image

Madhara ya Tiba mionzi

Post hii inahusu zaidi madhara ya Tiba mionzi kwa wagonjwa wa saratani, ni madhara yanayotokea kwa wagonjwa wanaotumia mionzi katika matibabu ya saratani.

1. Kupoteza hamu ya chakula.

Hii ni mojawapo ya madhara ambayo utokea kwa watumiaji wa mionzi kwa sababu ya kuwepo kwa dawa kwenye damu usababisha kuingilia mfumo wa  hamu ya kula kwa hiyo mgonjwa ushindwa kula, kwa hiyo mgonjwa anapaswa kula kidogo kidogo na kwa kila mara na pia anapaswa kula vyakula kama vile supu  na vyakula vingine vilaini Ili aweze kuruhusu dawa kufanya kazi maana dawa bila chakula mambo hayaendi vizuri.

 

2. Mgonjwa usikia uchovu mara kwa mara.

Kwa sababu mionzi uharibifu seli zinazosababisha saratani na vile vile zile ambazo ni nzima nazo uharibiwa na mionzi kwa hiyo  tunajua kabisa maisha yetu msingi wake ni seli kwa hiyo seli zikifa  bila kufikia mda wake na mambo mengine mwilini yanakwama ndo maana mtu uhisi uchovu kwa hiyo wanaotumia mionzi wanapaswa kupumzika kwa mda wa kutosha, kutembea walau dakika Kumi na Tano kwa siku na kunywa maji mengi, kula chakula Cha kutosha Ili kuupatia mwili nguvu.

 

3.Mabadiliko ya ngozi.

Kwa wagonjwa wanaotumia mionzi huwa na mabadiliko kwenye ngozi zao , pengine ngozi ubadilika na kuwa pinki, nyeusi, kuhisi moto kwenye ngozi, ngozi kuwa kavu, kuwasha na ngozi kuwa na upele au malengelenge kwa mgonjwa anayetumia mionzi akiona dalili kama hizi hasiogope Bali achukue dawa za kawaida zinazotumika kutibu magonjwa ya ngozi na pia apate ushauri wa daktari Ili kuweza kujua Cha kufanya maana madhara mengine kwenye ngozi huwa yanatisha na kumnyima mgonjwa amani.

 

4. Mgonjwa huisi kichefuchefu.

Kwa sababu dawa hizi za mionzi  zinaharibu seli na pia uingilia mfumo wa chakula na kumfanya mgonjwa kutaka kutapika kila kitu, kwa hiyo mgonjwa anapaswa kukaa woman Ili asitapike, pia anapaswa kula chakula kidogo kidogo kwa wakati b tofauti na pia anapaswa kujiadhari na vyakula vile ambavyo huwa havipendelei Ili kuepuka kutapika kwa kufanya hivyo mgonjwa ataweza kula chakula na dawa zitaweza kufanya kazi.

 

5. Tukumbuke kuwa mionzi huua seli zinazosababisha saratani na pamoja na zile ambazo ziko kawaida na pia mwili wa binadamu unapaswa kuwa na seli zinatosha Ila kwa sababu ya magonjwa seli zinaharibika kwa mionzi kwa hiyo wagonjwa hawa wanahitaji uangalizi wa karibu na kupewa chakula chenye virutubisho vyote Ili waendelee kuishi na pia jamii inapaswa kuwasaidia na kuwapa ushirikiano wa karibu.





           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 1967


Sponsored links
👉1 Kitabu cha Afya     👉2 Madrasa kiganjani     👉3 kitabu cha Simulizi     👉4 Kitau cha Fiqh    

Post zifazofanana:-

Tiba ya minyoo
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu tiba ya minyoo Soma Zaidi...

Fahamu matumizi ya Dawa iitwayo Aspirin.
Aspirini Ni dawa ya kutuliza maumivu.Majina yanayoaminika zaidi katika kutuliza maumivu sasa yanapatikana kwa njia mbadala inayookoa gharama kwa kutumia Aspirini. Aspirini inayopendwa na familia kwa miongo kadhaa, mara nyingi hutumiwa kupunguza maumivu y Soma Zaidi...

Fahamu kuhusu dawa ya Theophylline katika kutibi mfumo wa upumuaji
Post hii inahusu zaidi dawa ya theophylline ni dawa inayofanya kazi kwenye mfumo wa upumuaji. Soma Zaidi...

Fahamu zaidi kuhusiana na Dawa ya Moyo DIGOXIN
Digoxin ni nini? Digoxin inatokana na majani ya mmea wa digitalis. Digoxin husaidia kufanya mapigo ya moyo kuwa na nguvu na kwa mdundo wa kawaida zaidi. Digoxin hutumiwa kutibu kushindwa kwa moyo. Digoxin pia hutumiwa kutibu mpapatiko wa atiria, ugonjw Soma Zaidi...

Dawa ya fangasi ukeni
Usisumbuliwe tene na fangasi ukeni, zijuwe hapa dalili za fangasi ukeni, tiba yake na njia za kukabiliana na fangasi ukeni Soma Zaidi...

Fahamu kuhusu dawa ya potassium sparing
Post hii inahusu zaidi dawa ya potassium sparing katika matibabu ya magonjwa ya moyo. Soma Zaidi...

Njia zinazotumika Ili kumpatia mgonjwa dawa
Posti hii inahusu zaidi njia kuu nne ambazo utumika kumpatia mgonjwa dawa, Ili kumpatia mgonjwa dawa Kuna njia za kutumia kama ifuayavyo. Soma Zaidi...

Ni dawa gani hatari kwa mjamzito?
Ukiwa mjamzito uwe makini sana katika kuchagua matumizi ya dawa. Vinginevyobinawwza kuwa hatari. Hapa nitakujuza dawa ambazo ni hatari kutumia kwa ujauzito wako. Soma Zaidi...

Chini ya Tumbo langu Kuna uchungu lakini si sana shinda ni ni?
Nini kinasababisha maumivu ya tumbo chini ya kitovu? Soma Zaidi...

Ushauri kabla ya kubeba mimba.
Posti hii inahusu zaidi ushauri kwa akina Mama na wachumba kabla ya kubeba mimba, kabisa ya kubeba mimba akina Mama na wachumba wanapaswa kufanya yafuatayo. Soma Zaidi...

Dawa ya fangasi uumeni
kama unasumbuliwa na fangasi uumeni, nitakujuza dawa yake, sababu za fangasi uumeni, matibabu yake na njia za kuwaepuka Soma Zaidi...

Dawa za kutibu fangasi kwenye kucha
Makala hiii inakwenda kukueleza dawa za kutibu fangasi kwenye kucha. Soma Zaidi...