Mafunzo ya php level 1 somo la tatu (3)
hili ni somo la tatu katika masomo ya php level 1. Hapa utajifunza zaidi kuhusu variable na namna ya kuitengeneza.
SOMO LA TATU
NAMNA YA KUWEKA VARIABLE
Variable ni moja katika kitu mihimu kwenye faili la php. Huwezi kuunganisha tovuti yako kwenye database, huwezi kuzifikia data kwenye database bila kutumia variable. Huwezi kuweka function bilakutumia variable. Kwa ufupi php inazungumza kwa kutumia variable.
Variable ni nini?
Ni ngumu kutoa maana ya hili neno likafahamika bila maswali, ila niseme tu kwa ufupi variable unaweza kuwema ni chombo cha kuhifadhia data kwenye program. Unaweza kuzikusanya data nyingi zinazofanana kwa kutumia variable moja.
Kwa mfano unaweza kusema neno gari likawa na mgawanyiko kama toyota, benzi, basi na pikap. Sasa badala ya kuyaida majina yao unaweza tu kuweka variable ya gari hala fu compyuta ikadisplay magariyote. Badala ya kuanza tena kutaja, majina ya magari unaweka variable gari yanakuja yote.
Cheki mfano huu:
<?php
$gari = array("basi", "benzi", "toyota","tractor", "isuzu");
echo "tunauza magari aina ya ". $gari[2].",". $gari[1].".";?>
Kwa kutumia variable gari naweza kutaja vina la gari lolote kati ya hayo bila ya kuandika jina lake halisi. Hii inasaidia kusave time.
Kanuni za kuweka variable
- Kwanz aunatakiwa uanze na alama ya dola ambayo ni $
- Kisha utaandika jina la variable usianze na namba
- Kisha ruka nafasi kisha weka alama ya =
- Kisha weka alama za kunukuu “ ”
- Ndani ya alama za kunukuu andiak thamani ya variable yako, yaani unataka variable hiyo iwakilishe nini?
- Weka alama ya semi colon ambayo ni ;
- Baada ya hapo ni kuitumia variable yako.
Mafano 1
<?php
$chakula = "ugali wa sembe iliyonyeupe na samaki wa bwawani pamoja na kachumbari yenye ndimu nyingi";
echo " napenda kula $chakula";
?>
Kw akutumia mfano huu, baada ya kuyaudia maneno yaliyopo kwenye variable ambayo ni “ugali wa sembe iliyonyeupe na samaki wa bwawani pamoja na kachumbari yenye ndimu nyingi” sasa badala ya kuyaridia rudia nitatumia neno chakula kisha maneno hayo yatatolea. Haijalshi nimeyarudia mara ngapi.
Mfano 2
<?php
$a = "kaka";
$b = "mama";
$c = "baba";
$d = "shamba";
echo "$a, $b, na $c wamekenda $d kulima mihogo";
?>
Hapa utaona sentensi hii inasomeka kaka, dada na baba wamekwenda shamba kulima mihogo. Kwa kutumia variable hakuna haja ya kuandika tena kaka, dada na baba.
Unaweza kutumia variable kwenye elementi za HTML na kuleta matokeo kulingana na element ya HTML iliyotumika na style ambazo zimetumika. Angalia mfano namba 3 hapo chini:-
Mfano 3
<?php
$a = "kaka";
$b = "mama";
echo "
<h1><b>hiini hadithi ya $a na $b </b><h1>";
?>
Katika sentenzi hii hii hadithi ya kaka na baba, tag ya HTML <h1> na <b> zitatumika kuifanya sentensi iwe heading 1 na kuwa bolded.
Unaweza pia kutumia variable kufanyia hesabu, angalia mfano wa nne hapo chini
Mfano 4
<?php
$e = "5";
$f = "7";
$g = "5";
echo $e + $f;
echo "<br>";
echo $f * $g;
?>
Hapa utapata jibu la hesabu ya kwanza
5 + 7 ambalo ni 12
Na hesabu ya pili ambayo ni
7 * 5 ambalo ni 35
Kwa ufupi hivi ndivyo variable zinavyoweza kuhifadhi taarifa katika gaili la php. Ttajifunzamengi zaidi kuhusu variable katika masomo yanayokuja.
LINE BREAK KWENYE PHP
Katika html tulijifunza kuwa tag ya <br> ndio hutumika kukata msitari. Katika php endapo utaitumia tag hii inaweza kukupa error. Hivyo ili uweze kuitumia unatakiwa uiweke ndani ya echo ama print. Angalia mfano namba tano hapo chini
Mfano 5
<?php
echo "hi my budy are you drinking?";
echo "<br><br>";
echo "welcome at bongoclass";
?>
Hapo kama <br> itakuwa nje ya echo faili halitaweza kufunguka. Katika masomo yanayofata tujifunzapia namna ya kuongeza space zaidi ya moja kwenye php.
Mafunzo haya yanakujia kwa ihsani ya bongoclass
Web: www.bongoclass.com
Email:mafunzo@bongoclass.com
Phone: 0774069753 unaweza kunicheki wasap kwa link hii https://wa.me/message/7CTQP5BSWBR5I1
Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetuUmeionaje Makala hii.. ?
Share On:
👉1 Simulizi za Hadithi Audio 👉2 Bongolite - Game zone - Play free game 👉3 Dua za Mitume na Manabii 👉4 Kitau cha Fiqh 👉5 Tafasiri ya Riyadh Swalihina 👉6 Madrasa kiganjani
Post zinazofanana:
Mafunzo ya database MySQL somo la 3
Huu ni mwendelezo wa mafunzo ya database na jinsi ya kutengeneza bloga na website na hili ni somo la tatu. hapa utajifunza jinsiya kutengeneza database yako kwa mara ya kwanza.
Soma Zaidi...PHP level 1 somo la sita (6)
Katika somo hili la php level 1 somo la 6 utajifunza namna ya kutumia tarehe yaani function date() kwenye PHP
Soma Zaidi...Mafunzo ya HTML level 1 somo la 3 (HTML basic level FOR BEGINNERS)
Hili ni somo la Tatu katika mfululizo wetu wa mafunzo ya HTML kwa basic level kwa wanaoanza kujifunza. Hapa tutakwenda kujifunza tag za html ambazo huwa zinatumika katika uandishi.
Soma Zaidi...PHP level 1 somo la kumi na mbili (12) final
Mafunzo ya php level 1 somo ka 12 mwisho wa mafunzo. Hapa utaona project ambazo unaweza kufanya kutokana na mafunzo haya.
Soma Zaidi...Mafunzo ya DATABASE - MySQL database somo la 8
Huuu ni muendeleo wa mafunzo ya database kwa lugha ya kiswahili, na hili ni somo la nane. Katika somo hli utajifunza namna ya kuweka taarifa kwenye database, kuzfuta na kuziediti yaani kuzifanyia marekebisho.
Soma Zaidi...Mafunzo ya HTML kwa wenye kuanza (basic level)
Huu ni utangalizi wa mafunzo ya HTML kwa wenye kuanza level ya kwanza kwa lugha ya kiswahili. Haapa utapata msingi wa kuweza kutengeneza tovuti na blog.
Soma Zaidi...