image

Mafunzo ya php level 1 somo la pili (2)

hili ni somo la pili katika mfululizo wa mafunzo haya ya php level 1 na hapa utajifunza namna ya kuandika faili klako la kwanza la php.

SOMO LA PILI:

Tulishaona katika somo lililopita namna ya kuandaa kompyuta yako na simu yako kwa ajili ya kufunguwa php. Kwa maelezo yaliotangulia katika somo la kwanza uliweza kuandaa simu ama kompyuta yako kuwa server. Katika somo hili tutakwenda kujifunza tag za php na jinsi zinavyofanya kazi.

 

Php ni tofauti sana na html huwenda ni kwa sababu ni lugha mbili tofauti. Hata hivyo html ina mamia ya tag kama tulivyojifunza katika mafunzo ya html level ya kwanza na pili. Php ina tag chache.  Katika mafunzo ya HTML pia tulijifunza kuwa kuna tag za kufungulia na kufungia.

 

TAG ZA PHP

Php hufunguliwa na tag . huwenda hizi ndio tag pekee za php zinazotumika katika kucode php. Tag hizi pia unaweza kuzifupisha kwa mfano

 

 

?>

 

Au

 

?>

 

ECHO  na PRINT

Ili kuweza kuandika kitu na kionekane kama tulivyotumia kwenye html, basi php inatumia echo na print. Hizi ni statement mbili za php ambazo hutumika ili kuweza kuleta matokeo kwenye browser. Yaani unapoandika code za php zinachakatwa kwenye server, kisha matokeo yake hutolewa kwenye browser kama plain teext (maandishi ya kawaida) kisha html hufanya kazi yake ya kupangilia. Sasa ili kupata haya matokeo ya code za php ambapo mtumiaji wa mtandao ataona ndipo tunatumia hizi echo na print.

 

Mfano katika html unapotaka kuandika neno “hallo”  ili lionekane na mtumiaji wa ukurasa huo utatumia tag mfano

hallo

. sasa katika php utaanza tag za php ya kufunga na kufunguwa ambazo ni

echo “hello”;

?>

 

Kwa kutumia print

print “hello”;

?>

 

Echo na print sio tag, katika php hizi zinaitwa statement. Tutajifunza zaidi kuhusu statement katika masomo mengine.  Kwa ufupi ni kuwa echo na print zinafanya kazi sawa ijapokuwa utofauti wao ni mdogo. Kwa mfano echo ipo fasta katika kuleta matokeo kuliko print. Echo pia inatumika katika kuleta matokeo kutoka katika parameta zaidi ya moja. Hivyo ijapokuwa zote zinafanana ila zina utofauti mdogo.kama huna uhakika ipi utumie vyema kutumia echo.tutajifunza utofauti wao zaidi katika masomo yajayo.

 

HTML NA PHP

Php na html zote hutumika katika kutengeneza ukurasa wa wavuti. Katika faili ya html unaweza kutumia php na katika faili la php pia unaweza kutumia html. Ipo hivi browser yako inapokutana na tag za html itachakata na kuleta matokeo na ikikutana na tag ya php inapeleka mchakato kwenye server kisha server ikirudisha text ndipo inatoa matokeo. Mfano:-

 

Html ndani ya php

echo “

hello”>

 

?>

 

Au unaweza kutumia hii:-

print “

hallo

 

 

Pia unaweza kuandika code za html nje ya tag za php katika faili la php mfano

echo “hello”

?>

 

hello

 

 

PHP NDANI YA HTML

Kama ilivyo ndani ya php file unaweza kuandika html hivyo hivyo unaweza kuandika php ndabi ya faili la html. Unaweza kueka code za php kwenye html tag ama nje ya html tag. Mfano

 

 

 

 

 

 

 

Kwa mfano huu code zote za php zilizopo ndani ya

zitafuata style hiyo. Unaweza pia kutumia php kwenye faili la html nje nje ya tag za html na ikaleta matokeo.

 

 

 

NAMNA YA KUWEKA COMMENT KWENYE PHP

Tumejifunza kwenye html kuwa kukoment ni kwamba unaandika kumbukumbu zako katika code kwamba ili uweze kukumbuka amba mtu mwingine aweze kujuwa kwa urahisi kuwa msitari huo wa code unahusu nini. Komenti hazionekani kwa mtumiaji ijapokuwa zipo kwenye code.

 

Katika html tulujifunza kuwa ukitaka kukoment unatumia

 

Ila katika php utatumia // kisha utakomeny. Ama utatumia # kisha itakoment. Namna hii ya kukoment ni pale unapokoment kwa maneno yasiozidi msitari mmoja. Na kama unataka kukoment sana utatumia /* kisha utakomenta halafu utafunga kwa */ mfano:

//hallo

#hallo

?>

Au kama unataka kukoment misitari mingi

/* hello

Hii ni

Koment

*/

?>

 

Endelea kufanyika kazi zaidi somo hili, kwani somo linalofata litakuhitaji uwe umeweza angalau kujuwa tag za php.

 

Somo linalokuja tutakuja kuangalia namna ya kutumia variable, na kuonyesha matokeo.

 

Mafunzo haya yanakujia kwa ihsani ya bongoclass

Web: www.bongoclass.com

Email:mafunzo@bongoclass.com

Phone: 0774069753 unaweza kunicheki wasap kwa link hii https://wa.me/message/7CTQP5BSWBR5I1





           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 915


Sponsored links
πŸ‘‰1 kitabu cha Simulizi     πŸ‘‰2 Kitau cha Fiqh     πŸ‘‰3 Madrasa kiganjani     πŸ‘‰4 Kitabu cha Afya    

Post zifazofanana:-

Mafunzo ya HTML Level 2 somo la 4 (HTML FULL COURSE FOR BEGINNERS LESSON 4)
Karibu tena katika somo la nne la mafunzo ya HTML level2 html full course for beginners. Katika somo hili utajifunza kuhusu attributes na namna zinavyofanya kazi Soma Zaidi...

Utangulizi wa Android App Development
Haya ni mafunzo ya muda mfupi katika kujifunza hasa ujuzi wa kutengeneza Android App hata kama haujui kitu kuhusiana na Android Development Soma Zaidi...

Mafunzo ya php level 1 somo la kwanza (1)
Karibu kwenye mafunzo ya PHP level 1 na hili ni somo la kwanza. Hapa utajifunza maana ya php, inavyofanya kazi pamoja na historia yake kwa ufupi Soma Zaidi...

Mafunzo ya HTML level 1 somo la 2 (HTML basic level FOR BEGINNERS)
Hili ni somo la pili katika mfululizo wa mafunzo ya html level ya 1 na hapa tutakwenda sasa kunanza somo letu rasmi, kwani katika somo la kwanza umejifunza jinsi ya kuandaa kifaa chako kwa ajili ya mafunzo. Soma Zaidi...

Mafunzo yz database MySQL database somo la 12 (final)
Huu ni muendelezowa mafunzo ya database kwa kutumia MySQl na hili ni somo la 12. katika somo hili tutajifunza namna ya kufanya mahesabu kwa kutumia SQl katika database Soma Zaidi...

Mafunzo ya DATABASE MYSQL na SQL somo la 1
Karibu tena katika mafunzo yetu, na huu ni mwanzo wa mafunzoya DATABASE kwa kutumia MYSQL kwa lugha ya kiswahili. Na hili ni somo la kwanza, katka somo hili utajifunza jinsi ya kuandaa kifaa chako kwa ajili ya mafunzo. Soma Zaidi...

Mafunzo ya database mySQl database somo la 11
huu ni muendelezo wa mafunzo ya Database klwa kutumia MySQL na hili ni somo la 11. katika somo hili tutaendelea kujifunza mpangilio wa muonekano wa data kwenye database. Soma Zaidi...

Mafunzo ya Database MySQL database somo la 10
Huu ni muendelezo wa mafunzo ya Database kwa kutumia MySQL na hili ni somo la 10. katika somo hili tutakwenda kuendelea namna ya kupangilia muonekano wa data zako kwenye database. Soma Zaidi...

Mafunzo ya php level 1 somo la tatu (3)
hili ni somo la tatu katika masomo ya php level 1. Hapa utajifunza zaidi kuhusu variable na namna ya kuitengeneza. Soma Zaidi...

Mafunzo ya DATABASE kwa kutumia MySQL DATABASE kwa kiswahili somo la 4
Huu ni mwendelezo wa mafunzo ya database kwa kutumia MySQL na hili ni somo la nne katika mlolongo wa masomo haya. Katika somo hili utajifuza jinsi ya kubadili jina la database na kufuta database. Pia tutajifunza kutumia SQL kufanya hayo. Soma Zaidi...

Mafunzo ya HTML level 1 somo la 6 (HTML basic level FOR BEGINNERS)
hili ni somo la sita katika mfululizo wa mafunzo ya HTML level 1. Katika somo hili tutajifunza mambo makuu matatu ambayo ni kuweka menyu, kuweka background color na kufanya faili lako liwe responsive. Soma Zaidi...

Mafunzo ya HTML Level 2 somo la 3 (HTML FULL COURSE FOR BEGINNERS LESSON 3)
Hili n somo la tatu katka muendelezo wa mafunzo ya HTML LEVEL 2 kwa lugha ya kiswahili. Mafunzo haya yanakujia kwa Ihsani ya bongoclass Soma Zaidi...