image

MAGONJWA 7 YALETWAYO NA MBU: MALARIA, DENGUE, HOMA YA ZIKA, HOMA YA MANJANO

MAGONJWA 7 YALETWAYO NA MBU: MALARIA, DENGUE, HOMA YA ZIKA, HOMA YA MANJANO

MAGONJWA 7 YA MBU

BY RAJABU ATHUMAN

MAGONJWA 7 YALETWAYO NA MBU








UTANGULIZI 3
MARADHI ZAIDI YANAYOSABABISHWA NA MBU 4
1. VIRUSI VYA ZIKA (ZIKV) 4
2. HOMA YA DENGUE 4
3. HOMA YA CHIKUNGUNYA (CHIKV) 5
4. MALARIA 5
5. HOMA YA BONDE LA UFA (RVFD) 6
Magonjwa mengine ni:- 6
KWA NINI MBU HAWEZI KUAMBUKIZA HIV (UKIMWI) 6
UGONJWA WA MALARIA NI NINI? 7
NINI CHANZO CHA MALARIA? 8
NAMNA AMBAVYO MALARIA HUTOKEA 8
DALILI ZA MALARIA 9
ATHARI ZA KIAFYA ZA KUTOKUTIBU MALARIA 10
WATU WALIO HATARINI NA MALARIA 11
KUJIKINGA NA MALARIA 11
MTAMBUE MDUDU MBU (MOSQUITO) 12











UTANGULIZI
Mbu ni katika wadudu ambao husababisja vifo vya maelfu kila mwaka, na mamilioni ya watu wanaathirika na maradhi yaletwayo na mbu. Mbu bu katika wadudu wadogo ambao wamechukuwa nafasi kubwa katika tafiti za sayansi. Maeneo mengi ya duniani yamekuwa yakisumbuliwa na maradhi haya.


Mbu hupatikana sana katika maeneo yenye joto. Katika makala hii tutakwenda kueleza maradhi ambayo huletwa na mbu na hususani tutakwenda kuona pia kwa ndani kuhusu ugonjwa wa malaria, na maradhi mengine kama vyanzo vyao, dalili zao na athari zao kiafya.


Makala hii ni katika makala zetu za kiafya ambazo zimeangalia katika yale ambayo yameenea kwenye jamii katika maradhi. Tunatarajia msomaji wetu ukimaliza makala hii utakuwa na ufahamu wa kutosheleza kuhusu mbu, na maradhi ambayo anaambukiza.


Ukiwa na maoni ama mawazo, hakikisha kuwasiliana nasi kwa haraka zaidi kupitia mawasiliano yatu hapo chini. Pia kama unahitaji kutia sauti makala zetu hizi wasiliana nasi:-


Mawasiliano:-
Mwandishi: Rajabu Athuman
Msambazaji: www.bongoclass.com
Phone: +255675255927
Email: admin@bongoclass.com












MARADHI ZAIDI YANAYOSABABISHWA NA MBU
Mbu ni mdudu anayeongoza kwa kusababisha vifo vya watu wengi duniani. zaidi ya watu miliono mia mbili wanaathiriwa na maradhi yaletwayo na mbu kila mwaka duniani. Katika makala hii nitakwenda kukuletea maradhi ambayo yanasambazwa na mbu:-


1. VIRUSI VYA ZIKA (ZIKV)
Mnamo mwaka 2016 World Health Organization (WHO) iliitisha kikao cha dharura mnamo mwezi tarehe 1 mwezi wa pili mpaka tarehe 13 mwezi wa nne. katika kikao hiki ilitangazwa kuwa virusi vya ZIKA husambazwa na mbu aina ya Aedes aegypti.


Virusi vya zika husababisha kuzaliwa kwa watoto wasio wa kawaida kama vile watoto kuwa na vichwa vidogo ni athari ya virusi hivi. kwa sasa virusi hivi vimesambaa zaidi ya nchi 40 duniani. mbu hawa si kama wa malaria ambao hung'ata wakati wa usiku, mbu wanaobeba virusi wa zika wanang'ata wakati wa mchana.


miongoni mwa dalili za uwepo wa virusi hivi mwilini hufanana sana na dalili za malaria ijapo kuna utofauti kiasi. Dalili za uwepo wa virusi hivi ni kama:-
1. homa
2. mapele
3. athari kwenye macho
4. maumivu ya kichwa
5. maumivu ya misuli na viungio


Dalili hizi hizi huanza kutokea baada ya siku 3 mpaka 12 baada ya kupata virusi hawa. Ila tafiti zinaonesha kuwa yapata asilimia 80% ya watu wenye virusi hivi hawaonyeshi dalili yeyote na hawajui kama wana virusi hivi. Tofauti na kuwa virusi hawa wanasambazwa na mbu lakini pia tafiti zinathibitisha kuwa ngono pia huweza kuambukiza virusi hivi.


2. HOMA YA DENGUE
Homa ya dengue hupatikana sana Afrika, Asia na baadhi ya maeneo ya Caribbean. pia inapatikana maeneo mengine kama marekani na maeneo yenye joto. Dengue ni katika homa ambazo ni hatari sana. kama ilivyo virusi vua Zika havina chanjo, pia hakuna chanjo ya dengue.


dengue husambazwa na aina ya mbu waitwao Aedes aegypti. Mbu hawa pia wanang'ata wakati wa mchana tofauti na mbu wa Malaria. Dalili za dengue huweza kutokea siku nne mpaka saba baada ya kung'atwa na mbu.


Dalili za dengue dengue ni:-homa, maumivu ya kichwa, macho, viungio pamoja na misuli au miguu. Ugonjwa wa dengue mara chache hupelekea kifo. Dalili hizi zinakuwa hatari pale mgonjwa anapopata homa ya hemorrhagige. Hii hupelekea mgonjwa kutoka damu, ambayo haikati. Na hali hii pia inaweza kupelekea presha yaani shinikizo la damu kushuka sana.


3. HOMA YA CHIKUNGUNYA (CHIKV)
Haya ni maradhi ambayo husambazwa kutoka kwa mtu kwenda kwa mtu kwa kupitia mbu. Mbu aina ya Aedes aegypti ndiye ambaye anatuhumiwa kwa kusambaza maradhi haya. Homa hii kwa mara ya kwanza iligundulika mwaka 1952 Tanzania.


Dalili za maradhi haya zinaweza kutokea siku 3 mpaka 7 baada ya kung'atwa na mbu huyu. Dalili za malaria ni sawa na zile za dengue ila utofauti ni kuwa homa hii haipelekei kutokwa na damu. Dalili hizo ni kama homa, maumivu ya viungio, baridi, kutapika na kichefuchefu, maumivu ya mgongo pamoja na miwasho.


Neno 'chikungunya' ni neno la kabila ya kimakonde, kabila linalopatikana kusini mwa Tanzania. Neno hili linamaana ya "kunyumbulisha viungo katika hali isiyo ya kawaida". Nenohili lilimaanisha maumivu ya viungo anayoyapata mgonjwa. bado homa hii pia haina dawa ila zipo dawa za kupunguza athari ya dalili za homa hii.


4. MALARIA
Malaria ni katika maradhi ambayo husambazwa na na mbu jike aina ya anopheles. Kutokana na shirika la umoja wa mataifa linaloshughulikia afya (WHO) limetoa takwimu kuwa karibia watu milioni 300 mpaka 500, huathirika na ugonjwa wa malaria kila mwaka duniani. Na baadhi ya tafiti zinaonyesha kuwa yapata watu 470,000 wanafariki kwa ugonjwa wa malaria kila mwaka.


Ugonjwa wa malaria ulishakuwepo duniani toka zamani sana. Tafiti zinathibitisha kuwa malaria ilishakuwepo yapata miaka 2700 K.K yaani miaka 2700 kabla ya kuzaliwa kwa yesu. Na ndio maana kuna dawa nyingi za kienyeji ambazo zinatibu malaria, kwani wazee walishaugua ugonjwa huu toka zamani sana.


Dalili za malaria ni kama homa, maumivu ya viungo, viungio na mvurugiko wa tumbo. maumivu ya kichwa, kutapika ama kichefuchefu. Kutokwa na jaho na kukosa hamu yakula. Kuhisi baridi kali sana na kutetemeka. Kama mgonjwa atachelewa kutibu dalili hizi anaweza kuchanganyikiwa, kushindwa kupumua na hatimaye kifo.


5. HOMA YA BONDE LA UFA (RVFD)
Homa hii inapatikana katika maeneo ya bonde la ufa barani Afrika na na Mashariki ya kati. Historia inaonyesha kuwa mnamo mwaka 1977 na 1978 mamilioni ya watu waliathirika na maradhi haya na maelfu ya watu walifariki kwa ugonjwa huu.


Homa ya bonde la ufa mwanzo kabisa ilifahamika kuwa inaathiri mifugo, ila kwa sasa tunatambua kuwa binadamu nae anaweza kuupata ugonjwa huu. msambazaji mkuu wa maradhi haya ni mbu aina ya Aedes, pindi anapomng'ata mtu huweza kubeba vimelea na kusambaza.


Dalili za homa hii pia hufanana na baadhi ya maradhi tulioyataja hapo juu. Dalili hizo ni:-homa, udahifu, maumivu ya mgongo, kuhisi kizunguzungu pamoja na kupungua uzito. Mara cache sana ugonjwa huu unaweza kupelekea hemorrhage hali inayopelekea kutokwa na damu aua meningoencephalitis hali inayopelekea kuvimba kwa ubongo.



Magonjwa mengine ni:-
6.homa ya manjano
7.Heartworm
8.Western Equine Encephalitis (WEEV)
9.St. Louis Encephalitis (SLEV)
10.La Crosse Encephalitis (LACV)
11.Japanese Encephalitis Virus (JEV)
12.Eastern Equine Encephalitis (EEEV)
13.Western Nile virus (WNV)
14.Matende
15.Ngiri maji


KWA NINI MBU HAWEZI KUAMBUKIZA HIV (UKIMWI)
Tumekusha kuona na kujua kuwa mbu anaweza kuambukiza maradhi mengi na ya virusi kama zika. Na mradhi mengine kama malaria na homa ya bonde la ufa. Lakini kuna jambo linaumiza sana fikra za wasomaji. “kama mbu wanaweza kuambukiza maradhi hayo ya virusi, sasa ni kwa nini mbu hawezi kuambukiza HIV?”


Kwa hakika swali hili linasumbua fikra za watu wengi sana. Tafiti nyingi za kisayansi zimefanywa ili kuthibitisha majibu sahihi na kuwaridhisha waulizaji. Ukweli ni kuwa mbu katu hawezi kueneza HIV. Na huu ni ukweli ambao haupingiki katu, lakini sasa ni kivipi?. katika makala hii nitakueleza jibu la swali hili katika namna tatu:-


1.Mdomo wa mbu una sehemu kuu 6, katika hizo 6 nne hutumika kutoboa ngozi ya mwili wa kiumbe anachotaka kunyonya damu. Na sehemu 2 zilizobakia ni kwa ajili ya kunyonya damu. Katika sehemu 2 hizo mojawapo ni kunyonya damu na nyingine ni kupeleka mate kutoka kwenye mwili wa mbu na kuelekea kwenye mwili wa kiumbe kinachonyonywa damu. Mate haya hutumika kwa kuifanya damu isigande.


Hivyo basi kitu ambacho kinatoka kwa mbu kwenda kwa kiumbe kinachonyonywa damu ni mate ya mbu tu, na si damu, kwani damu haiwezi kutoka kutoka kwa mbu kwenda kwa kiumbe kinachonyonywa. Tafiti zinaonesha kuwa mate kati hayawezi kuambukiza ukimwi, hata yawe ya mtu. Hivyo basi hata kama mate ya mbu yataingia kwa mbu kati hayawezi kuambukiza ukimwi kkama amebeba virusi.


2.Virusi vya HIV vikifika mwilini mwa mbu vinaliwa na kupotea kabisa. Virusi vya HIV ili viendelee kuzaliana vinahitaji kupata T seli (T cell), lakini mbu hana seli aina hii. Hivyo virusi vinapofika kwa mbu, vinaliwa pamoja na damu na kupotea kabisa. Kwa sababu hii hakuna uwezekano wa virusi vya HIV kuingia kwenye mate ya mbu ambayo ndio huenda kwa kiumbe kinachonyonywa damu. Hii inaonyesha kuwa katu HIV haiwezi kusambazwa kwa mbu.


3. hata kama virusi vya HIV vitaweza kuingia kutoka kwa mbu kwenda kwa kiume kinachonyonywa damu (japo jambo hili haliwezekani) hakua uwezekano wa kuambukiza HIV. Tafititi zinaonyesha kuwa ili damu ama mate ya mbu yasambaze HIV inahitajika ang’ate si chini ya mara milioni 10. Jambo hili kisayansi haliwezekani. Pia kummeza mbu aliyebeba HIV HAIWEZEKANI KUSAMBAZA HIV. Haka akipasukia kwenye jeraha la mtu katu damu yake haiwezi kuambukiza HIV.






UGONJWA WA MALARIA NI NINI?
Malaria ni katika maradhi yanayosumbua sana na kusababisha maradhi ya watu wengi sana duniani. Malaria ni katika maradhi yanayopatikana katika maeneo yenye joto, hususani maeneo yenye uoto wa kitropiki. Miongoni mwa maeneo ambayo yanasumbuliwa zaidi na malaria ni bara la Afrika.


Inakadiriwa kuwa mila mwaka watu milioni 210 (210,000,000 wanapata malaria kila mwaka na kati ya hao watu laki nne na elfu arobaini (440,000) wanakufa kwa ugonjwa huu kila mwaka na wengi wao ni watoto walio chini ya umri wa miaka mitano.


Mpaka sasa bado hakuna chanjo ya malaria ijapokuwa wataalamu wa afya wanajitahidi kuitafuta chanjo yake. Miili inaweza kutengeneza njianjo yao wenyewe japo ni ya muda na sio ya kuzuia malaria kabisa isipokuwa inaweza kupunguza athari za ugonjwa huu. Na hii ndio maana matu anaweza kuishi na malaria kwa muda mrefu bila ya kuumwa hasa.


NINI CHANZO CHA MALARIA?
Malaria husababishwa na vimelea (parasite) ambavyo husambazwa ama kubebwa na mbu aina ya anopheles. Kuna aina zaidi ya 2000 za mbu lakini katika aina hizi aina moja tu ndio inayoweza kubeba vimelea hivi vinavyoweza kusababisha malaria. Na pia yapo maradhi mengine ambayo husambazwa na aina nyingine za mbu. Maradhi hayo ni kama matende na ngiri maji.


Mbu aliyebeba vimelea vya malaria akimng’ata mtu anamuachia vimelea vile. Vimelea hivi vinapoingia ndani ya mwili viunakimbilia kwenye ini ambapo huko ndipo hukaa na kukuwa. Pindi vikikomaa vinatoka kwenye ini na kuelekea kwenye damu. Vinapofika kwenye damu vinakwenda kushambulia seli hai nyekundu za damu. Na hapo sasa mgonjwa ndipo ataanza kupata dalili za malaria..


Inachukuwa takribani wili ama na zaidi kwa vimelea hivi kuanza kuonesha dalili kwa mtu. Pia upo uwezekano vimelea hivi vikakaa hata mwaka ndipo vikaanza kuonyesha dalili. Na ndio maana ni vyema kupima afya mara kwa mara ili kuweza kuondoa vijidudu hivi kwenye miili yetu hata kabla ya kuanza kuonyesha dalili.


NAMNA AMBAVYO MALARIA HUTOKEA
Kama tulivyokwisha kuona kuwa malaria inaweza kuambukizwa kwa kung'atwa na mbu aina ya anophelesi. basi tambua kuwa ni mbu jike tu ndiye huweza kuambukiza malaria. basi hapa nitakueleza namna ambavyo malaria huweza kutokea.


kwanza kabisa lazima kuwepo kwa vimelea vya malaria aidha kwa mtu mwenye mwili wa mbu jike aina ya anophelesi. vimelea hivi vya malaria vinaanza kuzaliana kwenye mwili wa mbu jike. baada ya siku 10 mpaka 18 vimelea hivi vinakomaa na kuwa kimelea kipya kinachojulikana kama sporozoite. Kisha hivi vimelea vingi vinahamia kwenye tezi za mate za mbu na hatimaye kuingia kwenye mate ya mbu.


Mdomo wa mbu una mirija mikuu miwiliu. Mmoja ni wa kunyonyea damu na mwingine ni wa kutolea mate. Wakati anapong'ata mtu mate yake huingia kwenye mwili wa mtu. Mate haya yakiwa yana vimelea vya malaria (sporozoite) vijidudu hivi huingia kwenye mwili wa mtu. Na hapa hatua nyingine ya vimelea hivi inaanza.


Vimelea hivi (sporozoite) vinapoingia kwenye mwili wa mtu moja kwa moja vinaelekea kwenye ini. na huko huanza kukuwa na kuwa schizonts baadaye hupasuka na kutoa merozoites hivi ni vimelea vipya vilivyokomaa. vimelea hivi kama havitapatiwa dawa ya kuondolewa vitaendelea kwenye mfumo wa damu na kuanza kushambulia seli nyekundu za damu.


Baada ya merozoite kupatikana huelekea kwenye mfumo wa damu na kuanza kushambulia seli hai nyekundu za damu na kuanza kuzaliana humo kwa mara nyingine na kuleta vimelea vipya vitambulikavyo kama schizont na baadaye kupasuka na kutoa vimlea waitwao merozoites.


Na hapa sasa vimelea hawa wapya wanaanza kushambulia seli hai nyekundi na kuzaliana humo kisha seli hupasuka na kuleta vimelea wengi zaidi. Na kuanzia hapa ndipo mgonjwa sasa ataanza kuona dalili za malaria kama homa, maumivu ya kichwa, tumbo, misuli na viungo, kichefuchefu, kutapika na kuharisha.


Kama vimelea hivi havitatibiwa athari zaidi itatokea na kuanza kushambulia maeneo mengine ya mwili kama ini, figo, mapafu na moyo. hapa mgonjwa ataweza kuchanganyikiwa, matatizo ya ini na figo, kupumua kwa shida ama kuhohoa. Kama mgonjwa hatatibiwa athari zaidi inaweza kutokea kama kupoteza fahamu na hatimaye kifo.


DALILI ZA MALARIA
Dalili za malaria huenda pia zikafungamana na maradhi mengine, lakini endapo zikikusanyika pamoja kwa asilimia kubwa vitakuwa vinaonyesha uwepo wa malaria. Kumbuka hizi ni dalili tu, lakini ni vyema kupima ili kuwa na uhakika zaidi kabla ya kumeza dawwa.


1.Homa, homa ni kupanda kwa joto mwilini. Kikawaida homa ni dalili za maradhi mengi sanaila leo nitakueleza homa ya malaria ilivyo. Kikawaida hima ya malaria inaweza kuambatana na mambo kadhaa wa kadhaa. Mambo hayo ni kama


2.Kuhisi baridi, kutetemeka na kutaka kuotea jua ama moto. Haijalishi ni saa ngapi iwe mchana ama usiku lakini mgonjwa atahisi baridi kali sana. Na inaweza kumsababishia hali ya kutetemeka viungo ama taya za mdomo wake kugongana kwa baridi. Hivyo endapo homa itaungana na hali hii huenda ni malaria. Lakini haitishi, inaweza pia kuambatana na japo hili hap chini:-


3.Maumivu ya kichwa, uchovu na maumivu ya misuli pamoja na viungio. Endapo homa ya mgojwa itaambatana na baridi, kisha ikafuatiwa na maumivu ya kichwa, maumivu haya yanaambatana na misuli kuuma pamoja na viungio. Mgonjwa anahisi katikati ya akutano ya viungio kama kuna vuta. Halli hizi zikikusanyika kwa pamoja huashiria malaria.


4.Mvurugiko wa tumbo unaopelekea kichefuchefu, ama kuharisha, ama kutapika ama vyote kwa pamoja. Mgonjwa anaweza kupata hali moja kati ya hizi ama akawa nazo zote. Mgonjwa anaweza kutapika maji ama chakula alichokula ama anaweza kutapika ile tunayoita nyongo. Hali hizi zinaweza kumpelekea mgonjwa akachoka sana. Tofauti na kuchoka huku lakini hatakuwa na hamu ya kula, na hata ladha ya chakula inabadilika na kuwa kichungu.


5.Uchovu, kukosa hamu ya kula, maumivu ya viungo, kuchanganyikiwa, maumivu ya kichwa, kutapika ama kuharishah. Hizi ni katika dalili za malaria.


ATHARI ZA KIAFYA ZA KUTOKUTIBU MALARIA
Pindi malaria isipotibiwa inaweza kufanya dalili ziendelee na hatimaye kusababisha kifo. Lakini kabla ya kutokea kifo malaria huanza kwa kuathiri maeneo nyeti sana ya kiafya na hivyo hupelekea athari kubwa ambazo huleta kifo. Hebu tuone maeneo ambayo malaria hushambulia:-


1.Ubongo, vimjidudud vya malaria vinapoingia kwenye mfumo wa damu huanza kushambulia seli hai nyekundu za damu. Kupitia damu vijidudu hivi vinaweza kuingia kwenye ubongo na kusababisha kuziba kwa vimishipa vijidogo ndani ya upongo. Vimishipa hivi ndivyo hupeleka virutubisho na hewa kwenye ubongo. Hali hii inaweza kumfanya mgonjwa achanganyikie na kupoteza fahamu kabisa.


2.Ini na figo, vijidudu hivi vinaweza kusababisha ini na figo kushindwa kufanya kazi kwa ufanisi, ama tena kufa kabisa. Endapo hali hii ikitikea basi itakuwa ni athari kubwa sana katika afya ya mtu husika.


3.Mapafu, endapo malaria haitatibiwa na ikiendelea kuwepo mwilini inaweza kusababisha kujaa kwa majimaji kwenye mapafu. Hali hii inaweza kusbabisha mgonjwa kushindwa kupumua kwa ufanisi. Endapo hili litatokea itakuwa ni katika athari mbaya sana za malaria.


4.Damu, kwakuwa vijidudu hivi hushabulia seli hai nyekundu za damu, na seli hizi ndizo hubeba hewa ya oksijeni na kuisambaza mwilini. Hivyo malaria inaweza kusababisha upungufu wa hewa ya oksijeni mwlini na kusababisha ugonjwa unaotambulika kama anaemia.


5.Wakati mwingine malaria inaweza kuwa kali zaidi na kusababisha sukari kushuka, hali hii kitaalamu inajulukana kama hypoglycaemia. Na ni katika hali mbaya sana kwani mgonjwa anaweza kupoteza fahamu.


WATU WALIO HATARINI NA MALARIA
Malaria inaweza kumpata mtu yeyote bila ya kujali mri. Lakini kuna watu endapo wakipata malaria inakuwa ni mbaya zaidi kwa afya yao binafsi ama na kwa ya watu wengine. Watu hao ni:-


1.Wajawazito: wajawazito ni katika watu ambao ni hatari sana kwao wakipata malaria. kwani inaweza ikahatarisha pia afya ya mtoto aliye tumboni. wajawazito wanashauriwa kulala kwenye chandarua tena kilichokuwa na dawa. hii itasaidia kupunguza uwezekano wa kupata malaria.


2.Watoto wadogo chini ya miaka mitano, tafiti zinaonesha kuwa wanaofariki kwa ugonjwa wa malaria wengi wao ni watoto tena walio chini ya umri wa miaka 5. kundi hili la watu ndilo ambalo bado halijakuwa madhubuti kiafya kiasi cha kuweza kupambana na athari za malaria. hivyo ni vyema kuhakikisha kuwa watoto siku zote wanalala kwenye chandarua chenye dawa.


3.Wazee; kundi jingine linaloathiriwa na malaria ni hili kundi la wazee. afya za wazee hazipo imara sana ukilinganisha na afya za vijana. huenda ni kwa sababu miili yao haipo active muda wowote, huenda kwa sababu wazee wengi hawana kawaida ya kufanya mazoezi ya hapa na pale.


4.Watu wanaotoka ameneo yasiyo na malaria, kundi la mwisho linawahusu sana wageni ambao wametoka katika maeneo yasiyo na mbu ama yasiyo na ugonjwa huu. watu hawa miili yao haina mazoea na ugo njwa huu hivyo hakuna walinzi walio tayari kwa ajili ya kupunguza athari za malaria.


KUJIKINGA NA MALARIA
Kwa kuwa mbu wanaosambaza malaria wanang’ata usiku sana ama alfajiri, hivyo tunaweza kujikinga na malaria kwa :-
1.Kulala kwenye chandarua, ni vyema kikatiwa dawa. pia ni vyema ukahakikisha kuwa chandarua hakina matundu yaani kiwe kizima. ha hakikisha unawatoa mbu kwenye chandarua kama wapo kisha ndipo ujiandae kulala.


2.Kupaka losheni ya mbu; hiki ni losheni ambazo zina harufu mbaya ambayo inawakera mbu. harufu hiki huweza kutofautiana. kuna nyingine ni kali na nyengine ni kawaida. kuna nyingine utapenda harufu zao na nyingine hutapenda. watu wengine wakipaka losheni hizi huwashwa hususani wanapopaka usoni. hakikisha haupaki mdomoni kiasi kwamba unaweza kuila losheni kwa bahati mbaya.


3.Kuvaa nguo ndefu zinazoziba viungo; nguo hizi zisiwe ndefu tu bali ziwe nzito kiasi kwamba zinaweza kuzuia mbu kuifikia ngozi yako. ni vyea zikafunika mikono na miguu, na maeneo mengine ambayo yanashambuliwa na mbu kama shingo.


4.Kutumia dawa za mbu; dawa hizi zipo za kupulizia kama pafyumu na zipo za kuchoma. unaweza kutumia za kupulizia wakati hupo ndani kwa muda wa dakika kama 30. dawa za kuchoma nazo pia ni vyema ukachoma ukiwa umetoka kisha baada ya dakika 30 kisha ingia ndani.


5.Fyeka vichaka, punguza nyasi na fukia madimbwi yaliyo karibu na nyumba. hakikisha hakuna makopo, vifuu ama chochote kinachoweka maji. hii itasaidia kupambana na mazalia ya mbu.


MTAMBUE MDUDU MBU (MOSQUITO)
Mbu ni katika wadudu wanaopatikana maeneo yenye joto hususan maeneo ynye hali ya hewa ya kitropik. Mbu anafahamika kwa kuwa ndiye msambazaji mkubwa wa malaria pamoja na matende na ngiri maji. Chakula cha mbu ni maji, bakteria pamoja na damu. Mbu dume huweza kumjua mwanamke kwa kutumia sauti ya mbawa. Mbu ni katika wadudu wadogo lakini wana maajabu makubwa. Katika mkala hii tutaangalia kwa ufupi mambo matano kuhusu mbu.


Tofauti na kuwa mbu ni mdogo lakini anaweza kunyonya damu iliyokuwa nzito kuliko mwili wake. Yaani sawa na mtu mwenye uzito wa kilo 70 kula chakula chenye uzito wa kilo 100. mara mbu anaponyonya damu mwili wake huchukuwa mpaka siku tatu kuweza kuimeng’enya damu ile na kuimaliza. Baada ya hapo mbu atakwenda kunyonya damu tena. Itambulike kuwa chakula cha mbu ni bakteria, maji pamoja na damu. Mbu jike hula damu pindi anapotaka kutaga. Wataalamu wanaeleza kuwa kuna aina 2000 za mbu.


Kabla ya mbu kutaga mayai yake anaanza kupima ardhi kama ina majimaji pamoja na joto la kutosha kwa maisha ya mayai yake. Mbu hutaga mayai juu ya maji, ardhi, miti na nyasi pamoja na maeneo mengine yaliyo na majimaji. Pia mbu anaweza kutaga yai lake hata pakiwa na maji kiasi cha tone moja tu. Nayai ya mbu ni chakula kwa samaki pamoja na watutu wengine hivyo mbu huwa makini sana wakati wa kutaga mayai yake.


Tofauti na wadudu wengine na ndege mbu anaweza kulizuia yai lake tumboni kulitaga pindia anapohofia usalama wa yai lake. Kuku na ndege wengine yai linapofikia kutagwa hana namna lazima akalitage, lakini hii ni tofauti kwa mbu. Yai la mbu linaweza kukaa kwa muda wa miaka miwili bila ya kufa na ndo maana ni vigumu kutokomeza kabisa mbu.


Yai la mbu lina rangi ya njano, tangi hii ni rahisi kulifanya yai hili lionewe na maadui walao mayai ya mbu. Hivyo ifikapo usiku yai la mbu hubadilika rangi na kuwa jeusi. Hali hii husaidia kuliepusha yai la mbu kuliwa na maadua. Pia yai la mbu halizami ndani ya maji, na linaweza kuelea hewani, njia zote hizi husaidia ulinzi wa yai hili lisidhuriwe.


Ijapokuwa mbu anakula binadamu lakini na yeye ni chakula kwa viumbe vingine kama popo. Hivyo popo hutusaidia katika mapambano dhidi ya wadudu hawa hatari. mbu pia anaweza kujuwa wati mtu yupo kwa kutumia pumzi anayopumua mwanadamu.








ENDELEA NA DARASA HILI


Unaweza kuendelea na somo hili la AFYA NA MARADHI , mama na mwana. Kuendelea na darasa hili pata kitabu chetu kizima kwa bei poa tu. Wasiliana nasi kwa mawasiliano hapo chini.


Unaweza pia kupata mwendelezo wa darasa hili ukiwa kwenye tovuti yetu www.bongoclass.com. bongoclass imejipanga vyema kukupatia elimu bure.


Mawasiliano:
Phone: 0620555380
Email: admin@bongoclass.com
Tovuti: www.bongoclass.com



Download kitabu hiki hapa





           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 1440


Sponsored links
👉1 kitabu cha Simulizi     👉2 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)     👉3 Kitau cha Fiqh     👉4 Kitabu cha Afya     👉5 Madrasa kiganjani    

Post zifazofanana:-

Kwanini najihisi mchovu alafu tumboni kunavitu navihisi vinacheza sielewi
Habari yako Dokta. Soma Zaidi...

AFYA YA UZAZI NI NINI?, PIA UTAJIFUNZA MATATIZO YA HEDHI, KUTOKUPATA UJAUZITO, ULEZI WA MIMBA NA MTOTO, TEZI DUME NA NGIRI MAJI, NGUVU ZA KIUME
AFYA YA UZAZI Afya ya uzazi huweza kufungamana na mambo mengi sana. Soma Zaidi...

Umuhimu wa kupiga push up kiafya
Posti hii inahusu zaidi umuhimu wa kupiga push up kiafya, ni mambo au faida zipatikanazo ki afya kwa wapigaji wa push up kama ifuatavyo. Soma Zaidi...

TAHADHARI KWENYE VYAKULA
Pata elimu juu ya afya hapa ukiwa na vitabu vyetu bila ya malipo yoyote Soma Zaidi...

Kitabu Cha Afya
Soma Zaidi...

Sheria za kutunza usafi wakati wa upasuaji.
Posti hii inahusu zaidi sheria za kutunza usafi wakati wa upasuaji, iwapo sheria mojawapo ikienda kinyume ijulikane kuwa usafi haujaenda sawa na pengine kwa kitaalamu huitwa contamination. Soma Zaidi...

ITAMBUE SARATANI CHANZO CHAKE, DALILI NA KUKABILIANA NAYO
Pata elimu juu ya afya hapa ukiwa na vitabu vyetu bila ya malipo yoyote Soma Zaidi...

MAGONJWA NA AFYA
Soma Zaidi...

KAULI ZA WATU MASHUHURI KUHUSU AFYA
Soma Zaidi...

UPUNGUFU WA PROTINI NA FATI
Pata elimu juu ya afya hapa ukiwa na vitabu vyetu bila ya malipo yoyote Soma Zaidi...

AINA ZA VYAKULA
Pata elimu juu ya afya hapa ukiwa na vitabu vyetu bila ya malipo yoyote Soma Zaidi...

Dondoo 100 za Afya
Soma Zaidi...