MALENGO KWA AKINA MAMA NA WACHUMBA KABLA YA KUBEBA MIMBA.


image


Posti hii inahusu zaidi malengo kwa akina Mama na wachumba kabla ya kubeba mimba, ni malengo ambayo yametolewa ili kuweza kusaidia mtoto azaliwe vizuri na mambo mengine kama tutakavyoona.


Malengo kwa akina Mama na wachumba kabla ya kubeba mimba.

1.Lengo la kwanza kabisa ni kuhakikisha kuwa Magonjwa hatarishi kwa Mtoto na Mama yanajulikana mapema na yanadhibitiwa mapema, kwa mfano Magonjwa kama vile Magonjwa ya zinaa na Maambukizi ya virus vya ukimwi, Magonjwa kama yanatibika watayatibu kama hayatibiki dawa maalum zitatolewa ili kumkinga Mama na mtoto.

 

2.Kuhakikisha kwamba Mama anakuwa na vitu vyote muhimu ki afya kwa ajili ya yeye na mtoto kwa mfano kuwa na damu ya kutosha, vitamini za kutosha,kubwa na madini ya kutosha, mwili kuwa na kinga ya kutosha na kutokuwepo kwa magonjwa hatarishi ya kutoka kwa Mama kwenda kwa mtoto.

 

3.Tunafanya hivyo ili kumpa Mama elimu kama vile kuepuka mambo hatarishi kabla ya kubeba mimba kama vile matumizi ya madawa ya kulevya, matumizi ya vileo vikali, matumizi ya madawa ya kienyeji, kuishi kwenye sehemu za viwanda vyenye kemikali kali, kutumia vitu vyote vyenye mionzi, kuwa na mazoezi yanayozidi mipaka kwa kufanya hivyo tutamwandaa mama ili aweze kupata mtoto asiye na Magonjwa.

 

4.Kwa hiyo basi tunapaswa kuwaelimisha wachumba wote na akina Mama wanaoendelea kuzaa wajiandae mapema ili kuweza kuepuka matatizo ya kupata watoto wenye ulemavu na Magonjwa ambayo yatawatesa katika maisha pale wazazi wanapoangaika ili kumtibisha mtoto na hatimaye kusababisha uchumi wa familia kushuka kwa hiyo tuendelee kutafakari msemo huu ambao unasema usipoziba ufa utajenga ukuta kwa hiyo wapendwa maandalizi ni ya muhimu sana na tunaokoa mambo mengi sana.



Sponsored Posts


  ðŸ‘‰    1 Mafunzo ya php       ðŸ‘‰    2 Madrasa kiganjani       ðŸ‘‰    3 Hadiythi za alif lela u lela       ðŸ‘‰    4 Magonjwa na afya       ðŸ‘‰    5 Mafunzo ya html kwa kiswahili       ðŸ‘‰    6 Maktaba ya vitabu    


Je! una maswali, mapendekezo ama maoni? tuma ujumbe wa meseji SMS hapo chini ili kuunganishwa na muhusika au bofya hapa

SMS SMS



Post Nyingine


image Mambo muhimu ambayo mama mjamzito anatakiwa kuzingatia.
Posti hii inazungumzia kuhusiana na Mambo ambayo mama mjamzito anatakiwa kuzingatia katika kipindi Cha ujauzito au mimba Soma Zaidi...

image Fahamu Ugonjwa wa Brucellosis
Posti hii inazungumzia kuhusiana na Ugonjwa wa Brucellosis ni maambukizi ya bakteria ambayo huenea kutoka kwa wanyama hadi kwa watu mara nyingi kupitia maziwa ambayo hayajasafishwa au kuchemshwa vizuri na bidhaa zingine za maziwa. Mara chache zaidi, bakteria zinazosababisha Brucellosis zinaweza kuenea kwa njia ya hewa au kwa kuwasiliana moja kwa moja na wanyama walioambukizwa. Soma Zaidi...

image Madhara ya minyoo
Somo hili linakwenda kukuletea madhara ya minyoo Soma Zaidi...

image Maambukizi ya tezi za mate
Psti hii inazungumzia kuhusiana na Ugonjwa wa Maambukizi ya tezi za mate ambao hujulikana Kama MABUSHA (mumps) ni maambukizi ya virusi ambayo kimsingi huathiri tezi mojawapo ya jozi tatu za tezi za mate zinazotoa mate, zilizo chini na mbele ya masikio yako. Ikiwa wewe au mtoto wako atapatwa na mabusha, inaweza kusababisha uvimbe katika tezi moja au zote mbili. Soma Zaidi...

image Sababu za kutokea kwa maumivu ya jino
Somo Hili linakwenda kukueleza kuhusu sababu za kutokea kwa maumivu ya jino Soma Zaidi...

image Yajue mashambulizi ya bacteria kwenye Ngozi (cellulitis)
Mashambulizi ya bacteria kwenye Ngozi hujitokeza sehemu yenye jeraha pia huonyesha wekundu wenye upele,Uvimbe na malengelenge. Soma Zaidi...

image Huduma ya Kwanza kwa mtu aliyekunywa sumu
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu huduma ya Kwanza kwa mtu aliyekunywa sumu Soma Zaidi...

image Sababu za ugonjwa wa pumu, dalili zake na jinsi ya kujilinda na pumu.
Ugonjwa wa pumu ni ugonjwa unaoshambulia mfumo wa hewa ambapo mgonjwa hushindwa kupumua vizuri na hupelekea matatizo ya kudumu kama haujatibiwa mapema. Soma Zaidi...

image Faida za kiafya za kula karanga
Somo hili linakwenda kukuletea faida za kiafya za kula karanga Soma Zaidi...

image Nini kinasababisha uume kutoa maji meupe bila muwasho,na tiba yake ni ipi
Je unasumbuliwa na Majimaji kwenye uume. Je unapata miwasho, ama maumivu wakati wakukojoa. Soma Zaidi...