picha

Mafunzo ya php level 1 somo la nne (4)

somo hili la 4 katika mafunzo ya PHP level 1 utajifunza aina za data mabazo php inakwenda kuzitumia.

SOMO LA NNE

TYPE OF DATA IN PHP:

Kabla ya kuendelea mbele zaidi katika somo la PHP sasa kwanza lazima tujuwe aina za data ambazo tunakwenda kuzitumia kwenye php. Kila taarifa tunayotaka kuitumia aka kuionyesha lazima tujuwe ipo katika aina ipi ya data. Hii itakusaidia wewe katika kupanga actions. Pia katika kuweka fomu za madodoso.

 

Kwa ufupi katika php kuna aina kuu 7 za data ambazo tutakwenda kuziangalia.

  1. Sting
  2. Interger
  3. Float
  4. Boolean
  5. Array
  6. Object
  7. NULL

 

1. STRING

String ni mkusanyiko wa herufi ama character. Mfano “hello” “I am a student”. Katika PHP string huwekwa ndani ya alama za semi yaani alama za kunukuu ambazo ni “ “. hata hivyo pia unaweza kuchaguwa eidha utumie alama ya kunukuu moja ama mbili mfano ‘ ’  au “ “. mfano wa string kwa alama moja ‘hello’   mfano wa string kwa alama mbili “hello”. pia string inaweza kuwa na mchanganyiko wa herufi, namba na character nyingine. Angalia mifano hapo chini.

 

2. INTEGER

Aina hii ya data ni zile data zote ambazo ni namba tu. Pia zinatakiwa ziwe namba ambazo hazina desimali. Pia integer zinaweza kuwa nmaba ambazo ni positive ama negative. Kitu cha kuzingatia hapa ni kuwa integer haitakiwi iwe na desimali. Mfano 6353

 

3. FLOAT

Hizi ni data ambazo ni namba zilizo na desimali ama exponent. Mgano 23.9

 

4. BOOLEAN

Hizi ni data ambazo hutumika katika kujaribu hali. Hizi zinaitwa condition test. Bolean zipo katika namna mbili ambazo ni TRUE au FALSE.

 

5. ARRAY

Hizi ni data ambazo zinahifadhi taarifa zaidia ya moja kwenye variable. Kwa mfano inaweza kuzungumzia variable miti kisha ikaendelea kutaja aina za mita ambayo itahusika kwenye variable hiyo moja.

 

6. OBJECT

Object ni aina ya data ambayo inahifadhi taarifa na namna ambavyo taarifa hiyo itachakatwa. Tutajifunza zaidi kwenye masomo yajayo.

 

7. NULL

Katika php data ambayo ni null ni data maalumu ambayo inakuwa na thamani moja tu a,bayo ni NULL. Na variable yake inakuwa tu. N endapo umeweka variable na hukuweka kuwa itafanya nini amba itatoa thamani ya kitu gani, basi automatic variable hii hubadilishwa kuwa NULL.

 

 

JINSI YA KUJUWA AINA YA DATA KATIKA PHP:

Ili uweze kujuwa aina ya data iliyotumika huwa tunatumia var_dump(). hii ni function ambayo hutumika katika kuonyesha aina ya data iliyotumika kwenye php. Angalia mifano hapo chini:-

 

Mfano 1:

<?php

$a = 7635262;

Var_dump ($a);

?>

Hapa utapata matokeo haya int(7635262) hii inamaana kuwa namba hizo ni integer ambayo ndio aina ya data iliyotumika

 

Mfano 2:

<?php

$a = "hello piga *112#";

Var_dump ($a);

?>

 

Hapa iakuletea: string(16) "hello piga *112#" hii inamaana kuwa data nilizotumia kwenye mfano huu ni string, ambazo ni mkusanyiko wa herufi, namba na alama kama * na #. hiyo 16 hapo ina maanisha kuwa string iliyotumika ina character 16.

 

 

Mfano 3:

<?php

$a = 626.9;

Var_dump ($a);

?>

 

Hii itakuletea matokeo: float(626.9) inamaana kuwa aina ya data iliyotumika ni float ambayo ni namba zenye desimali na exponent.

 

Mfano 4:

<?php

$mti = array("mpera", "muembe", "mchungwa", "mlimao");

Var_dump($mti);

?>

 

Hii itakupa matokeo array(4) { [0]=> string(5) "mpera" [1]=> string(6) "muembe" [2]=> string(8) "mchungwa" [3]=> string(6) "mlimao" }  hii inamaana kuwa data iliyotumika ni array ambayo ndani yake kuna string 5.

 

Mfano 5:

<?php

$a = '';

$a = null;

Var_dump($a);

?>

Hii itakupa matokeo kuwa NULL

 

Tutajifunza zaidi katika viindi vijavyo, tutajifunza zaidi juu ya hizi aina za data. Tutaangalia namna ya kutumia string katika uandishi.

 

Mafunzo haya yanakujia kwa ihsani ya bongoclass

Web: www.bongoclass.com

Email:mafunzo@bongoclass.com

Phone: 0774069753 unaweza kunicheki wasap kwa link hii https://wa.me/message/7CTQP5BSWBR5I1

 

 

Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu
Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

       
Author: Rajabu image Tarehe: 2024-05-10 14:53:23 Topic: Tehama Main: Post File: Download PDF Views 1203

Share On:

Share follows: 0 | Unique share links followed: 0
Sponsored links
👉1 Kitau cha Fiqh     👉2 Madrasa kiganjani     👉3 Bongolite - Game zone - Play free game     👉4 Kitabu cha Afya     👉5 Tafasiri ya Riyadh Swalihina     👉6 ai web app    

Post zinazofanana:

Mafunzo ya DATABASE - MySQL somo la 7

Mafunzo ya database kwa utumia software ya MySQL kwa lugha ya kiswahili na hili ni somo la 7.

Soma Zaidi...
PHP level 1 somo la tano (5)

Haya ni mafunzo ya php na hili ni somo la tano. Katika somovhili utajifunza namna ya kutengeneza functions.

Soma Zaidi...
Mafunzo ya HTML Level 2 somo la 3 (HTML FULL COURSE FOR BEGINNERS LESSON 3)

Hili n somo la tatu katka muendelezo wa mafunzo ya HTML LEVEL 2 kwa lugha ya kiswahili. Mafunzo haya yanakujia kwa Ihsani ya bongoclass

Soma Zaidi...
Mafunzo ya HTML Level 2 somo la 4 (HTML FULL COURSE FOR BEGINNERS LESSON 4)

Karibu tena katika somo la nne la mafunzo ya HTML level2 html full course for beginners. Katika somo hili utajifunza kuhusu attributes na namna zinavyofanya kazi

Soma Zaidi...
Mafunzo ya Database MySQL DATABASE somo la 2

Huu ni mwendelezo wa mafunzo ya DATABASE kwa kutumia MySQL na hili ni somo la pili. Hapa tutakwenda kuona kwa ufupi ni nini DATABASE

Soma Zaidi...
Mafunzo ya HTML Level 2 somo la 7 (HTML FULL COURSE FOR BEGINNERS LESSON 7)

Ktika somo hili la 7 utajifunza namna ya kuandaa na kujiandaa kutengeneza website ama blog. Pia utajifunza maandalizi ya kuhost

Soma Zaidi...