picha

Homa ya manjano, dalili za homa ya manjano na namna ya kujikinga na homa ya manjano

HOMA YA MANJANO (yellow fever)Homa ya manjano ni maradhi yanayosababishwa na virusi na husambazwa na mbu.

Homa ya manjano, dalili za homa ya manjano na namna ya kujikinga na homa ya manjano

HOMA YA MANJANO (yellow fever)
Homa ya manjano ni maradhi yanayosababishwa na virusi na husambazwa na mbu. Homa hii ipo sana nchi za Afrika na Amerika ya Kusini. Kwa hali ya kawaida homa ya manjano huweza kusababisha homa, maumivu ya kichwa, kichefuchefu na kutapika. Pia homa ya manjano inaweza kuwa mbaya zaidi na kupelekea matatizo kwenye ini, figo na moyo pamoja na kutoka kwa damu yali inayotambulika kitaalamu kama hemorrhaging.



Inakadiriwa kuwa asilimia 50 ya wanaopata homa ya manjano wanafariki kwa maradhi maradhi haya. Tafiti zinaonyesha kuwa mpaka sasa hakuna tiba maalumu ya homa ya manjano, ila ipo chanjo kwa ajili ya kujikinga na virusi wanaosababisha homa hii.



Tafiti zinaonesha kuwa baada ya kungโ€™atwa na mbu na kukuachia virusi hawa wa haoma ya manjano, virusi hivi huchukuwa siku tatu mpaka sita kumomaa. Kipindi hiki kitaalamu hufahamika kama incubation period. Katika kipindi hiki katu hutohisi dalili yeyote. Kisha hatua inayofuatainatambulika kama accute phrase kisha hatua ya meisho ni toxic phrase.



DALILI ZA HOMA YA MANJANO
A.Dalili za homa nya manjano katika hatua ya pili (Acute phrase)
1.Homa
2.Maumivu ya kichwa
3.Maumivu ya misuli hasa ya kwenye mgongo na magoti
4.Kutokufurahia mwanga wa jua
5.Vichefuchefu na kutapika
6.Kukosa hamu ya kula
7.Kuhisi kizunguzungu
8.Macho kuwa mekundu, uso na ulimu pia kuwa na rangi nyekundu



B. Dalili za homa ya manjano katika hatua ya pili (toxic phrase)
1.Macho na ngozi kuwa na rangi ya njano
2.Maumivu yasiyo ya kawaida pamoja na kutapika damu
3.Kuongezeka kukojoakojoa
4.Kutoka na damu kwenye mdomo, pua na macho
5.Kupungua kwa mapigo ya moyo (bradycardia)
6.Ini na figo kushindwa kufanya kazi
7.Ubongo kushinwa kufanya kazi, vyema na kusababisha matatizo kama kifafa (seizure), kupoteza fahami (coma) pamoja na kuchanganyikiwa (delirium)



SABABU ZA HOMA NA MANJANO (YELLOW FEVER)
Kama tulivyokwisha kuona kuwa homa ya manjano husababishwa na virusi wanaoenezwa na mbua aina ya Aedes aegypti. Mbu hawa hukaa karibu na maeneo ambayo watu huwa wanaishi na huzaliana kwenye maji yaliyo safi. Virusi vya homa ya manjano vinaweza pia kuwaathiri manyani.



KUJIKINGA NA HOMA YA MANJANO
Ijapokuwa asilimia 20 mapa 50 ya wanaopata homa ya manjano hufariki, lakini itambulike kuwa mgonjwa anauwezo wa kupona kabisa endapo atawahi kupatiw matibabu. Zifuatazo ni baadhi ya njia tu za kujikinga na homa ya manjano



1.pata chanjo ya homa ya manjano
2.Jikinge na kungโ€™atwa na mbu kwa:
?Kulala kwenye chandarua kizima na chenye dawa
?Kupaka losheni ya kuzuia mbu
?Kuondoa majimaji yaliyotuwama na kukata nyasi







                   



Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

       
Author: Rajabu image Tarehe: 2024-05-10 14:53:23 Topic: magonjwa Main: Post File: Download PDF Views 4201

Share On:

Share follows: 0 | Unique share links followed: 0
Sponsored links
๐Ÿ‘‰1 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)     ๐Ÿ‘‰2 Tafasiri ya Riyadh Swalihina     ๐Ÿ‘‰3 Kitau cha Fiqh     ๐Ÿ‘‰4 Simulizi za Hadithi Audio     ๐Ÿ‘‰5 Bongolite - Game zone - Play free game     ๐Ÿ‘‰6 web hosting    

Post zinazofanana:

AINA ZA MINYOO: tapeworm, livefluke, roundworm, hookworm, flatworm

AINA ZA MINYOO Minyoo ambao wanaweza kuishi ndani ya mwili wa binadamu wapo aina nying, lakini hapa nitakueleza aina kuu tatu za minyoo hawa.

Soma Zaidi...
Dalili za Ugonjwa wa ini

Posti hii inahusu zaidi dalili za ugonjwa wa inni, hizi ni dalili ambazo ujitokeza kwa mtu Mwenye ugonjwa wa inni, Dalili zenyewe ni kama ifuatavyo.

Soma Zaidi...
โ€‹Kupima HIV Nyumbani

Posthii inatoa mwongozo kamili kuhusu upimaji wa HIV nyumbani. Tutachunguza umuhimu wake, jinsi ya kutumia vifaa hivyo, faida zake, na hatua za kuchukua baada ya kupata majibu, ili kukuwezesha kufanya maamuzi sahihi kuhusu afya yako kwa usiri na utulivu.

Soma Zaidi...
Figo ni nini, ni yapi maradhi yake na nitajiepusha vipi na maradhi ya figo

Makala hii itakwenda kukueleza ni nini hasa hizi figo, na ni yapi maradhi yake na ni kwa namna ggani utaweza kujilinda na maradhi ya figo.

Soma Zaidi...
Sababu za wanawake kuwa na maumivu kwenye kiuno

Posti hii inahusu zaidi sababu za wanawake kuwa na maumivu kwenye viungo, ni ugonjwa unaowapata na wanaume ila kwa wanaweza unaowapata sana ukilinganisha na wanaume.

Soma Zaidi...
Ugonjwa wa Uti wa Mgongo (Meningitis): Dalili za dharura.

Ugonjwa wa uti wa mgongo (meningitis) ni dharura ya kitabibu inayohitaji utambuzi na matibabu ya haraka. Makala haya yanachunguza kwa kina maana ya ugonjwa huu, visababishi vyake (bakteria, virusi, na fangasi), dalili hatarishi zinazohitaji huduma ya dharura, na njia za kujikinga. Lengo ni kutoa mwongozo wa kitaalamu kwa jamii ili kupunguza vifo na madhara ya kudumu yatokanayo na ugonjwa huu.

Soma Zaidi...