukua mfano wa pombe Mtume (s.a.w.) amesema:

 


Kinacholewesha kikiwa kingi ni haramu pia hata kikiwa kichache. (Tirmidh, Abu Daud, Ibn Majah). Kwa hiyo kilicho haramishwa kwa mtu binafsi, pia ni haramu kwa taifa na ni haramu kwa mataifa yote ulimwenguni. Kwa upande mwingine jambo la haramu litakapotendwa kitaifa litakuwa na athari mbaya zaidi kwa jamii kuliko likitendwa katika kiwango cha mtu binafsi, hali kadhalika jambo baya likitendwa kimataifa huwa na athari kubwa na mbaya zaidi kwa jamii ya mwanadamu kuliko likitendwa katika kiwango cha kitaifa.

 


(iv) Riba ni mali ya dhulma inayonyakuliwa na matajiri kutoka kwa wanyonge kwa njia moja au nyingine kiuchumi, pia riba inaukandamiza na kuudidimiza uchumi wa kitaifa au kimataifa. Mali ya riba kwa kuwa ni mali inayopatikana bila jasho na bila hata ya kushiriki katika mashaka ya uchumi, huwafanya matajiri na wenye uwezo wa kuendesha miradi mbali mbali ya kiuchumi wakae tu bila kazi wakingojea fedha zao zizae katika mabenki ambazo wana kila uhakika wa kuzipata hata itokee gharka ya namna gani. Kwa hiyo kutokana na riba, jamii huwakosa watu wenye uwezo mkubwa wa kuzalisha mali ambao wangaliweza kuendesha miradi mbali mbali ya kiuchumi ambayo ingaliinua uchumi wa taifa na wa kimataifa kwa ujumla.

 


Wataalam wa uchumi wanakiri kuwa riba inaporomosha uchumi. Wamegundua kuwa kadiri kiwango cha riba kinavyokuwa kikubwa ndivyo uchumi unavyozidi kushuka kwa sababu matajiri huona kuwa wanapata faida kubwa zaidi na kwa njia nyepesi isiyotoa jasho lolote wakiweka fedha zao benki kuliko kuziingiza katika miradi ya kiuchumi. Hivyo utaona kuwa riba hupunguza uzalishaji na huongeza gharama za uzalishaji.



Sponsored Posts


  ðŸ‘‰    1 Magonjwa na afya       ðŸ‘‰    2 Madrasa kiganjani       ðŸ‘‰    3 Mafunzo ya html kwa kiswahili       ðŸ‘‰    4 Mafunzo ya php       ðŸ‘‰    5 Maktaba ya vitabu       ðŸ‘‰    6 Jifunze fiqh    


Je! una maswali, mapendekezo ama maoni? tuma ujumbe wa meseji SMS hapo chini ili kuunganishwa na muhusika au bofya hapa

SMS SMS



Post Nyingine


image Swala ya tahiyatul masjidi yaani maamkizi ya msikitini, pamoja na swala za qabliya na baadiya
Post hii inakwenda kukujuza kuhusu swala za qabliya, baadiya na tahiyatul masjid. Soma Zaidi...

image Zijuwe nguzo 17 za swala.
Ili swala itimie utahitajika kutimiza nguzo zake na masharti yake. Hapa utajifunza nguzo 17 za swala. Soma Zaidi...

image Kujitwaharisha kutokana na najisi
Post hii itakufundisha namna ya kutwaharisha Najisi. Soma Zaidi...

image Namna ya kutawadha yaani kuchukuwa udhu
Kuchukuwavudhu ni ibada, lakini pia ni matendo ya kuufanya mwilivuwe safi. Katika post nitakwenda kukifundisha namna ya kutia udhu katika uislamu. Soma Zaidi...

image Swala ya witiri na faida zake, na jinsi ya kuiswali
Hapa utajifunza jinsi ya kuswali swala ya witiri na faida zake kwa mwenye kuiswali. Soma Zaidi...

image Maana ya hadathi na aina zake
Post hii inakwenda kukugundisha maana ya hadathi pamoja na kutaja aina za hadathi Soma Zaidi...

image Hili ndio lengo la kufunga.
Ni kwa nini Allah ametutaka tugunge. Je kuna lengo gani hasa katika kufunga. Soma Zaidi...

image Sunnah za swaumu, sunnah ambazo zinaambatans ns kufungabmwezi wa Ramadhani
Yajuwe mambo ambayo yanapendeza kuyafanya wakati ukiwa umefunga Ramadhani. Soma Zaidi...

image Ni nini maana ya swala
Post hii inakwenda kukugundisha kuhusu maana halisi ya ibada ya swala. Soma Zaidi...

image Siku ambazo haziruhusiwi kufunga
Ni haramu kufunga katika masiku haya. Na endapo utafunga basi funga haitakuwa na malipo. Soma Zaidi...