picha

DALILI ZA UGONJWA WA MALARIA, (homa,uchovu, kutapika, kichefuchefu, maumivu ya kichwa n.k)

DALILI ZA UGONJWA WA MALARIA, (homa,uchovu, kutapika, kichefuchefu, maumivu ya kichwa n.k)

DALILI ZA MALARIA

 

Dalili za malaria huenda pia zikafungamana na maradhi mengine, lakini endapo zikikusanyika pamoja kwa asilimia kubwa vitakuwa vinaonyesha uwepo wa malaria. Kumbuka hizi ni dalili tu, lakini ni vyema kupima ili kuwa na uhakika zaidi kabla ya kumeza dawwa.

 

Homa, homa ni kupanda kwa joto mwilini. Kikawaida homa ni dalili za maradhi mengi sanaila leo nitakueleza homa ya malaria ilivyo. Kikawaida hima ya malaria inaweza kuambatana na mambo kadhaa wa kadhaa. Mambo hayo ni kama


Kuhisi baridi, kutetemeka na kutaka kuotea jua ama moto. Haijalishi ni saa ngapi iwe mchana ama usiku lakini mgonjwa atahisi baridi kali sana. Na inaweza kumsababishia hali ya kutetemeka viungo ama taya za mdomo wake kugongana kwa baridi. Hivyo endapo homa itaungana na hali hii huenda ni malaria. Lakini haitishi, inaweza pia kuambatana na japo hili hap chini:-

 

Maumivu ya kichwa, uchovu na maumivu ya misuli pamoja na viungio. Endapo homa ya mgojwa itaambatana na baridi, kisha ikafuatiwa na maumivu ya kichwa, maumivu haya yanaambatana na misuli kuuma pamoja na viungio. Mgonjwa anahisi katikati ya akutano ya viungio kama kuna vuta. Halli hizi zikikusanyika kwa pamoja huashiria malaria.

 

Mvurugiko wa tumbo unaopelekea kichefuchefu, ama kuharisha, ama kutapika ama vyote kwa pamoja. Mgonjwa anaweza kupata hali moja kati ya hizi ama akawa nazo zote. Mgonjwa anaweza kutapika maji ama chakula alichokula ama anaweza kutapika ile tunayoita nyongo. Hali hizi zinaweza kumpelekea mgonjwa akachoka sana. Tofauti na kuchoka huku lakini hatakuwa na hamu ya kula, na hata ladha ya chakula inabadilika na kuwa kichungu.

 

Uchovu, kukosa hamu ya kula, maumivu ya viungo, kuchanganyikiwa, maumivu ya kichwa, kutapika ama kuharishah. Hizi ni katika dalili za malaria.

 



                   

Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu

Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

Nzuri            Mbaya            Save
Author: Rajabu image Tarehe: 2018-08-01 Topic: magonjwa Main: Afya File: Download PDF Views 4309

Share On:

Facebook WhatsApp
Sponsored links
👉1 web hosting    👉2 Bongolite - Game zone - Play free game    👉3 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)    👉4 Dua za Mitume na Manabii    👉5 Kitabu cha Afya    👉6 kitabu cha Simulizi   

Post zinazofanana:

Dalili za kisukari aina ya type 2

Kisukari cha Aina ya 2, ambacho wakati mmoja kilijulikana kama Kisukari cha watu wazima au kisichotegemea insulini, ni ugonjwa sugu unaoathiri jinsi mwili wako unavyobadilisha sukari (glucose), chanzo muhimu cha nishati ya mwili wako.

Soma Zaidi...
Sababu za vidonda kwenye uume

Vidonda kwenye uume vinaweza kusababishwa na maambukizi ya magonjwa ya zinaa (STIs) kama kaswende na herpes, maambukizi ya fangasi au bakteria, majeraha madogo, mzio (allergy), au usafi duni. Uchunguzi wa kitabibu ni muhimu ili kutambua chanzo na kupata tiba sahihi.

Soma Zaidi...
Madhara ya ugonjwa wa ukimwi kwenye jamii.

Posti hii inahusu zaidi madhara ambayo yanaweza kutokea ikiwa Ugonjwa huu wa ukimwi ukishasmbaa kutoka sehemu moja kwenda nyingine na kuleta madhara makubwa kama ifuatavyo.

Soma Zaidi...
Sababu za kutokea kwa maumivu ya jino

Somo Hili linakwenda kukueleza kuhusu sababu za kutokea kwa maumivu ya jino

Soma Zaidi...
MJUE MBU, NA YAJUWE MARADHI MAKUU MATANO (5) HATARI YANAYOAMBUKIZWA NA MBU, malaria kukamata namba moja kwenye maradhi hayo)

Mbu ni katika wadudu ambao husababisja vifo vya maelfu kila mwaka, na mamilioni ya watu wanaathirika na maradhi yaletwayo na mbu.

Soma Zaidi...
Dalili na ishara za Ugonjwa wa kuambukiza.

Magonjwa ya kuambukiza ni maradhi yanayosababishwa na vijidudu kama vile bakteria, virusi, fangasi au vimelea. Viumbe vingi vinaishi ndani na kwenye miili yetu. Kwa kawaida hazina madhara au hata kusaidia, lakini chini ya hali fulani, baadhi ya viumbe

Soma Zaidi...
Ni nini husababisha mate kujaa mdomoni, na ni yapi matibabu yake

Hapa tutaangalia baadhi ya sababu zinazopelekea mdomo kujaa mate na namna ya kutibu tatizo la kujaa kwa mate mdomoni

Soma Zaidi...
Fahamu Ugonjwa wa kifua kikuu kwa watoto chini ya miaka mitano

Posti hii inaonyesha mambo mbalimbali yanayoweza kusababisha Ugonjwa wa kifua kikuu kwa watoto chini ya miaka mitano.

Soma Zaidi...
Tatizo la fizi kuachana.

Posti hii inahusu zaidi tatizo la fizi kuachana, ni tatizo ambalo uwakumba watu wengi kwa wakati mwingine unakuta fizi zimeachana kutoka sehemu moja kwa nyingine kwa hiyo tunaweza kuona sababu kama ifuatavyo.

Soma Zaidi...
Ugonjwa wa degedege na dalili zake

Ugonjwa wa degedege ni ugonjwa unaowapata sana watoto chini ya miaka mitano ingawa na watu wazima wanapatwa na ugonjwa huo

Soma Zaidi...