image

Mafunzo ya database MySQL - DATABASE somo la 6

Huu ni muendelezo wa mafunzo ya database kwa kutumia MySQL na hili ni somo la 6. Katika somo hili tutakwenda kuona jinsi ya kutengeneza table kwa kutumia MySQL na kwa kutuma SQL.

JINSI YA KUTENGENEZA TABLE KWENYE DATABASE

Katika somo la tano tuliona aina za data ambazo tunakwnda kuzitumia kwenye DATABASE hivyo katika somo hili tutakwenda kuona jinsi ya kutengeneza jedwali au table kwa ajili ya kuhifadhia data.

 

Kabla ya kuanza somo nataka uelewe vyema tunaposema tadatase table tunamaanisha nini hasa. Kama umeshawahi kutumia microsoft access bila shaka umetambuwa namna ambavyo table inavyofanya kazi. Kama ndio kwanza osijali , somo hili ni kwa ajili yako.

 

Kwanza chukulia mfano una excel document yako, ambayo ina majina ya wanafunzi na ya wazazi wao. Hivyo utahitaji kuwa na colum kama tatu hivi. Colum ya kwanza ni namba, ya pili ni jina la mwanafunzi na ya tatu ni jina la baba. Sasa excel yako mathalani itakuwa na wanafunzi 45 hivyo kwenye colum ya namba itaanzia moja hadi 45 kwa kulingana na idadi ya wanafunzi. Na hivyo hivyo colum ya majina nayo italingana na namba. Sasa faili kama hili kwenye database ndio huitwa table.

 

Yaani kwa ufupi table tunaweza taarifa ambazo zinafanana kwenye database. Mfano database ni ya shule ina madarasa. Hivyo kila darasa utaliandikia table yake, ambayo mfano wake ni sawa na kuwa na kila darasa na faili lake la excel ila zote ni za wanafunzi wa shule ambalo ndio itakuwa database yako.

 

 

Wacha nikupe mfano mwingine huwenda ukafahamu zaidi. Chukulia tunataka kuhifadhi post zetu kwenye database. Hivyo tutatakiwa ktengeneza table ambayo itakuwa na namba ya post, kichwa cha habari cha post, muhtasari wa post, maudhui ya post, picha, aliyechapisha na tarehe. Wacha nikwambie kitu, angalia post kwenye blog utaona zina vitu hivyo, tarehe, aliyechaposha, muhtasari, maudhui yenyewe, na kichwa cha habari.

 

Sasa taarfa kama hiyo tutahitaji kuwa na table ambayo itahifadhi taarifa hizo kwa kila post. Kwa mujibu wa mfano huo table yetu itakuwa na colum 7. hizi kwenye database wakati wa kutengeneza table tutaziita field. Hivyo tunaasema table yetu itakuwa na field 7. ili tupunguze urefu wa maneno wacha tutumie kingereza. Field zetu ni id, titlle, summary, content, image, publisher, date.

 

Ufupi wa maneno ni kuwa ndani ya database taarifa huhifadhiwa kwenye table. Hivyo database moja inaweza kuwa na table hata 100 ama zaidi. Na kila table huhifadhi taarifa zinazofanana ndio maana zinawekwa pamoja. Ok sasa somo letu litakwenda kukufundisha namna ya kutengeneza hizo table.

 

Jinsi ya kutengeneza table kwenye MySQL

Hapa tutatumia MySQL na pia tutatumia SQL command. Jambo la kwanza unalotakiwa ulijuwe ni kuwa utambuwe aina za data zako unazotaka kuziweka pia ujuwe length ya kila data je unataka ihifadhi character ngapi. Kama tulivyoona katika somo lililotangulia kuwa kila aina ya ata ina idadi ya character zake.

 

Kwanza tengeneza database na iite blog. Baada ya hapo ifunguwe hiyo database utaona kunasehemu pameandikwa CREATE TABLE IF NOT EXISTS. Darasa letu litaanzia hapo. Kama umefika hapo fuata hatuwa zifuatazo:-

1. Funguwa database

2. Utaona sehemu pameandika CREATE TABLE IF NOT EXISTS na jini kuna kabosi

3. Weka jina la table hapo weka post

4. Kuna palipoandika number of columns hapo weka 7 idadi ya colum zetu kama ilivyo kwenye maelezo hapo juu

5. Boyya GO

 

6.Utaona ukurasa mpya ambao una vijumba vingivingi lakini ukivihesabu kwa kwenda chini utaona ni 7 kama ulivyoweka hapo mwanzo.

 

7. Cheki kuna palipoandika name kisha msururu wa vijumba unafata kuelekea chini. Hapo unatakiwa ujaze majina ya kila colum kulingana na maelezo ambayo tumeona hapo juu. Hivyo tutajaza kuanzia na id, kisa kijumba kinefuata ni title kisha kinachofuata ni summarty kisha kinachofuata utajaza contente, kisha ujtajaza image kisha publisher kisha date.

 

8. Kisha angalia juu kulia kwa name kuna type. Hapo utajaza kila colum ulioandika jina unataka uchukuwe data za aina gani? Kwa mfano id kwa kuwa inaonyesha namba za post hivyo itakuwa inachukuwa data za namba ambazo ni INT. Title kwa kuwa ni herufi hii unaweza kuipa VARCHAR, kisha summary hii kwa kuwa ni text na zinaweza kuwa nyingi zipe MEDIUMTEXT. Halafu content kwa kuwa ni text ambazo zinaweza kuwa nyingi ipe TEXT, kisha image hapa kama utaupliad kupitia database ipe blob, ila kwa sasa hatutafanya kitu hizo tutatumia link ya image hivyo ime VARCHAR. Kisha publisha pia ni herufi na ni chache sana ipe CHAR. Kisha kwenye date ipe DATE.

 

9. Jaza kwa umakini taarifa hicho kwa kuchaguwa kutoka kwenye kibosi. Hakuna sehemu ya wewe kuandika.

 

10. Kisha pembeni ya type kule juu utaona palipoandikwa Length/Values hapa sasa utajaza idadi ya character unazotaka zikae kwenye kila colum. Hapo kwenye INT weka hata 10, character za namba zikiwa 10 ni linamba kubwa sana chukulia mfano 1000,000,000 hizi character zipo 10 hii ni bilioni moja, hivyo length ya character 0 ni kubwa sana ambapo sio rahisi kuijaza. Kwenye title ekwa 255 ambapo character 255 ni title kubwa sana. Mfano bongoclass neno hili lina character 10 tu. Kwenye summary na content wacha hivyohivyo maana ni vigumu kukadiria , lakini ukitaka unaweza kuweka hata 5000. kwenye image hapo kwa kuwa tutatumia link za image unaweza kuweka hata 255, kwenye publisher weka hata 100. na kwenye date wacha kama palivyo.

11. Jaza hizo taarifa vyema kabisa

 

12. Juu pembeni ya length utaona kuna palipoandikwa default, hapo utajaza kama kuna taarifa unataka ziwepo tayari. Kwa sasa waccha kama palivyo. Pembeni ya default kuna palipoandika coalition hapa unakwenda kujaza taarifa kuhusu character set ipi unataka itumke kwa kila colum. Kwa sasa wacha kama palivyo yenyewe itajaza UTF-8 ambayo ndio standard. Kisha pembeni tena kuna palipoandikwa attributes hapa utaweza attrubutes za kila colum kwa saa wacha kama palivyo. Kisha pembeni kuna null na index pia wacha kama palivyo. Hapa pendewe panaangalia kama kuna colum unataka ziwe NUll na index kama unataka ziwepo kwenye search.

 

Pembeni tena kuna A_I maana yake autoincrement. Hizi ni taarifa ambazo zitakuwa zinajijaza automatiki. Kwa mfano ID yenyewe kwa kuwa nni namba ya kila daatifa hivyo unaweza kuweka ijijaze yenyewe. Kama ndivyo basi weka tiki kwenye kijumba kidogo chani nywenye colum ya id, hapo chini ya neno A_I. kisha pembeni kuna comments hapo utaweka comment kuhusu hiyo column.

 

13. Kufikia hapo utakuwa umeshajaza taafifa muhimu hivyo bofya SAVE ipo kwa chini.

14. Mpaka kufikia hapo table yako itakuwa imesha tengenezwa.

 

KUTENGENEZA DATABASE TABLE KWA KUTUMIA SQL

Sasa nitakufunsisha namna ya kutengeneza table kwa kutumia SQL. Tutakwenda kutengeneza table yenye jina menu. Hii ni menu ya blog yetu, au category ya blog tutakayoitengeneza. Hivyo fuata hatuwa zifuatazo:-

  1. Ingia kwenye uwanja wa SQL
  2. Andika CREATE TABLE IF NOT EXISTS
  3. Kisha weka jina la table ambalo ni menu hivyo itakuwa hivi
  4. CREATE TABLE IF NOT EXISTS menu
  5. Kisha weka mano ( ambapo itakuwa hivi
  6. CREATE TABLE IF NOT EXISTS menu (
  7. Ndani ya bano tutaweka majina ya colum pamoja na character length. Sasa tujaalie table yetu itakuwa na column 2 tu ambazo ni id na title. Id ni kwa ajili ya kuorodhecha item kwenye menu na title ni uonyesha jina la item.  Lenth za character zitakuwa ndani ya mabano kisha kufuatawa na alama ya koma ila item ya mwiho hutakiki kuweka koma (,) Ukimaliza utafunga bano kuu la mwanzo kisha utamaliza na alama ya semicoloni (;) Angalia mfano wake hapo chini

CREATE TABLE IF NOT EXISTS menu (

id int (10),

title varchar(255)

);

 

8. Ukimaliza bofya GO

9. Kufikia hapo utakuwa umeshatengeneza table mpya inayoitwa menu kwenye database yake. Hivyo database yetu ya blog ina table 2 ambayo ni post na menu.

 

Somo linalofata tutakwenda kujifunza namna ya kufuta table na kuedidi pamoja na kuingiza data kwenye database. Hivyo hakikisha somo hili umelielewa kabla ya kuingia somo linalofata.

 

Mafunzo haya yanakujia kwa Ihsani ya BONGOCLASS

Web: www.bongoclass.com

Email: mafunzo@bongoclass.com

 





           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Topic: Tehama Main: Post File: Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 1151


Sponsored links
👉1 Simulizi za Hadithi Audio     👉2 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)     👉3 Kitabu cha Afya     👉4 Madrasa kiganjani     👉5 kitabu cha Simulizi     👉6 Kitau cha Fiqh    

Post zifazofanana:-

Mafunzo ya database MySQL database somo la 9
haya ni mafunzo ya database kwa kutumia MySQl na hili ni somo la 9. katika soo hili utajifunza namna ya kusoma ama kutumia taarifa zilizomo kwenye DATABASE. Soma Zaidi...

Mafunzo ya HTML level 1 somo la 7 (HTML basic level FOR BEGINNERS)
Hii ni project ya HTML ambayo imetengenezwa kulingana na mafunzo ya HTML level1. Tunatarajia project hii kuboreshwa kadiri mafunzo yanavyozidi kusonga mbele. Soma Zaidi...

PHP level 1 somo la tisa (9).
Somo la nane mafunzo ya php, katika somo hili utajifunza kuhusu array na jinsi ya kutengeneza array. Soma Zaidi...

PHP level 1 somo la nane (8)
Hapa utajifunza utofauti kati ya php constant na variable. Na hili ni somo la nane katika mfululizo wa masomo haya ya php level 1. Soma Zaidi...

Mafunzo ya php level 1 somo la tatu (3)
hili ni somo la tatu katika masomo ya php level 1. Hapa utajifunza zaidi kuhusu variable na namna ya kuitengeneza. Soma Zaidi...

Mafunzo ya php level 1 somo la pili (2)
hili ni somo la pili katika mfululizo wa mafunzo haya ya php level 1 na hapa utajifunza namna ya kuandika faili klako la kwanza la php. Soma Zaidi...

PHP level 1 somo la kumi (10)
Somo la 10 mafunzo ya php level 1. Katika somo hili utajifunza kuhusu condition statement. Soma Zaidi...

Mafunzo ya database MySQL somo la 3
Huu ni mwendelezo wa mafunzo ya database na jinsi ya kutengeneza bloga na website na hili ni somo la tatu. hapa utajifunza jinsiya kutengeneza database yako kwa mara ya kwanza. Soma Zaidi...

Mafunzo ya HTML level 1 somo la 4 (HTML basic level FOR BEGINNERS)
Hili ni somo la nne katika mafunzo ya html basic level. Hapa tutakwenda kuona jinsi ya kuzifanyia kazi tag ambazo umejifunza katika somo lililotangulia. Soma Zaidi...

Mafunzo ya database MySQL - DATABASE somo la 6
Huu ni muendelezo wa mafunzo ya database kwa kutumia MySQL na hili ni somo la 6. Katika somo hili tutakwenda kuona jinsi ya kutengeneza table kwa kutumia MySQL na kwa kutuma SQL. Soma Zaidi...

Mafunzo ya HTML Level 2 somo la 5 (HTML FULL COURSE FOR BEGINNERS LESSON 5)
Karibu tena katika mafunzo haya ya html level 2 na hili ni somo la 5. Katika somo hili utajifunza zaidi kuhusu kuweka style kwenye html file. Soma Zaidi...

Mafunzo ya HTML kwa wenye kuanza (basic level)
Huu ni utangalizi wa mafunzo ya HTML kwa wenye kuanza level ya kwanza kwa lugha ya kiswahili. Haapa utapata msingi wa kuweza kutengeneza tovuti na blog. Soma Zaidi...