Presha ya kushuka (hypotension) dalili zake na njia ya kukabiliana nayo

Presha ya kushuka (hypotension) dalili zake na njia ya kukabiliana nayo

Presha ya kushuka ama kitaalamu huitwa hypotension, presha ya kushuka ni hatari kwa afya kama ilivyo presha ya kupanda, maana mwili unakosa nguvu kabisa.

Presha ya kushuka (hypotension) dalili zake na njia ya kukabiliana nayo

RPESHA YA KUSHUKA (HYPOTENION)


Presha ya kushuka ama kitaalamu huitwa hypotension, presha ya kushuka ni hatari kwa afya kama ilivyo presha ya kupanda, maana mwili unakosa nguvu kabisa. Kama ilivyo presha ya kushuka presha ya kupanda unaweza kuizuia ana kujilinda nayo kwa kula vyakula salama.



VYAKULA MUJARABU KWA MWENYE PRESHA YA KUSHUKA


1.Tumia chumvi zaidi; wataalamu wa afya wanahimiza sana kutumia chumvi zaidi kwani madini ya sodium yaliyomo kwenye chumvi husaidia katika kupandisha presha. Ila tambua kuwa kwa wazee kuzidi kula chumvu kunaweza kusababisha moyo kujashinwa kufanya kazi vyema.
2.Kunywa maji mengi ya kutosha: maji husaidia katika kuongeza hali ya umajimaji kwenye miili. Hii husaidia kukabilia na upungufu wa maji mwilini (dehydration) hali hizi ni muhimu kwa kukabiliana na presha ya kushuka.
3.Punguza ulaji wa vyakula vya wanga kwa zaidi. Kwa mfano viazi mbatata, mchele na mikate
4.Kunywa chai yenye caffein;



DALILI ZA PRESHA YA KUSHUKA


1.Kushundwa kuona vyema
2.Kuchanganyikiwa
3.Kizunguzungu
4.Kuzimia
5.Uchovu wa hali ya juu.
6.Kuhisi baridi
7.Kushindwa kufikiri kwa kina
8.Kichefuchefu
9.Kushindwa kuhema vyema
10.Kutokwa na jasho




NJIA ZA KUKABILIANA NA MRESHA YA KUSHUKA


1.Fanya mazoezi ya mwili na viungo walau kila siku kwa muda wa dakika 30 mpka 60
2.Kunywa maji mengi na ya kutosha
3.Unapokaa usikae mkao wa kukunja miguu
4.Punguza ulaji wa vyakula vya wanga kama viazi mbatata, mchele na mikate
5.Punguza ama wach kabisa uvutaji wa sigara
6.Punguza ama wacha kabisa unywaji wa pombe.




HUDUMA YA KWANZA KWA ALIYEPATWA NA PRESHA YA KUSHUKA


1.Lala chini kwenye kitu kilicho flati.
2.Kunywa maji mengi
3.Tumia chumvi, unaweza kuilamba unaweza pia kukoroga chumvi kwenye kikombe na kunywa.
4.Kama hali inaendelea kuwa mbaya zaidi ni vyema kuwasiliana na kituo cha afya kilicho karibu nawe.



                   

Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

       
Author: Rajabu Rajabu
Tarehe: 2024-05-10 14:53:23 Topic: magonjwa Main: Post File: Download PDF
Views: 13870

Share On:

Share follows: 0 | Unique share links followed: 0
Sponsored links
👉1 Madrasa kiganjani     👉2 web hosting     👉3 Simulizi za Hadithi Audio     👉4 Kitau cha Fiqh     👉5 Kitabu cha Afya     👉6 kitabu cha Simulizi    

Post zinazofanana:

Dalili za Uvimbe kwenye mfuko wa uzazi (uterine fibroid)

Uvimbe kwenye mfuko wa uzazi hukua kutoka kwenye tishu laini za misuli ya uterasi. Fibroids nyingi ambazo zimekuwepo wakati wa ujauzito hupungua au kutoweka baada ya ujauzito, kwani uterasi inarudi kwenye ukubwa wa kawaida.

Soma Zaidi...
Maumivu, kizunguzungu, kichefuchefu na kutoka na damu ni dalili zamimba?

Je unapata dalili zisizoeleweka ni ni za mimba ama laa. Hapa nitakujuza hali baadhi ya wanawake zinazowatokea.

Soma Zaidi...
Dalili za fangasi kwenye mapafu

Posti hii inaonyesha dalili za fangasi kwenye mapafu.

Soma Zaidi...
Jinsi ya Kujenga Mahusiano Imara

Mahusiano imara hayaji kwa bahati mbaya, bali hujengwa kwa juhudi, uelewano, na heshima. Post hii inachunguza nguzo muhimu za kujenga uhusiano wenye furaha na ustahimilivu, ikizingatia mawasiliano, uaminifu, na utatuzi wa migogoro.

Soma Zaidi...
Je mtu akapima ukimwi na kile kipimo kidogo .je kina usahihi au la ..na pia kama inaonyesha mistari miwili.

Hivi umeshawahi kuwazakuwa jekipimo cha HIV ni sahihi kwa kiasi gani. Unadhani huwa kinakoseaga kutoa majibu?

Soma Zaidi...
Matatizo ya mapigo ya moyo

posti hii inazungumzia kuhusiana na matatizo ya mapigo ya moyo.Mapigo ya moyo ni hisia za kuwa na moyo wa haraka, unaodunda. Mapigo ya moyo yanaweza kuchochewa na mafadhaiko, mazoezi, dawa au, mara chache, hali ya kiafya. Ingawa mapigo ya moyo yanaweza k

Soma Zaidi...