hili ni somo la pili katika mafunzo ya HTML level 2 html full course for beginners. Katika somo hili tutaangalia utangulizi juu ya HTML na pia utajifunza faida za HTML.
HTML FULL COURSE FOR BEGINERS
Kaributena katika mafnzo ya HTML na jinsi ya kutengeneza blog na website. Somo hili litakwenda kukupeleka zaidi kwenye ujuzi wa kujuwa kutengeneza website ambayo ipo katika ubora na muonekano mzuri. Uendeshwaji wa masomo yetu haya ni kujifunza kwa vitendo. Kila somo litakujia na video yake. Pia mwisho wa course utashiriki kufanya project kulingana na somo husika. Katika mlolongo huu wa mafunzo haya tutaangalia namna ya kumzawadia ambaye ataleta project iliyo nzuri kuliko wengine. Sharti iendane na masomo yaliyofundishwa.
NITAFAIDIKA VIPI NIKIJIFUNZA HTML?
Kwa kuwa utakuwa umeongeza elimu hiyo pia ni faida. Lakini hzi ni faida tu ambazo utaweza kuzipata:-
1.Utaweza kutengeneza website (wavuti) yako mwenyewe kwa kucode na si kwa kutumia onlineplatform ambapo hutakuwa na umiliki na data zako.
2.Itakuwa rahisi kujifunza lugha nyingine za kikompyuta kama javascript, na php.
3.Html hutumika katika kupangilia muonekano wa blog na website hata kama unatumia onlineplatform kama blogger na wordpress
4.Kwa anayetaka kumanage database HTML itamsaidia katika kupangila muonekano wa taarifa hizo akisaidia na mchanganyiko wa lugha nyingine kama php n.k
5.Html hutumika katika kutengeneza Android App na Web App.
JE HTML PEKEE INATOSHA KWAWEBSITE?
Ndio inatosha kama hutojali kuweka mbwembwe. Angalia website ya kwanza kwenye link hii http://info.cern.ch/hypertext/WWW/TheProject.html ukiangalia kwa uzuri utagunduwa kuwa website ya kwanza imetengenezwa kwa HTML.
KWA NINI UJIFUNZE PAMOJA NASI.
Kuna maeneo mengi ambayo unaweza kujifunza hizi mabo ikiwemo youtube. Lakini kwa nini ninakushauri ujifunze pamoja nasi? Ni kwa sababu:-
1.We work on real project. Mwisho wa kila course tunafanya project ambapo kila mshiriki atashiriki katika kukamilisha project yake akiwa na msaada wa kundi kubwa nyuma yake.
2.Tunajifunza kwa kushirikiana kwa pamoja. Yaani utashiriki mafunzo haya moja kwa moja na wenzio, tauliza swali na kujibiwa ndani ya muda mfupi.
3.Utajifunza kulingana na kifaa chako. Huna ulazima wa kuwa na kompyuta ndio ujifunze code.
MUDA WA COURSE HII
Madomo haya yatakuchuwa muda usiozidi wiki mbili kwa kuskoma. Yaani mwisho ni vipindi 15 huwenda visifike. Inaamaana utajifunza ndani ya wiki 2 utafanya project.
VIGEZO VYA KUSHIRIKI MAFUNZO HAYA:
1.Uwe na simu janja (smartphone) au kompyuta
2.Uwe na uwezo wa kujuwa kusoma na kuandika
3.Uwe mjanja
JE NAHITAJIKA KULIPA?
Hapana, hutahitajika kulipa hata kkidogo katika mafunzo haya. Hata hivyo kama utahitaji kujifunza zaidi nje ya mafunzo haya yes malipo yatafanyika kwa gharama nafuu.
JINSI YA KUANDAA KOMPYUTA YAKO AMA SIMU KWA AJILI YA SOMO:
1.Kwa watumiaji wa simuingia playstore andika TrebEdit itakuja Appkisha download au tumia link hii https://play.google.com/store/apps/details?id=com.teejay.trebedit. Funguwa App, bofya menu, kisha bofya palipoandika workspace kisha bofya alama ya + kutengeneza project mpy. Kisha new project andika jina la folda weka website2, kisha save. Ukiwa ndani ya folda jipa ulilotengeneza bofya alama ya + kisha new folder andika image kisha save.rudi nyima ukiwandani ya folda la websitee bofya alama ya + kisha new file kisha weka jina andiak index.html kisha save. Funguwahilo faili la index.html, futa code ama maandisho yote utakayoyakuta kama yapo, copy code hizo hapochini kisha pest hapo kwenye faili lako. Ukifika hapo upo tayari kuanza somo. Angalia video link yake ipo chini hapoitkusaidia.
2.Kwa watumiaji wa kompyuta funguwa notepad, ama notepadplus ama sublimetext3. unaweza kudowload bure ila kwa notepad haina haja ya kudownload ipo kwenye kompyuta yako. Kwanza tengeneza folder lipe jina website2.kisha ndani ya folder hilo tengeneza folda jingine lipe jina imae. Rudi kwenye folda la website2 Tengeneza faili jipya kisha pest code hizo hapo chini kwenye faili lako.save as andika jina index.html. Lifunguwe faili lako la index.html kwakutumia browser kama chrome litafungukakama website. Angalia video itakusaidia. Unaweza kudownload notepadplus hapa https://notepad-plus-plus.org/downloads/v8.1.4/
CODE ZENYEWE NI HIZI HAPA:
<!DOCTYPE html>
<html>
<head>
<title>My First Webpage</title>
<meta charset="UTF-8">
<meta name="description" content="This is my first website">
</head>
<body>
<h1>Welcome to my webpage</h1>
<p>Welcome to my brand new website.</p>
<a href="http://www.google.com">Google</a>
</body>
</html>
Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu
Umeionaje Makala hii.. ?
Ktika somo hili la 7 utajifunza namna ya kuandaa na kujiandaa kutengeneza website ama blog. Pia utajifunza maandalizi ya kuhost
Soma Zaidi...haya ni mafunzo ya database kwa kutumia MySQl na hili ni somo la 9. katika soo hili utajifunza namna ya kusoma ama kutumia taarifa zilizomo kwenye DATABASE.
Soma Zaidi...Karibu kwenye mafunzo ya PHP level 1 na hili ni somo la kwanza. Hapa utajifunza maana ya php, inavyofanya kazi pamoja na historia yake kwa ufupi
Soma Zaidi...Hili ni somo la pili katika mfululizo wa mafunzo ya html level ya 1 na hapa tutakwenda sasa kunanza somo letu rasmi, kwani katika somo la kwanza umejifunza jinsi ya kuandaa kifaa chako kwa ajili ya mafunzo.
Soma Zaidi...Huu ni muendelezowa mafunzo ya database kwa kutumia MySQl na hili ni somo la 12. katika somo hili tutajifunza namna ya kufanya mahesabu kwa kutumia SQl katika database
Soma Zaidi...Huu ni utangalizi wa mafunzo ya HTML kwa wenye kuanza level ya kwanza kwa lugha ya kiswahili. Haapa utapata msingi wa kuweza kutengeneza tovuti na blog.
Soma Zaidi...Katika somo hili la 6 mafunzo ya HTML level 2, tutajfunza namna ya kugawa ukurasa wa wavuti wa html.
Soma Zaidi...Katika somo hilivutajifunza namna ya kutumia HTML form. Namna ya kuookea taarifa kutoka kwenye madodoso ya html form.
Soma Zaidi...Hii ni project ya HTML ambayo imetengenezwa kulingana na mafunzo ya HTML level1. Tunatarajia project hii kuboreshwa kadiri mafunzo yanavyozidi kusonga mbele.
Soma Zaidi...Huu ni muendelezo wa mafunzo ya DATABASE kwa kutumia software ya MySQL na hili ni somo la tano. katika somo hili utajifunza type of data yaani aina ya taarifa ambazo unaweza kuzihifadhi kwenye database yako.
Soma Zaidi...