Mafunzo ya hadithi zilizochaguliwa
Sunnah na hadithi (EDK form 3: dhana ya elimu ya uislamu)
7.2. Mafunzo ya Hadith Zilizochaguliwa.
- Hadith ya Kwanza; Kuamrisha mema na Kukataza Maovu.
Kutoka kwa Abi Saidil-Khudhur (r.a) amesema: Nimemsikia mjumbe wa Mwenyezi Mungu anasema;
“Mwenye kuuona uovu miongoni mwenu na auondoshe kwa mkono wake, ikiwa hawezi (na aondoshe) kwa ulimi wake iwapo hawezi (na aondoshe) kwa moyo wake (achukie) na hiyo ndiyo imani dhaifu.”
(Ameipokea Muslim).
Hatua za kuondosha uovu:
- Hatua ya kwanza na bora ni kuondosha kwa mikono.
- Hatua ya pili kwa ubora ni kuondosha kwa kusema.
- Na hatua ya mwisho na dhaifu ni kuchukia moyoni.
Mafunzo ya Hadith kwa Ufupi:
- Ni wajibu kuondosha maovu kwa kisaidizi chochote kile kiwacho kulingana na mazingira.
- Jukumu la kuamrisha mema na kukataza maovu linaanzia kwa mtu mmoja mmoja na ummah kwa ujumla
- Kutochukia uovu na kuridhika nao ni dalili ya kukosa imani moyoni.
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
👉1 kitabu cha Simulizi 👉2 Madrasa kiganjani 👉3 Simulizi za Hadithi Audio 👉4 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w) 👉5 web hosting 👉6 Dua za Mitume na Manabii
Post zinazofanana:
Dua Sehemu ya 01
Zijue fadhila za kuomba dua, tambua umuhimu na mahimizo juu ya kuomba dua?
Soma Zaidi...Dua Ambazo Hazirudi: Dua Zenye Kujibiwa kwa Haraka Zaidi
Katika dini ya Kiislamu, kuomba dua ni ibada kubwa na njia ya moja kwa moja ya kuwasiliana na Allah (S.W.T). Hata hivyo, kuna nyakati, mazingira, na hali za watu fulani ambazo Mtume Muhammad (صلى الله عليه وسلم) ametuhakikishia kuwa dua zao hazirudi nyuma na ni zenye kujibiwa kwa haraka sana.
Soma Zaidi...Nafasi ya Elimu na wenye elimu katika Uislamu
Nafasi ya elimu na mwenye elimu katika uislamu inaonkana katika maeneo yafuatayo: Kwanza, Elimu ndio takrima ya kwanza aliyokirimiwa mwanaadamu na Mola wake.
Soma Zaidi...