Huu ni mwendelezo wa mafunzo ya DATABASE kwa kutumia MySQL na hili ni somo la pili. Hapa tutakwenda kuona kwa ufupi ni nini DATABASE
SOMO LA PILI:
LENGO LA MAFUNZO HAYA KWA UJUMLA:
Lengo la mafunzo haya ni kukuwezesha kutumia database kwenye bloga ama website yako. Pia uweze kutumia database kwa ajili ya Android App ama web App. Pia utaweza kutumia database kwa ajili ya kudhibiti taarifa zako.
Ni nini maana ya DATABASE?
Data base ni neno la kiingereza ambalo ukilileta kwa kiswahili ni mkusanyiko wa taarifa zilizopangiliwa na kuhifadhiwa na huweza kupatikana katika mfumo wa kielectronic. Taarifa hizi zinakuwa katika majedwali (table).
SQL ni nini?
SQL ni lugha ya kikompyuta ambayo hutumika katika udhibiti wa database. Lugha hii yenyewe hutumiaka kwenye server. Je unajuwa ni nini maana ya server? Pitia somo la kwanza mafunzo ya PHP.
SQL ni kifupisho cha maneno ;- Structured Query Language. Hii ndio lugha ya kikompyuta ambayo inahusika katika kuthibiti database kama kufuta taarifa, kuedit na kuongeza ama kupunguza.
Ni ni Databae management System (DBMS)
Hizi ni software ambazo zimetengenezwa kwa ajili ya kudhibiti taarifa kwenye database. Mifano ya software hizi ni kama:-
Software hizi ndizo ambazo zinatumia lugha ya SQL kwa ajili ya kutumia database. Chukulia mfano php ni lugha ya kikompyuta lakini haiwezi kufanya kazi mapaka kuwe na server pamoja na software ya php. Hivi ndivyo na SQL inafanya kazi kwenye server na inahitahi software.
MySQL
Katika masomo yetu haya tutatumia MySQL, kwa kuwa ni free, pa inatumiaka sana kuliko hizo nyingine. Pia ni rahisi kuitumia. Unaweza kuipata kwa kutumia simu ama kompyuta.
SQL inaweza kufanya nini?
Mahusiano ya PHP na SQL
SQL na MySQL
Kwa watumiaji wa kawaida MYySQL inatosha kuitumia hata kama hijui SQL lakini ili kuweza kudhibiti vyema database utahitaji kuzungumza kwa lugha hii ya SQL kwenye MySQL ili kudhibiti database. SQL ni lugha ya kikompyuta kama ilivyo PHP lakini MySQL ni software ambayo hutumia SQL kwa ajili ya kudhibiti database.
Je wajuwa kuwa:
“Katika siku za mwanzoni mwa facebook ilihitaji PHP, SQL na MySQL kwa ajili ya kudhibiti database yote ya facebook”. kwa mchanganyiko wa HTML, JAVASCRIPT, CSS unaweza kufanya makubwa.
Tukutane somo la Tatu tutakapoanza kujifunza hasa kuhusu hiii SQL na sheria zake. Na vipi utaweza kuitumia. Hakikisha somo la kwanza umelipitia vyema na umeweza kuandaa kifaa chako vyema.
Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu
Umeionaje Makala hii.. ?
katika somo hili la tano kwenye mafunzo ya HTML level 1 utajifunza jinsi ya 1.Kuweka picha 2.Kuweka rangi 3.Kuweka linki 4.Kupangilia position na alignment ya maandishi 5.Kuongeza ukubwa wa herufi 6.Kukoment
Soma Zaidi...Mafunzo ya database kwa utumia software ya MySQL kwa lugha ya kiswahili na hili ni somo la 7.
Soma Zaidi...Somo la nane mafunzo ya php, katika somo hili utajifunza kuhusu array na jinsi ya kutengeneza array.
Soma Zaidi...Huuu ni muendeleo wa mafunzo ya database kwa lugha ya kiswahili, na hili ni somo la nane. Katika somo hli utajifunza namna ya kuweka taarifa kwenye database, kuzfuta na kuziediti yaani kuzifanyia marekebisho.
Soma Zaidi...Hapa utajifunza utofauti kati ya php constant na variable. Na hili ni somo la nane katika mfululizo wa masomo haya ya php level 1.
Soma Zaidi...Huu ni mwendelezo wa mafunzo ya database na jinsi ya kutengeneza bloga na website na hili ni somo la tatu. hapa utajifunza jinsiya kutengeneza database yako kwa mara ya kwanza.
Soma Zaidi...haya ni mafunzo ya database kwa kutumia MySQl na hili ni somo la 9. katika soo hili utajifunza namna ya kusoma ama kutumia taarifa zilizomo kwenye DATABASE.
Soma Zaidi...hili ni somo la pili katika mafunzo ya HTML level 2 html full course for beginners. Katika somo hili tutaangalia utangulizi juu ya HTML na pia utajifunza faida za HTML.
Soma Zaidi...Huu ni muendelezo wa mafunzo ya DATABASE kwa kutumia software ya MySQL na hili ni somo la tano. katika somo hili utajifunza type of data yaani aina ya taarifa ambazo unaweza kuzihifadhi kwenye database yako.
Soma Zaidi...Hili ni somo la nne katika mafunzo ya html basic level. Hapa tutakwenda kuona jinsi ya kuzifanyia kazi tag ambazo umejifunza katika somo lililotangulia.
Soma Zaidi...