image

Magonjwa madogo madogo kwa Mama wajawazito.

Posti hii inahusu zaidi magonjwa madogo madogo kwa akina Mama wajawazito, ni magonjwa ambayo hayawezi kupelekea kupoteza maisha kwa Mama mjamzito, magonjwa haya upotea ikiwa Mama atajifungua.

Magonjwa madogo madogo kwa Mama wajawazito.

1. Kizungu Zungu na kutapika.

Ni mojawapo ya magonjwa kwa mama wajawazito ambayo hayawezi kupoteza maisha ya mama kwa hiyo hali huu umpata Mama akiwa na wiki nne mpaka kumi na sita, hasa hasa hali hiii utokea wakati wa asubuhi kwa akina Mama wengi na kwa wengine utokea mda wote, hali hii usababishwa na homoni za mimba ambazo ni progesterone, oestrogen na chorionic gonadotropin .

 

2. Na kwa wakati mwingine harufu ya chakula usababisha mama kubwa na kichefuchefu na kutapika kwa hiyo  wauguzi na wataalam wa afya wanapaswa  kuongea na Mama ili kuona hali huu ni ya kawaida kabisa na akina Mama wanapaswa kuambiwa ukweli kabisa na kuepuka woga usio na Maana kuhusu hali hii ya kuhisi kichefuchefu na kutapika.

 

3. Kuhisi maumivu kwenye kiuno na kwenye mgongo, hali huu uwapata akina Mama wakati wa ujauzito kwa sababu ya uzito wa mtoto anapoongezeka na anapobadilika mkao kwa hiyo Mama uhisi maumivu na pengine miguu kufa ganzi  kwa hiyo Mama anapaswa kufanya mazoezi, kunyoosha miguu kwa sentimita ishilini na tano, pia anaweza kutumia dawa ya vitamini B complex na calcium na pia Mazoezi ni lazima kwa kina Mama wajawazito.

 

4. Pia Mama wajawazito huwa wanakojoa mara kwa mara kwa sababu kibofu cha mkojo na uterus vimekaribiana sana kwa hiyo mtoto anakandamiza kibofu cha mkojo na kila mkojo unaoingia kwenye kibofu utolewa mara moja kwa hiyo Mama uonekane anakojoa Mara kwa Mara, pia kwa sababu ya mabadiliko ya kimwili kwa Mama mjamzito pengine uhisi kiu na kunywa maji mengi na baadae kuokoa sana, kwa hiyo wajawazito wanapaswa kuelewa kubwa huu si ugonjwa ila ni hali inayotokea na baadae ulisha baada ya kujifungua.

 

5. Na pia wajawazito wana hali ya kusikia ganzi kwenye mikono na vidole na pia kusikia vitu vinachoma kama vile pini na sindano huu ni kwa sababu ya maji maji ambayo kwenye nevu kwa hiyo Mama anapaswa kuweka mikono yake kwenye mito na kuvaa nguo raini wakati wa usiku, hali huu kwa wajawazito ni kawaida na wasiogope na uisha tu baada ya kujifungua, na wakati mwingine wajawazito ushindwa kutulia kwa sababu ya kukua kila siku kwa mtoto aliyeko tumboni.

 

6.Kuongezeka kwa kiasi au spidi ya damu kwenye uterus usababisha mtoto kutembea sana  ambapo hali hii usababisha mama kulala sana na kuwahi kusinzia mapema wakati wa jioni, pia Mama  kwa wakati mwingine uhisi wasiwasi pindi anapofikilia kujifungua kwa wakati huu Mama uhitaji mda mwingi wa kupata ushauri na kufarijiwa kuona kubwa ni hali ya kawaida. Kubadilika kwa homoni pia usababisha Mama kuwa mzito na kupata mawazo mengi sana. Kwa hiyo wauguzi wanapaswa kumwambia Mama kubwa akijifungua hali utapotea tu.

 

7. Tunaona wazi kuwa akina Mama wakati wa ujauzito kuna mabadiliko mengi ambayo utokea kwa hiyo jamii inayowazunguka kuanzia kwa mme, watoto, ndugu na jamii kwa ujumla kuwavumilia wajawazito na kuwapa ushirikiano wa hali na mali kuna pengine wahisi kukwazika waone kuwa ni hali ya kawaida ambayo ujitokeza na kuanza kuwaonyesha upendo kuwadhamini na kuwaelewa kwa kipindi chote cha ujauzito kwa hiyo kwa wale wanaowatesa wahawazito na kuonyesha kuwa maudhi yanayotokea kwao ni kuwa wanajifanyisha wapigwe marufuku na wapewe elimu kuhusu wajawazito wakati wa ujauzito.





           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 1629


Sponsored links
👉1 Madrasa kiganjani     👉2 Kitau cha Fiqh     👉3 Kitabu cha Afya     👉4 kitabu cha Simulizi    

Post zifazofanana:-

Dawa ya chango na dawa maumivu ya tumbo la hedhi
Nitakujiza dawa ya chango na maumivu ya tumbo lahedhi, dalili zake na njia za kukabiliana na maumivu ya tumbo la chango. Soma Zaidi...

Dalili kuu za mwanzo za mimba changa, kuanzia siku ya kwanza
Ni ngumu ila nitakujuza namna ya kuitambuwa mimba ya siku moja hadi 3, mimba ya wiki moja na mimba ya miezi mitatu kwa dalili. Soma Zaidi...

Mabaka yanayowasha chini ya matiti.
Posti hii inahusu zaidi mabaka yanayowasha chini ya matiti, ni ugonjwa ambao uwapata wanawake walio wengi na wengine hawajapata jibu Sababu zake ni zipi na pengine uchukua hatua za kutumia miti shamba wakidai juwa hospitalini nugonjwa huu hautibiwa, ila n Soma Zaidi...

kunauwezekano wa darri ya kchefuchefu ictokee kabsa kwa mjauzito
Kichefuchefu ni moja katika dalili za mimba za mapema, Lucinda je upo uwezekano kwa mwanamke kuwa na ujauzito bila hata ya kuwa na kichefuchefu? Soma Zaidi...

Nini husababisha maumivu ya uume
Kama uume wako unauma ama unahisi kuwa unaunguza ama kuchoma choma, post hii imekuandalia somo hili. Soma Zaidi...

Dalili za tezi dume.
Posti hii inahusu zaidi Dalili ambazo anaweza kuzipata mwenye Ugonjwa wa tezi dume, sio Dalili zote mtu anaweza kuzipata kwa sababu dalili kama hizi zinaweza kujitokeza hata kwa magonjwa mengine. Soma Zaidi...

Je, mwanamke anapataje Ugonjwa wa Maambukizi ya mfumo wa Uzazi PID?
Posti hii inaelezea namna mwanamke anavyoweza kupata Ugonjwa wa Maambukizi ya mfumo wa Uzazi. Soma Zaidi...

Endapo nina dalili za mimba na nikipima sina mimba, je, tatizo ni nini?
dalili za mimba zinaweza kuwa na mkanganyiko kwani zinafanana na shida nyingine za kiafya. Hali hii utaigunduwa endapo utakuwa na dalili za mimba lakini kila ukipima hakuna mimba. Soma Zaidi...

Njia za kupunguza tatizo la kutanuka kwa tezi dume.
Posti hii inahusu zaidi njia ambazo tunaweza kutumia ili kuweza kupunguza tatizo hili la kutanuka kwa tezi dume, kwa hiyo tunaweza kutumia njia zifuatazo ili kuweza kupunguza tatizo hili kwenye jamii kama ifuatavyo. Soma Zaidi...

Malezi ya mtoto mchanga na mama mjamzito
Post hii itakwenda kukuletea mambo kadhaa yanayohusiana na malezi bora ya mama mjamzito na mtoto mchanga Soma Zaidi...

Sababu za mwanamke kukosa hamu ya tendo la ndoa.
Posti hii inahusu zaidi sababu za mwanamke kukosa tendo la ndoa, ni sababu ambazo uwakuta wanawake wengi unakuta mama yuko kwenye ndoa ila hana hata hamu ya lile tendo la ndoa hali ambayo umfanya mwanamke kuona kitendo cha tendo la ndoa ni unyanyasaji au Soma Zaidi...

Mambo yanayosababisha nguvu za kiume kupungua
Posti hii inazungumzia kuhusiana na Dalili pamoja na mambo yanayosababisha nguvu za kiume kupungua kwa Wanaume Soma Zaidi...