MAFUNZO YATOKANAYO NA UPINZANI WA MAQURAISH DHIDI YA UISLAMU


image


Bara arabu zama za jahiliyyah (EDK form 2 dhana ya elimu ya uislamu)


Mafunzo yatokanayo na Upinzani wa Maquraish dhidi ya Uislamu (Qur’an).

  1. Upinzani wa Makafiri dhidi ya ujumbe wa Uislamu upo nyakati na muda wote na hautaisha.

 

  1. Hatuna budi kuufikisha ujumbe wa Uislamu kwa kuanzia familia, ndugu na jamaa zetu wa karibu kabla ya wengine ili kupata wasaidizi wa karibu.

 

  1. Waislamu hawana budi kuwa tayari na kutokata tamaa katika kuusimamisha Uislamu bila ya kumchelea yeyote yule.

 

  1. Makafiri siku zote wako tayari kutumia kila mbinu na njia kuhakikisha kuwa wanabaki katika utawala na itikadi za ibada zao ili kuendeleza na kuimarisha maslahi yao kupitia unyonyaji na ukandamizaji.  

 

  1. Mbinu za Makafiri za kutaka kuuhilikisha Uislamu na waislamu zinafanana katika zama zote za historia ya maisha ya mwanaadamu.

 

  1. Mtume (s.a.w) na maswahaba wake waliweza kuhimili vitimbi vya makafiri na hatimaye kuweza kuusimamisha Uislamu katika jamii ni baada ya wao kufuata na kutekeleza kikamilifu mafunzo ya Qur’an (96:1-5), (73:1-10) na (74:1-7).

 

  1. Suala la kuulingania na kuutangaza ujumbe wa Uislamu ni zito, lenye misukosuko na gharama kubwa ya kutoa mali na nafsi (uhai).

 

  1. Siku zote makafiri na maadui wengine wa Uislamu hawakotayari kuona Uislamu unasimama katika jamii na waislamu wanautekeleza vilivyo.

 

  1. Tusitarajie matunda ya kusimama Uislamu kupatikana kwa muda mfupi na kwa urahisi, kwani linahitaji mipango ya muda mrefu na kujitoa muhanga.

 

  1. Wakati wowote Waislamu watakapojizatiti katika kuulingania na kuupigania Uislamu kwa mali na nafsi zao, Allah (s.w) atawapa nusura dhidi ya maadui wao.

Rejea Qur’an (61:8, 10-13).



Sponsored Posts


  ðŸ‘‰    1 Mafunzo ya php       ðŸ‘‰    2 Magonjwa na afya       ðŸ‘‰    3 Mafunzo ya html kwa kiswahili       ðŸ‘‰    4 Madrasa kiganjani       ðŸ‘‰    5 Hadiythi za alif lela u lela       ðŸ‘‰    6 Jifunze fiqh    


Je! una maswali, mapendekezo ama maoni? tuma ujumbe wa meseji SMS hapo chini ili kuunganishwa na muhusika au bofya hapa

SMS SMS



Post Nyingine


image Mji wa Makkah na kabila la kiqureish
Bara arabu zama za jahiliyyah (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

image Sanda ya mwanamke na namna ya kumkafini
Mambo ya faradh kwa maiti ya muislamu (EDK form 2: Dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

image Kuamini vitabu vya mwenyezi Mungu (s.w)
Nguzo za Imani (EDK form 2: Dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

image Waislamu wanaolazimika kufunga
Nguzo za uislamu (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

image Zoezi la 5
Maswali mbalimbali kuhusu fiqih Soma Zaidi...

image Maana ya kuamini malaika katika maisha ya kila siku
Nguzo za imani (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

image Namna lengo la zakat linavyofikiwa
Nguzo za uislamu (EDK form 3:dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

image Uandishi wa hadithi wakati wa maswahaba wa mtume (s.a.w)
Sunnah na hadithi (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

image Kuandaliwa kwa Muhammad wakati na baada ya kupewa utume
Bara arabu zama za jahiliyyah (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

image Kusimamisha swala.
Kwenye kipengele hiki tutajifunza maana ya swala ni nin?. Na masharti ya swala. Soma Zaidi...