Maradhi ya Ini na dalili zake, na vipi utajikinga nayo

MAGONJWA YA INI NA DALILIZAKE, NA KUKABILIANA NAYO Ini ni katika viungo vikuu katika mwili wa binadamu.

Maradhi ya Ini na dalili zake, na vipi utajikinga nayo

MAGONJWA YA INI NA DALILIZAKE, NA KUKABILIANA NAYO
Ini ni katika viungo vikuu katika mwili wa binadamu. Ni katika viungo vichache ambavyo vikikatwa vinaweza kujirudisha, yaani kukuwa. Ini ni katika viungo vinavyo shambuliwa na vimelea vya maradhi mbalimbali pamoja na sumu za vyakula. Ini mwilini husaidia katika mmengenyo wa chakula, na kuondoa sumu za vyakula mwilini. Endapo ini litadhurika kwa namna yeyote ile afya ya mtu katu haitakuwa salama, na athari zake endapo zitachelewa kupatiwa matibabu hupelekea kifo.

Katika makala hii tutakwenda kuyaona baadhi ya maradhi ya ini, dalili zake na njia za kukabiliana nayo. Kuwa nasi kwenye makala hii, na wasambazie wengine uwapendao, kulinda afya zao. Makala kama hizi na nyinginezo utazipata kwenye tovuti yetu www.bongoclass.com

Maradhi yanayoshambulia figo yapo mengi sana, na yapo ambayo hurithiwa na mengine hayarithiwi. Na yapo ambayo huambukizwa na mengine hayaambuizi. Ifuatayo ni orodha ya maradhi ya ini:-



SABABU ZA KUTOKEA KWA MARADHI YA INI:
Ili tuone sababu hizo kwanaz atuone aina za maradhi ya ini. Na himo kwenye aina hizo ndipo utakapojua ni sababu ipi imesababisha maradhi hayao:-

A. Maradhi ya ini yanayosababishwa na maambukizi
Maradhi ya ini yanayosababishwa na maambukizi yanajulikana kama homa ya heatitis. Homa hii husababishwa na virusi wanaotambulika kama hepatisis viruses. Miongoni mwa virusi hao ni:-
1.hepatitis A
2.Hepatitis B
3.Hepatitis C



B. Maradhi ya ini yanayosababishwa na mashambulizi ya mfumo wa kinga mwilini, kushambulia seli za ini. Kitaalamu hutambulika kama immune system Abnomality au Autoimune. Maradhi ya ini yanayosababishwa kwa njia hii ni:-
1.Autoimmune hepatitis
2.Primary biliary cirhosis
3.Primary sclerosing cholangitis




C. Maradhi ya ini yanayosababishwa kwa kurithi
Unaweza kurithi maradhi ya ini kutoka kwa wazazi wako ,ima mmoja wapo ama kwa wote. Maradhi ya ini yanayosababishwa na kurithi ni:-
1.Homochromatosis
2.Hyperoxaluria na oxalosis
3.Wilson's diseases



D. Maradhi ya ini yanayosababishwa na saratani (cancer)
1.saratani ya ini
2.Saratani ya nyongo
3.Kuvimba vya ini



DALILI ZA MARADHI YA INI
Katika maradhi yote tulioyataja hapo juu, ynashirikiana kwa pamoja katika dalili zifuatazo:
1.macho na ngozi kuwa na rangi ya njano.
2.Maumivu yasiyo ya kawaida yanayoendana na kuvimba mwili
3.Kuvumba kwenye miguu na vifundo vya miguu (ankles)
4.Kuuma kwa ngozi
5.Mkojo kuwa na rangi nyeusi ama giza
6.Kupata choo chenye rangi kupauka, ama kuwa na damu
7.Uchovu mkali sana na usio wa kawaida
8.Kichefuchefu na kutapika
9.Kukosa hamu ya kula
10.Ngozi kuchubuka kwa urahisi.



MAMBO YANAYOHATARISHA AFYA YA INI NA KULETA MARADHI YA INI
1.unywaji wa pombe kupitiliza
2.Kujidunga sindano kwa kushirikiana
3.Uwekaji wa tatuu
4.Kuongezewa damu
5.Muingiliano wa majimajin ya mwili na damu
6.Kupanya ngono zembe
7.Kisukari
8.Kuzidi kwa uzito



VIPI UTAWEZA KUZUIA MARADHI YA INI
1.Punguza unywaji wa pombe
2.Jiepushe na tabia hatarishi kama kujidunga masindano, kushirikiana vitu vya ncha kali, ngono zembe n.k
3.Pata chanjo ya baadhi ya maradhi ya ini kama hepatitis
4.Ilinde ngozi yako
5.Hakikisha huna uzito wa kuzidi
6.Fanya mazoezi
7.Unapopuliza dawa za wadudu vaa kitambaa puani (mask)



                   

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2018-08-01     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 202

Post zifazofanana:-

Darsa za Sira historia ya Mtume (s.a.w) Jaribio la 02
Soma Zaidi...

KIJUWE KISUKARI CHANZO CHAKE, DALILI ZAKE NA KUKABILIANA NACHO
Pata elimu juu ya afya hapa ukiwa na vitabu vyetu bila ya malipo yoyote Soma Zaidi...

Nini maana ya protini
Unaijuwa maana ya virutubisho vya protini, na kazi zake mwilini. Soma zaidi hapa Soma Zaidi...

Chemsha bongo namba 15
24. Soma Zaidi...

HISTORIA YA NABII ADAM
Soma Zaidi...

Muhtasari wa madili malezi ya jamii kama ilivyobainishwa katika Qur-an
(v)Kuwaombea dua wazazi. Soma Zaidi...

Chemsha bongo namba 03
Tatua mzozo wa NI NANI MUUAJI? Soma Zaidi...

tarekh11
KUKUTANA NA BAHIRA (MTAWA) WA KIYAHUDIMzee Abu talib alikuwa ni mfanya biashara, hivyoslikuwa akimchukuwa kijana wake kwenda kwenye biashara. Soma Zaidi...

malezi ya mtoto mchanga baada ya talaka
Soma Zaidi...

NAMNA YA KUSWALI: NIA YA SWWALA, NA KUPIGA TAKBIRA (yaani kusema Allah akbar)
Mtume (s. Soma Zaidi...

Historia ya Mwanadamu
Soma Zaidi...

Lengo la swala
Lengo la Kusimamisha SwalaBila shaka swala imepewa umuhimu mkubwa kiasi cha kufanywa nguzo kubwa ya Uislamu kutokana na lengo lake. Soma Zaidi...