image

CHEMSHABONGO NA BONGOCLASS

CHEMSHABONGO NA BONGOCLASS

Chemshabongo na Bongoclass

CHEMSHABONGO NA BONGOCLASS

1.Mfungwa majaribuni
Mnamo mwaka 1978 Kitui alipewa majaribio pindi alipopatwa na hatia ya wizi. Baada ya kesi alipelekwa gerezani kifungo kisicho na mwisho. Ila alipewa siku tatu za kutoka gerezani. Hakupewa chakula wala maji. Kitu pekee alichopewa ni chepe tu. Kama unavyoona kwenye picha. Pia chumba cha gereza kilikuwa kidogo kikiwa na dirisha moja tu dogo lenye upenyo mdogo wa kupita na kwa nyuma limezungukwa na bahari.


Chumba kilikuwa ni kirefu hivyo asingeweza kupanda. Urefu wa ukuta mpaka kufikia nkadirisha ni mita 5. cha chini ukuta umekwenda umbali wa mita tano, hivyo asingeweza kutoroka kwa kupitia chini. Kitui alitakiwa atoroke ndani ya siku tatu si hivyo angepoteza maisha. Je! Ungelikuwa ni wewe ungefanya nini? Tumia maarifa uliyo nayo kuweza kutoroka gerezani


Jibu
Kwa kutumia chepe alilo nalo anaweza kuchimba udongo na kuukusanya. Udongo huo ukiwa mwingi ataweza kuuparamia na hatimaye kulipata dirisha kwa urahisi. Ukuta ni mrefu lakini kwa kuwa nje kuna bahari. Ataweza kuruka kupitia dirishani na kuingia baharini, kwa kuogelea ataweza kuokoka kwa urahisi bila ya kuumia.


2.Mauaji Mnamo mwaka 2006 Mwalimu wa Geography aliuliwa siku ta kufungua shule, majira ya jioni mwezi wa kwanza. Miongoni mwa watuhumiwa walokamatwa ni Mwalimu mkuu, Mwalimu wa zamu na mwalimu wa hisabati.


Askari walipowauliza vyema mwalimu mkuu akasema yeye alikuwa ofisinu muda wote. Mwalimu wa hisabati aliseme yeye alikuwa anasimamia mtihani wa robo muhula darasani. Mwalimu wa zamu alisema yeyea alikuwa akiandaa ripoti ya siku pamoja na kuandaa masomo ya kufundisha kesho.


Baada ya upelelezi kulingana na maelezo ya watuhumiwa hawa watatu. Hatimaye Mwalimu wa hisabati alitiwa mbazoni na hatia ya mauaji. Je unadhani ni kwa nini askari walimtia hatia mwalimu wa hisabati?


Jibu Kulingana na maelezo ya mwalimu wa Hisabati yanaonekana sio sahihi. Haiwezekani siku ya kufungua shule aweze kusimamia mtihani wa robo muhula ambao unatakiwa ufanyike mwezi wa tatu. Mwalimu wa hesabau amejichanganya maelezo. Huenda kuna jambo analificha hapa.


3.Nani muuaji
Sikumoja mwalimu aliingia darasani, aliwakuta watoto wanajisomea somo la kiswahili. Mwalimu akawauliza kitendawili. Wanafunzi watatu tu ndio walikipata. Kitendawili hiko ni:


“Nyumba yangu ni ya kijani. Ndani ya nyumba ya kijani kuna nyumba nyeupe. Ndani ya nyumba nyeupe kuna nyumba nyekundau. Ndani ya nyumba nyekundau kuna watoto weusi”Je! Hii ni nyumba gani?


Jibu
Nyumba hii ni tunda tikit lililowivai. Juu la kijani, mbaada ya kijani kuna nyama laini nyeupe, kisha nyama nyekundu kisha zinafata mbegu nyeusi.


4.Punda Mjinga
Ni kwa nini Punda alichelewa kufika?
Kijana mmoja kwa jina la malikutwa alikuwa na punda wake. Alikuwa akimmbebesha mizigo na alipendelea kumpitisha kwenye njia ambayo huwa anavuka kamto kama maji. Hakika punda huyu alifurahia sana njia hii. Alikuwa akimbebesha chumvi. Punda yule alikuwa akifika kwenye mto huwa anajitotesha maji ama huoga kisha khuendelea na safari.


Siku moja alimbebesha mzigo wa sufi ala baada ya kuvuka mto kwa mwendo kama wa dakika 10, Punda alikuwa ameshoka sana, na alikuwa akitembea kidogo kidogo. Kwa hakika siku ile walifika usiku.


Unadhani ni kwa nini punda alichoka sana. Unafikiri ni kwa nini punda alipenda kuoga akifika mtoni?


Jibu.
Punda aligundua kuwa anapojitotesha mzigo wa chumvi hutota hivyo chumvi humung’unyikia kwenye maji. Hatimaye mzigo hupungua. Ila hakujuwa kuwa sio kila mzigo humung’unyika kwenye maji. Leo amebeba sufi ambayo hunywa maji, hivyo huongeza uzito wa mzigo.


5.Mpira hudunda.
Mpira hudunda, na wakati mwinginge ukiupiga unaweza kudunda na kukujia mwenyewe. Lakini leo Mchezaji mmoja wa mpira alipiga mpira pila ya kidunda sehemu na mpira ule ukamrudia mwenyewe. Unadhani ni mwanini mpira ulimrudia bila ya kudunda mahali?


Jibu
Ni kwa sababu mpira aliupiga kuelekea juu.


6.Je! Bado unakumbuka hii?
Nina sungura, nyasi na mbwa nataka kuvuka nao mto. Nikiwaacha peke yao mbwa atamla sungura na sungura atakula nyasi. Nikianza kuvuka na mbwa sungura atakula nyasi. Nikianza kuvuka na nyasi, mbwa atamla sungura.


Na mtumbwi ninaovukia uinaruhusu niwe mimi pamoja na kimojawapo. Je! Nitafanyaje nivushe salama mizigo yangu?


Jibu.
Nitaanza kuvuka na sungura na kuziacha nyasi na mbwa, kwani mbwa hali nyasi. Kisha nitarudia kuvuka na nyasi. Nikifika nitarudi na sungura, wakati huo kule kutabakia nyasi tu. Safari hii nitamuacha sungura na kuvuka na mbwa, na kumuacha sungura peke yake. Nikifika nitarudi kumchukua sungura na hatimaye wote watakuwa wamevuka.



Download kitabu hiki hapa





           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 793


Sponsored links
👉1 kitabu cha Simulizi     👉2 Kitau cha Fiqh     👉3 Kitabu cha Afya     👉4 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)     👉5 Madrasa kiganjani    

Post zifazofanana:-

CHEMSHABONGO NA BONGOCLASS
Soma Zaidi...

Chemsha bongo namba 18
21. Soma Zaidi...

Chemsha bongo namba 21
15. Soma Zaidi...

Chemsha bongo namba 15
24. Soma Zaidi...

Chemsha bongo namba 22
4. Soma Zaidi...

Chemsha bongo namba 10
7. Soma Zaidi...

Chemsha bongo namba 11
10. Soma Zaidi...

Chemsha bongo namba 16
9. Soma Zaidi...

Chemsha bongo namba 19
Soma Zaidi...

Chemsha bongo namba 08
20. Soma Zaidi...

SIRI
Hapana mpaka sasa hautambui chochote kuhusu kilichotokea. Soma Zaidi...

Chemsha bongo namba 03
Tatua mzozo wa NI NANI MUUAJI? Soma Zaidi...