Makubaliano ya Mkataba wa Al Fudhul
Sara na historia ya Mtume Muhammad s.a.w, sehemu ya 13. Hapa utajifunza historia ya Mkataba wa al fudhul na makubaliano yake.
MKATABA WA AL-FUDHUL
Baada ya vita hivi viongozi wa pande mbili hizi waliamuwa wakae chini na wakubaliane kuweka kanun i na utaratibu utakaozuia kutotokea uonevu kama huuu tena. Na hii ni kuwa maeneo mengi ya waarabu enzi hizo yalikuwa na utaratibu kama huu wa kuweza kusaidiana na kuzuia uonevu na unyanganyi wa haki. Makataba huu ulikuwa na lengo la kuwasaidia watu wanyonge ambao hawana urafiki na mahusiano na watu wenyenguvu, madaraka ama uwezo wa kipesa.
Hivyo lengo kuu la kiapo au mkataba huu ilikuwa kulinda haki za wanyonge, kuzuia dhulma na uonevu. Kuwapa haki watu wanaostahiki kupewa haki bila ya kujali wapi wametoka, ni nani ndugu zao au wanauwezo gani. Makataba huu ulifanyika kwenye nyumba ya mzee mwenye heshima,na mwenye umri aliyefahamika kwa jina la Abdallah bin Jad’an. Walohudhuria kwenye mkutano huu ni wawakilishi kutoka kabila la Banu hashim, Banu Al-Muttalib, Asad bin Abdul ‘Uzza, Zahran bin Kilab pamoja na Taim bin Murra.
Baada ya makubaliano yao ya kujenga amani kati yao wenyewe na wageni wao wanaokuja Makkah walikwenda kwenye Al-Ka’abah na kufanya kiapo. Kiapo chao ni kuyatekeleza walokubaliana kuwa watampa kila mtu haki yake na watapigana na yeyote ambaye atadhulumu na kumsaidia atakaye dhulumiwa. Watapigana na yeyote atakayevunja makubaliano haya mpaka haki ipatikane. Walifanya kiapo ndani ya al-ka’aba mbele ya kiwe jeusi.
Miongoni mwa walohudhuria mkutano huu kutoka upande wa maquraysh ni Mtume s.a.w. na baada ya kupewa utume Mtume (a.s.w) alisema: “nilishuhudia (mkutano, makubaliano mkataba) kwenye nyumba ya Abdallah bin Jad’an, mkutano ninaoupenda kuliko ngamia mwekundu, na lau ningeliitwa tena kwenye mkutano kama huu hakika ningehudhuri”. Maneno haya yanathibitisha kuwa mkutano huu uliridhiwa na Allah. Hizi pia zilikuwa ni katika vitangulizi vya kuja kwa mtume wa mwisho.
Na inasemekana kuwa chimbuko na wao kukutana ni kuwa alitokea mfanyabiashara mmoja kutoka katika kabila la Zubaid alikuja Makkah kufanya biashara. Hivyo akamuuzia Al-‘As bin Wa’il As-Sahmy baadhi ya bidhaa zake. Baadaye Al-As akakataa kumlipa mtu huyu. Hivyo mfanyabiashara akawa anaomba msaada kwa Maquraysh waweze kumsaidia ili apate haki yake, lakini hakuna ambaye alimjali.
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
π1 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w) π2 ai web app π3 Tafasiri ya Riyadh Swalihina π4 Dua za Mitume na Manabii π5 Simulizi za Hadithi Audio π6 kitabu cha Simulizi
Post zinazofanana:
Historia ya Watoto Wawili wa Nabii Adam
βNa wasomee khabari za watoto wawili wa Adam kwa kweli, walipotoa sadaka, ikakubaliwa ya mmoja wao na ya mwingine haikukubaliwa Akasema (yule asiyekubaliwa sadaka yake): βNitakuuaβ.
Soma Zaidi...Ni nani alikuwa sahaba wa mwisho kufariki
Katika somo hili utakwenda kujifunza kuhusu nani alikuwa wamwisho kufariki katika masahaba wa Mtume kwa mujibu wa historia
Soma Zaidi...Kwanini mwanadamu hawezi kuunda dini sahihi
Dini anayostahiki kufuata mwanadamu (EDK form 2 dhana ya elimu ya uislamu)
Soma Zaidi...Uchaguzi wa Omar (Umar) kuwa khalifa wa Pili baada ya Mtume
Uchaguzi wa βUmar bin Khattab kuwa Khalifa wa Pili.
Soma Zaidi...