Matatozo katika choo kidogo, maradhi ya figo na dalili zake pia namna ya kujikinga na madhradhi ya figo
MATATIZO YA CHOO KIDOGO NA FIGOFigo ni kiungo muhimu sana katika uchujaji wa mkojo, na afya ya mfumo wa utoaji taka mwili.
MATATIZO YA CHOO KIDOGO NA FIGO
Figo ni kiungo muhimu sana katika uchujaji wa mkojo, na afya ya mfumo wa utoaji taka mwili. Figo inakazi ya kuchija damu na kuondoa uchafu usiohitajika. Uchafu hii hukusanyika na kutoka nje kwa kupitia moko. Ndani ya mkojo kumekusanyika uchafu wa kemikali, ikiwemo sumu za vyakula na makemikali mabaya kutoka mwilini.
Endapo mfumo huu wa mkojo ukitetereka unaweza kuaathiri afya ya mtu kwa ujumla. Miongoni mwa matatizo katika mfumo wa mkojo ni kuwepo kwa vijijiwe vidogo. Hivi vinaweza kusababisha maumivu makali na kukosa choo kidogo.
Makala hii inakwenda kukupa ufahamu juu ya tatizo la choo kidogo na kutokea kwa vijijiwe kwenye figo. Pia tutaona sababu za kutokea kwa tatizo hili na vipi tutaweza kujiepusha. Songa nayo makala hii ya afya kwa ni ni muhimu sana kufahamu afya yako na afya ya walio karibu nawe.
VIJIWE VYA KWENYE FIGO NI NINI?
Hivi ni vitu vidogo vigumu kama vijijiwe vilivyotengenezwa ka kemikali zinazopatikana kwenye mkojo kama aina za chumvi na tindikali zilizomo kwenye mkojo. Vijijiwe hivi vinaweza kutokea kwenye figo, kibovu ama mirija ya kusafirisha mkojo. Vijiwe hivi hutengenezwa pale mkojo unapojikusanya kwa muda mrefu hivyo hali hii hutoa nafasi kwa kemikali kujikusanya na kutengeneza vijiwe.
Vijiwe hivi huweza kutoka kwa kupitia njia ya mkojo, kwa maumivu makali sana. Pia endapo hali itakuwa ni mbaya zaidi mgonjwa atafanyiwa upasuaji ili kuweza kuondoa vijiwe hivi. Katika kipindi kama hichi mjonjwa anaweza kutumia dawa za kupunguza maumivu. Athari ya vijiwe hivi inaweza kupelekea maumivu wakati wa kukojoa.
DALILI ZAKE
Vijiwe hivi mwanzoni havina dalili yeyote lakini endapo vitakuwa vimeshajikusanya vinaweza kuonyesha dalili zifuatazo:-
1.maumivu wakati wa kukujoa
2.Maumivu upande mmoja, kwenye mgongo na chini ya mbavu
Kukojoa mkojo wa rangi ya pinki, nyekundu ama wenye harufu mbaya
3.Kukojoa mara kwa mara
4.Kupata mkojo kidogo unapokwenda kukojoa
5.Homa
6.Kupata kichefuchefu ama kutapika.
SABABU ZA TATIZO HILI NA CHOO KIDOGO NA FIGO
1.vyakula, ulaji wa baadhi ya vyakula kwa wingi unawza kuwa sababu ya kutengenezwa kwa majingira ya kufanyika kwa viji wa vyakula vyenye chumvi hasa calcium unaweza kusababisha vijiwe hivi. Ulaji wa vyakula vya protini kupitiliza pia unaweza kuleta athaji hasi hata kutokea vijiwe hivi.
2.Athari za mashambulizi ya bakteria katika mfumo wa mkojo; mashambulizi kama ya UTI (Urinary track Infection) yanaweza kusababisha vijijiwe hivi. Endapo ugonjwa wa UTI utakaa kwa muda mrefu bila ya kutibiwa na kupona unakuwa UTI sugu, hii inaweza ksababisha kutokea kwa vijiwe kwenye mfumo wa mkojo.
3.nmna ya mtu anavyoishi yaani staili za maisha (life style). mtindo ambao mtu anaishi unaweza kuwa ni hatari kwa afya yako. Kwa mfano kuwa na tabia ya kutokunywa maji mengi, wakati huo huo ukawa unafanya kazi ambazo zinapoteza maji mwilini kwa wingi, kwa mfano kazi ambazo zinaleta jasho sana kisha ukawa haunywi maji ya kutosha. Hii inaweza kusababisha vijijiwe hivi.
4.kurithi baadhi ya matatizo ya kiafya., unaweza kurithi hali ambazo zinaweza kusababisha kwa urahisi kutokea kwa vijiwe hivi. Unaweza kurithi matatizo flani ya kiafya ambayo husababisha figo kuchuja aina maalumu ya asidi za amino itambulikayo kama cystinuria.
MAMBO YAAYOWEZA KUSAIDIA KUTOKEA KWA MATATIZO KATIKA NJIA YA MKOJO NA KUTOKEA KWA VIJIWE VYA KWENYE FIGO
1.familia (kurithi)
2.Kupungua kwa maji mwilini
3.Vyakula
4.Kuzidi kwa uzito
5.Upasuaji
JE UTAZUIAJE MATATIZO KATIKA NJIA YA MKOJO NA VIJIWE VYA KWENYE FIGO?
Wataalamu wa afya wanatueleza baadhi ya njia za kuweza kukabiliana na kujikinga na matatizo ya haja ndogo yaani mkojo. Njia hizi ukizifuata zitakusaidia usiweze kupatwa na vijiwe katika figo:-
1.kunywa maji mengi ya kutosha
2.Punguza kula vyakula vya chumvi kupituliza
3.Punguza ulaji wa baadhi ya vyakula kwa wingi kupitiliza kama bamia, unywaji wa chai kupitiliza, spinachi, viazi vitamu, maharage ya soya, karanga, na chokoleti
JE MADHARA HAYA YA FIGO, NJIA YA MKOJO NA VIJIWE VYE KWENYE FIGO HUWEZA KUTIBIKA?
Ndio matatizo haya yanatibika bila ya tatizo lolote. Mgonjwa atapewa dawa kulingana nna tatizo lake. Kwa hakika atapona kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu.
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
👉1 Bongolite - Game zone - Play free game 👉2 ai web app 👉3 Kitabu cha Afya 👉4 Kitau cha Fiqh 👉5 web hosting 👉6 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)
Post zinazofanana:
Jinsi ya kujikinga na magonjwa ya zinaa (STIs).
Magonjwa ya zinaa, yanayojulikana pia kama STIs (Sexually Transmitted Infections), ni miongoni mwa changamoto kubwa za afya ya umma duniani. Kila mwaka, mamilioni ya watu hupata maambukizi mapya ya magonjwa haya, huku wengi wakikosa kutambua kuwa wameambukizwa kutokana na kutokuwa na dalili katika hatua za awali. Habari njema ni kwamba sehemu kubwa ya maambukizi ya magonjwa ya zinaa inaweza kuzuilika kwa kufuata mbinu sahihi za kinga na kufanya maamuzi salama kuhusu afya ya uzazi. Katika makala hii utajifunza maana ya magonjwa ya zinaa, namna yanavyoenea, sababu zinazoongeza hatari ya maambukizi, njia bora za kujikinga, umuhimu wa kupima afya mara kwa mara, pamoja na ukweli muhimu ambao kila mtu anapaswa kuufahamu kuhusu STIs.
Soma Zaidi...Maambukizi kwenye mfumo wa usagaji chakula unaotokea kwenye utumbo mkubwa (diverticulitis)
Posti hii inazungumzia kuhusiana na mifuko midogo midogo, iliyobubujika ambayo inaweza kuunda kwenye utando wa mfumo wako wa usagaji chakula. Wao hupatikana mara nyingi katika sehemu ya chini ya utumbo mkubwa (koloni). Hali hiyo inajulikana kama Divert
Soma Zaidi...Maumivu ya magoti.
Maumivu ya magoti ni malalamiko ya kawaida ambayo huathiri watu wa umri wote. Maumivu ya goti yanaweza kuwa matokeo ya jeraha, kama vile ligament iliyopasuka au cartilage iliyochanika.
Soma Zaidi...Dalili za kisukari aina ya type 2
Kisukari cha Aina ya 2, ambacho wakati mmoja kilijulikana kama Kisukari cha watu wazima au kisichotegemea insulini, ni ugonjwa sugu unaoathiri jinsi mwili wako unavyobadilisha sukari (glucose), chanzo muhimu cha nishati ya mwili wako.
Soma Zaidi...Dalili za maumivu yanayosababishwa na mtiririko mdogo wa Damu.
Posti hii inazungumzia kuhusiana na maumivu yanayosababishwa na mtiririko mdogo wa damu, kwa kawaida wakati wa mazoezi. Wakati mwingine huitwa upenyo wa vipindi, hali hii kwa ujumla huathiri mishipa ya damu kwenye miguu, lakini upenyo unaweza kuathiri mi
Soma Zaidi...