ATHARI ZA KIAFYA ZA KUTOTIBU MALARIA AU KUCHELEWA KUTIBU MALARIA

Pindi malaria isipotibiwa inaweza kufanya dalili ziendelee na hatimaye kusababisha kifo.

ATHARI ZA KIAFYA ZA KUTOTIBU MALARIA AU KUCHELEWA KUTIBU MALARIA

ATHARI ZA KIAFYA ZA KUTOKUTIBU MALARIA

Pindi malaria isipotibiwa inaweza kufanya dalili ziendelee na hatimaye kusababisha kifo. Lakini kabla ya kutokea kifo malaria huanza kwa kuathiri maeneo nyeti sana ya kiafya na hivyo hupelekea athari kubwa ambazo huleta kifo. Hebu tuone maeneo ambayo malaria hushambulia:-

 

Ubongo, vimjidudud vya malaria vinapoingia kwenye mfumo wa damu huanza kushambulia seli hai nyekundu za damu. Kupitia damu vijidudu hivi vinaweza kuingia kwenye ubongo na kusababisha kuziba kwa vimishipa vijidogo ndani ya upongo. Vimishipa hivi ndivyo hupeleka virutubisho na hewa kwenye ubongo. Hali hii inaweza kumfanya mgonjwa achanganyikie na kupoteza fahamu kabisa.

 

Ini na figo, vijidudu hivi vinaweza kusababisha ini na figo kushindwa kufanya kazi kwa ufanisi, ama tena kufa kabisa. Endapo hali hii ikitikea basi itakuwa ni athari kubwa sana katika afya ya mtu husika.

 

Mapafu, endapo malaria haitatibiwa na ikiendelea kuwepo mwilini inaweza kusababisha kujaa kwa majimaji kwenye mapafu. Hali hii inaweza kusbabisha mgonjwa kushindwa kupumua kwa ufanisi. Endapo hili litatokea itakuwa ni katika athari mbaya sana za malaria.

 

Damu, kwakuwa vijidudu hivi hushabulia seli hai nyekundu za damu, na seli hizi ndizo hubeba hewa ya oksijeni na kuisambaza mwilini. Hivyo malaria inaweza kusababisha upungufu wa hewa ya oksijeni mwlini na kusababisha ugonjwa unaotambulika kama anaemia.

 

Wakati mwingine malaria inaweza kuwa kali zaidi na kusababisha sukari kushuka, hali hii kitaalamu inajulukana kama hypoglycaemia. Na ni katika hali mbaya sana kwani mgonjwa anaweza kupoteza fahamu.

 



                   

Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu

Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

Nzuri            Mbaya            Save
Author: Rajabu image Tarehe: 1970-01-01 03:33:44 Topic: magonjwa Main: Afya File: Download PDF Views 1758

Share On:

Facebook WhatsApp
Sponsored links
👉1 Tafasiri ya Riyadh Swalihina    👉2 kitabu cha Simulizi    👉3 web hosting    👉4 Dua za Mitume na Manabii    👉5 Madrasa kiganjani    👉6 Simulizi za Hadithi Audio   

Post zinazofanana:

Aina za ajali kwenye kifua,

Post hii inahusu Zaidi aina za ajali kwenye kifua,pamoja na kifua kuwa na sehemu mbalimbali na pia na ajali ambazo utokea Huwa za aina mbalimbali kama tutakavyoona.

Soma Zaidi...
Presha ya kushuka na matibabu yake

Somo Hili linakwenda kukueleza kuhusu presha ya kushuka na matibabu yake

Soma Zaidi...
Dalili za mtu aliyekula chakula chenye sumu

Post hii inahusu zaidi mtu aliyekula chakula chenye sumu, chakula chenye sumu ni chakula ambacho kikitumiwa na mtu yeyote kinaweza kuleta madhara kwenye mwili wa binadamu hata kifo.

Soma Zaidi...
Dalili za ugonjwa wa uvimbe na mashambulizi ya bacteria kwenye korodani

Posti hii inaonyesha dalili,Sababu,na namna ya kujikinga na ugonjwa wa uvimbe na mashambulizi ya bacteria kwenye korodani ambao kitaalamu hujulikana Kama orchitis.

Soma Zaidi...
Sababu za mkojo kushindwa kutoka kwenye kibofu.

Post hii inahusu zaidi mkojo kushindwa kutoka kwenye kibofu na kwa kitaalamu huitwa retention of urine.

Soma Zaidi...
Njia za maambukizi ya Homa ya inni

Posti hii inahusu zaidi njia za maambukizi ya Homa ya inni, Homa ya inni usababishwa na virusi viitwavyo Hepatitis B, huwapata watu wote hasa wale wenye umri chini ya miaka mitano.

Soma Zaidi...
Minyoo na athari zao kiafya

Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu minyoo na athari zao kiafya

Soma Zaidi...
YAMINYOO NA ATHARI ZAO KIAF

Kupata kitabu hiki download faili la PDF hapo chini na usome bila ya internet.

Soma Zaidi...
Dalili za awali za ugonjwa wa kizukari

ugonjwa wa kisukari ni moja katika magonjwa hatari sana, na mpaka sasa bado hauna matibabu ya kuponya moja kwa moja

Soma Zaidi...