DALILI ZA HIV ZA MWANZO NA DALILI ZA UKIMWI ZA MWANZO Kama ilivyo magonjwa mengi hupitia hatua kadha kadha na kuonyesha dalili kadha katika hatua hizo.
DALILI ZA HIV ZA MWANZO NA DALILI ZA UKIMWI ZA MWANZO
Kama ilivyo magonjwa mengi hupitia hatua kadha kadha na kuonyesha dalili kadha katika hatua hizo. Basi HIV nayo ina hatua zake mpaka kuwa UKIMWI.
DALILI ZA MWANZO ZA HIV AMA UKIMW
Dalili hizi huanza kuonekana kuanzia wiki mbili mpaka nne na wakati mwingine mpaka sita toka kuingia mwilini. Mara chache sana huweza kuonekana mwanzoni mwa wiki ya kwanza. Katika kipindi hiki mtu anaweza kuona dalili zifuatazo:
1.kufimba kwa tezi za kwenye makwapa, mapaja na shingo
2.Homa
3.Uchovu
4.Kuharisha
5.Kupungua uzito
6.Kikohozi
7.Pumzi kutoka kidogodogo
8.Mafua
Dalili hizi pia zinaweza kuhusiana na maradhi mengine, hivyo inaweza kuwa vigumu kujuwa nini chanzo zaidi. Wengi katika wanaopata HIV wametaja kuwa kuvimba kwa tezi ndio dalili pekee walioweza kuopata mwanzoni mwa kuathirika kwao. Wengine wanataja mafua kuwa ndio dalili yao ya kwanza.
Baada ya kipindi hiki kupita mgonjwa hatapata dalili yeyote ile. Hiki ni kipindi hatari sana kwani mtu hataweza kujijua kama ameathirika. Kipindi hiki kinaweza kudumi mpaka miaka 10. katika kipindi hiki virusi vinaendelea kuathiri seli za mwili. Baada ya mwili kuwa umeathirika sana na kudhoofu mtu ataanza kupata dalili za UKIMWI.
DALILI ZA UKIMWI
1.kutokwa na jasho jingi wakati wa usiku
2.Kupata homa za mara kwa mara na kuhisi baridi
3.Kikohozi
4.Kushinwa kupumua vyema
5.Madoa madoa kwenye ulimi na mdomoni
6.Maumivu ya kichwa
7.Uchovu usiokuwa na sababu na usioisha
8.Kutokuona vyema
9.Kupungua uzito
10.Mapele na ukurutu kwenye ngozi
Umeionaje Makala hii.. ?
Kubana kwa kifuwa ni katika hali ambazo si naweza kuhatarisha maisha. Huwenda kuwa ni miongoni mwa dalili za magonjwa mengi. Je unadhani na HIv na UKIMWI ni moja ya magonjwa hayo?
Soma Zaidi...Post hii inahusu zaidi dalili za maambukizi kwenye uume, ni dalili ambazo ujitokeza pale maambukizi yanapotokea kwenye uume.
Soma Zaidi...Pepopunda ni ugonjwa hatari wa kutishia maisha unaosababishwa na sumu inayojulikana Kama tetanospasmin inayotolewa kwenye majeraha yaliyoambukizwa. Bakteria ya pepopunda huingia kwenye mwili wa mtoto mchanga kupitia kisiki cha kitovu ambacho kimekatwa na
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi njia mbalimbali za matibabu ya ugonjwa wa saratani,ni ugonjwa ambao unaweza kupona ikiwa umegundulika mapema katika hatua za mwanzo na kama ugonjwa huu umefikia hatua za mwisho Tiba yake huwa ni kupunguza makali ya ugonjwa.
Soma Zaidi...Je unasumbuliwa na maumivuvya tumbo chini ya kitovu upande wa kushito. Post hii itakuletea sababu za maukivubhayo na nini ufanye.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi maumivu ya kiuno na dalili zake, ni maumivu ambayo utokea kwenye kiuno na kusababisha madhara mbalimbali katika mwili,
Soma Zaidi...Nini hasa kinatokea mpaka mtu anakuwa na pumu, ama anashambuliwa na pumu. Makala hii itakwenda kukufundisha jambo hili
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi mbinu mbalimbali ambazo zinaweza kutumika ili kuweza kupunguza kiwango cha kuwepo kwa magonjwa ya kuambukiza, kwa hiyo zifuatazo ni mbinu ambazo zinapaswa kutumika ili kupunguza kiwango cha magonjwa ya kuambukiza.
Soma Zaidi...Somo Hili linakwenda kukueleza kuhusu dalili za presha ya kushuka
Soma Zaidi...