Mafunzo yatokanayo na maandalizi ya mtume ki-wahay
Bara arabu zama za jahiliyyah (EDK form 2 dhana ya elimu ya uislamu)
Mafunzo yatokanayo na Maandalizi ya Mtume (s.a.w) Kimafunzo
(Ki-wahay).
- Elimu katika fani zote (isipokuwa uchawi) ndio nyenzo kuu katika maandalizi kuusimasha Uislamu katika jamii.
- Kisimamo cha usiku kufanya ibada, ni katika nyenzo kuu ya pili katika maandalizi ya kusimamisha Uislamu katika jamii.
- Kusoma Qur’an kwa mazingatio kwa lengo la kuifanya muongozo pekee wa maisha pia ni maandalizi ya kuutawalisha Uislamu katika jamii.
- Kumtaja na kumtukuza Allah (s.w) vilivyo, pia ni katika nyenzo na maandalizi katika kuusimamisha Uislamu ndani ya jamii.
- Kujitupa kwa Allah (s.w) kwa kweli – ni kumcha Allah (s.w) peke yake ukweli wa kumcha, nayo ni katika maandalizi ya kusimamisha Uislamu.
Rejea Qur’an (3:102).
- Kumfanya Allah (s.w) ndiye mlinzi pekee na kumtegemea, ni jambo la muhimu katika kusimamisha Uislamu katika jamii.
- Kusimama na kuonya (kulingania Uislamu), ni jambo muhimu sana linalowezesha Uislamu kufahamika kwa watu.
- Kutakasa (kutwaharisha) nguo ni amri ya Allah (s.w) inayomtaka kila mlinganiaji wa Uislamu kuwa safi wa kuigwa kimwili na kiroho pia.
Rejea Qur’an (41:33).
- Kupuuza na kujitenga na mabaya na wabaya ni jambo la muhimu ili kukataza kwake maovu kuwe na athari.
- Kufanya ihsani (wema) kwa ajili tu kwa ajili ya kutafuta radhi za Allah (s.w) ndio uhai wa ibada ya muislamu.
- Kufanya subira kwa ajili ya Allah (s.w) ni katika nyenzo kuu katika kupelekea kuusimamisha Uislamu katika jamii.
- Utekelezaji wa ujumbe wa Qur’an ni kazi nzito na yenye kila aina ya misukosuko, hivyo kuwa na subira ndio nyenzo pekee.
- Mtume (s.a.w) Kuulingania Uislamu Makkah kwa siri.
- Mtume (s.a.w) alianza kulingania familia yake, kisha rafiki zake na jamaa zake wa karibu walio rafiki.
- Mtume (s.a.w) alianza kulingania Uislamu kwa siri kwa muda wa miaka mitatu kwa kukutana na waislamu waliosilimu mwanzo kabisa katika nyumba ya bwana Arqam bin Arqam – maarufu kama Darul-Arqam.
- Mtume (s.a.w) kuutangaza Uislamu Makkah kwa jamii nzima.
- Baada ya miaka mitatu ya kuulingania Uislamu kwa siri, aliamrishwa kuutangaza sasa hadharani kwa jamii yote inayomzunguka.
- Mara tu baada ya Mtume (s.a.w) kuutangaza ujumbe wa Uislamu hadharani, alikumbana na Upinzani dhidi ya ujumbe wake huo kutoka kwa Makafiri wa Kiqureish wa Makkah.
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
👉1 web hosting 👉2 Kitau cha Fiqh 👉3 Kitabu cha Afya 👉4 Madrasa kiganjani 👉5 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w) 👉6 kitabu cha Simulizi
Post zinazofanana:
Kuandaliwa kwa Muhammad wakati na baada ya kupewa utume
Bara arabu zama za jahiliyyah (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu)
Soma Zaidi...HISTORIA YA MTUME DHUL-KIFL(A.S)
Mtume Dhul-kifl ananasibishwa na Ezekiel anayetajwa ndani ya Biblia.
Soma Zaidi...Mbinu za Da’wah Alizotumia Nuhu(a.s)
Katika kufikisha ujumbe huu kwa watu wake Nuhu(a.
Soma Zaidi...