NINI CHANZO CHA UGONJWA WA MALARIA? NI YUPI MBU ANAYESAMBAZA MALARIA
Malaria husababishwa na vimelea (parasite) ambavyo husambazwa ama kubebwa na mbu aina ya anopheles.
NINI CHANZO CHA MALARIA?
Malaria husababishwa na vimelea (parasite) ambavyo husambazwa ama kubebwa na mbu aina ya anopheles. Kuna aina zaidi ya 2000 za mbu lakini katika aina hizi aina moja tu ndio inayoweza kubeba vimelea hivi vinavyoweza kusababisha malaria. Na pia yapo maradhi mengine ambayo husambazwa na aina nyingine za mbu. Maradhi hayo ni kama matende na ngiri maji.
Mbu aliyebeba vimelea vya malaria akimng’ata mtu anamuachia vimelea vile. Vimelea hivi vinapoingia ndani ya mwili viunakimbilia kwenye ini ambapo huko ndipo hukaa na kukuwa. Pindi vikikomaa vinatoka kwenye ini na kuelekea kwenye damu. Vinapofika kwenye damu vinakwenda kushambulia seli hai nyekundu za damu. Na hapo sasa mgonjwa ndipo ataanza kupata dalili za malaria..
Inachukuwa takribani wili ama na zaidi kwa vimelea hivi kuanza kuonesha dalili kwa mtu. Pia upo uwezekano vimelea hivi vikakaa hata mwaka ndipo vikaanza kuonyesha dalili. Na ndio maana ni vyema kupima afya mara kwa mara ili kuweza kuondoa vijidudu hivi kwenye miili yetu hata kabla ya kuanza kuonyesha dalili.
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
๐1 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w) ๐2 kitabu cha Simulizi ๐3 Bongolite - Game zone - Play free game ๐4 Simulizi za Hadithi Audio ๐5 web hosting ๐6 Tafasiri ya Riyadh Swalihina
Post zinazofanana:
Vyakula Muhimu kwa Mama Mjamzito
Ujauzito ni kipindi cha kipekee kinachohitaji uangalizi maalum wa lishe. Makala hii inaangazia vyakula muhimu ambavyo kila mama mjamzito anapaswa kuzingatia ili kuhakikisha afya yake na ukuaji bora wa mtoto aliyepo tumboni.
Soma Zaidi...Dalili za ugonjwa wa ngiri
Posti hii inahusu zaidi Dalili ambazo mgonjwa wa ngiri anaweza kuzipata, kwa hiyo baada ya kusoma na kuelewa dalili hizi mgonjwa anapaswa kuwahi hospitali mapema kwa ajili ya kupata matibabu.
Soma Zaidi...Sababu za Kichefuchefu Katika Mimba
โKichefuchefu na kutapika ni hali ya kawaida inayowapata wanawake wengi wajawazito, maarufu kama "asubuhi yenye kichefuchefu" (morning sickness). Posti hii inaelezea kwa nini hali hii hutokea, mambo yanayoichochea, na jinsi unavyoweza kuikabili ili kupata unafuu.
Soma Zaidi...Dalili za Maambukizi kwenye mifupa
Posti hii inahusu zaidi dalili za Maambukizi kwenye mifupa, ni dalili ambazo ukionyesha kwa mtu mwenye Maambukizi kwenye mifupa.
Soma Zaidi...Dawa za kutibu fangasi sugu za ukeni (Vaginal Candidiasis).
Fangasi wa ukeni (Vaginal Candidiasis) husababishwa na kuzaliana kupita kiasi kwa fangasi aina ya Candida. Ingawa mara nyingi hutibika kwa dozi moja, baadhi ya wanawake hukumbwa na fangasi sugu (recurrent candidiasis)โhali inayojitokeza mara nne au zaidi kwa mwaka. Hii si hali ya kawaida na inahitaji mbinu madhubuti za kitabibu badala ya kutegemea dawa za dukani pekee. Makala haya yanakupa mwongozo wa tiba na hatua za kudumu za kuondoa kero hii.
Soma Zaidi...Dalili zinazoonyesha joto la kupungua mwilini (hypothermia)
joto la mwili wako linapungua, moyo wako, mfumo wa neva na viungo vingine haviwezi kufanya kazi kwa kawaida. Isipopotibiwa, Hypothermia hatimaye inaweza kusababisha moyo wako na mfumo wa upumuaji kushindwa kabisa na hata kifo.
Soma Zaidi...