huu ni muendelezo wa mafunzo ya Database klwa kutumia MySQL na hili ni somo la 11. katika somo hili tutaendelea kujifunza mpangilio wa muonekano wa data kwenye database.
Katika somo lililotangulia tumejifunza amna a kupangilia taarifa za kwenye databse. Tuliona namna ya kutumia ORDER BY. Isha tukapanga data zetu kutoka kubwa kwenda ndogo na kinyume chake. Sasa katika somo hili tutatkwenda kuendelea na nnamna ya kupangilia data hizo ila kwa kutumia WHERE .
Kwa nini tunatumia where ?
Tunatumia WHERE endapo tuna masharti yanatakiwa yafikiwe ili data kuonekanna. Kwa mfano unataka kusoma menu zote ambazo gharama yake ni zaidi ya 1000. hapa hili tunaita ni sharti ama condition. Sasa ili sharti hili liweze kufanya kazi kwenye SQL tunatumia where.
1. Mfano wa kwanza
Tunahitaji kusoma data zote ambazo price yake ni sawa na 1000.
Kufanya hivyo tutatumia alama ya = mbele ya where. Hivyocommand nzima itaonekana.
SELECT * FROM `menu` WHERE price =1000
hapo menu itakayoonekana ni ile tu ambayo proce yake ni sawa na 1000.
2. Mfano wa pili
Tunataka kusoma data ambazo id yake ni 3, 4, na 8. yaani data tu zenye id hizo ndizo tunataka kuziona na si nyinginezo. Hivyo tunatarajia kuwa na row tatu tu. Kufanya hivyo tutatumia OR kwa maana au. Yaani eidha id iwe 3 au id iwe 4 au id iwe 8. Na command yote itaonekana hivi
SELECT * FROM `menu` WHERE id =3 OR id =4 OR id =8; pia unweza kuondoa nyota na kupunguza column
SELECT name, price FROM `menu` WHERE id =3 OR id =4 OR id =8;
3. Mafno wa tatu
Chukulia mfano kwenye menu kuna ugali mbili. Kuna ugali nyama abayo ni 1500 na kuna ugali ng’onda ambaypo ji 1000. sasa mimi nataka kusoma ile ambayo ni ugali nyama ya 1500. kumbuka zote ni ugali na kwenye menu zitanasomeka hivyo hivyo. Ili kuona ya ugali 1500 tu tunatakiwa tutumie AND yaani tuselect ugali lakini kwa ulazima kuwa na id yake iwe 1. ambapo kwenye menu yetu id 1 ni ugali hivyo itakuwa hivi:-
SELECT * FROM menu WHERE name = 'ugali' AND id =1
Kuna jambo hapa unatakiwa ulijuwe. Tunapotumia string (sting ni mkusanyiko wa herufi na namba, rejea mafunzo ya php) value inatakiwa ikae ndani ya alama za kufnga na funguwa semi ‘’ kama ulivyo kwenye mfano 'ugali'.
4. Tofauti ya AND na OR.
Unapotumia AND maana yake ni lazima masharti yafikiwe ili data kuonekana. Ila unapotumia OR hata shart moja likifikiwa data zitaonekana. Kwa mfano kwenye mfano namba 2 hapo hata kama kusingekuwa na id 3 data zingeonekana lakini kama tungetumia AND endapo id tatu isingekuwepo kwenye database yetu data zote zisingesoma.
5. Mfano wa nne
Tunahitaji kusoma menu ambazo tu majina yake yameanziwa na herufi u. chukulia mfano kuna orodha ya majina ya vyakula 50 kwenye hoteli moja kubwa sana. Sasa nataku kuona vyakula vinavyoanziwa na herufi u tu, hapo nikiwa naamini nitaona bei ua ugali kwa haraka zaidi tofauti na kuanza kusoma kutoka kwanzo hadi mwisho.
Kufanya hivi tutatumia LIKE kisha tutaweka hiyo heru u kikifuatiwa na alama ya asilimia %. na ikiwa unahitaji kufatuta menu iliyoishiwa na herufi u basi alama ya asilimia % utaiweka mwanzo mfano %u. mfano huu pia utaweza kuutumia kama unataka kusearch kitu kwenye database ambacho kinaanziwa na herufi fuani. Hivyo kulingana na mfano wetu command itakuwa hivi:-
SELECT * FROM menu WHERE name LIKE 'u%'
Tutajifunza zaidi somo hili tutakaposoma namna ya kutafuta kitu kwenye database. Hila unaweza kutumia mfano huu pia kutafuta kitu kama mpangilio hapo unavyouona. Mfano unataka kutafuta neno supu utaweka ‘supu%’
6. Mfano wa tano
Kwa kutumia SQL pia unaweza tumia mathematical operation kama >, <, !=, == na nyinginezo. Hapa nitatumia < na >. kwa ufupi > humaanisha kubwa kuliko na < humaanisha ndogo kuliko. Hapa nitatuia mifano miwili tu ya > na < .
A. Tunahitaji kuona menu ambazo price zake ni kubwa kuliko 1000 hapa tutatumia > .hivyo menu itakayokuja ni ile tu ambayo price yake imezidi 1000. hivyo itakuwa hivi
SELECT * FROM menu WHERE price >1000
B. Tunataka kuona menu ambazo price yake ni ndogo kuliko 900. hapa tutatumia <, hivyo menu tutakazoona ni zile tu ambazo price yake haijafika 900. hivyo itakuwa hivi:-
SELECT *FROM menu WHERE price <900
Tukutane somo la 12 tutajifunza kanuni kadhaa za kihesabu kwa kutumia SQL. Tafadhali usikose somo la 12 kwani ndio somo letu la mwisho wa course hii ta mafunzo ya database kwa kutumia MySQl.
Mafunzo haya yamekujia kwa Ihsani ya bongoclass
Web: www.bongoclass.com
Email: mafunzo@bongoclass.com
Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetuUmeionaje Makala hii.. ?
Katika somo hilivutajifunza namna ya kutumia HTML form. Namna ya kuookea taarifa kutoka kwenye madodoso ya html form.
Soma Zaidi...Mafunzo ya database kwa utumia software ya MySQL kwa lugha ya kiswahili na hili ni somo la 7.
Soma Zaidi...hili ni somo la pili katika mfululizo wa mafunzo haya ya php level 1 na hapa utajifunza namna ya kuandika faili klako la kwanza la php.
Soma Zaidi...Somo la 10 mafunzo ya php level 1. Katika somo hili utajifunza kuhusu condition statement.
Soma Zaidi...Ktika somo hili la 7 utajifunza namna ya kuandaa na kujiandaa kutengeneza website ama blog. Pia utajifunza maandalizi ya kuhost
Soma Zaidi...Karibu tena katika mafunzo haya ya html level 2 na hili ni somo la 5. Katika somo hili utajifunza zaidi kuhusu kuweka style kwenye html file.
Soma Zaidi...Haya ni mafunzo ya HTML kwa wanaoanza level ya kwanza, na hili ni somo la kwanza katika masomo 8 yatakayokujia katika mtiririko wa course hii.
Soma Zaidi...somo hili la 4 katika mafunzo ya PHP level 1 utajifunza aina za data mabazo php inakwenda kuzitumia.
Soma Zaidi...haya ni mafunzo ya HTML level 2 kwa wenye kuanza. Mafunzo haya ni muendelezo wa level 1 html. Katika course hii utajifunza mengi zaidi lu;iko level1 pia tutazidi kuboresha project yetu.
Soma Zaidi...Somo la pili katika mafunzo ya HTML level 2. Katika somo hili utajifunza maana ya HTML pamoja na historia yake fupi.
Soma Zaidi...