Malengo ya huduma za uzazi kwa akina Mama.
Posti huu inahusu zaidi malengo ya huduma za uzazi kwa akina Mama, ni huduma muhimu ambazo zimetolewa kwa akina Mama ili kuweza kuepuka hatari mbalimbali zinazowakumba akina Mama wakati wa ujauzito, kujifu na malezi ya watoto chini ya miaka mitano.
Malengo ya huduma za uzazi kwa akina Mama.
1.Kuangali Magonjwa yanayoweza kutokea kwa wajawazito na kuwapatia dawa mapema ili wasiweze kuwaambukiza watoto.hili ni lengo mojawapo kuhakikisha kubwa kama kuna dalili yoyote ya ugonjwa ambao unaweza kujitokeza na kuwa tayari kuwapatia dawa ili kutibu na kuepuka kuwaambukiza watoto wakati wa ujauzito, mfano wa magonjwa ni kaswende na HIV kutoka kwa Mama kwenda kwa mtoto na kwa asilimia tisini hili limeweza kufanikiwa katika jamii zilizo nyingi.
2.Kuhakikisha kwamba maendeleo ya mtoto na Mama yako vizuri. Kwa kuhakikisha kuwa Mama anakuwa na damu ya kutosha mwilini kwa kupima wingi wa damu, kumpatia Mama dawa za minyoo na kupima kama kuna Malaria na kumpatia Mama vidonge vya sp kwa kila udhulio na kumpatia Mama neti mara tu anapoanza kliniki kwa kufanya hivyo Mama anaweza kuwa na afya nzuri pamoja na mtoto wake.
3. Kuhakikisha kuwa Mama anajua Maana ya uzazi wa mpango ili aweze kupata watoto anaowahitaji na kuwa na distansi fulani kama ni kuzidiana miaka minne au mitano kuu kadri ya maamuzi ya wazazi wenyewe kwa kufanya hivyo watoto wanaozaliwa wanapata upendo kutoka kwa wazazi wao na pia Mama anapata nafasi ya kushiriki kwenye shughuli za kiuchumi kwa kupata mda wa kutosha badala ya kubaki katika kulea watoto wanaofuatana bila mpangilio.
4.Lengo lingine ni kuhakikisha kuwa Dalili za hatari wakati wa ujauzito zinapungua kwa kuwapatia akina mama elimu kabla ya kuanza mahudhurio ili mama akiona dalili mojawapo ambayo ni ya hatari aweze kuja hospitali mara moja ili kuepuka madhara kwa mtoto, Dalili hizo ni pamoja na mtoto kushindwa kucheza, kugongwa na kichwa, kizungu Zungu, kutoka damu ukeni, kuhisi maumivu makali ya tumbo, homa kali na mabadiliko mengine ambayo siyo ya kawaida kwa Mwanamke mjamzito.
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
👉1 Simulizi za Hadithi Audio 👉2 Tafasiri ya Riyadh Swalihina 👉3 Kitau cha Fiqh 👉4 Dua za Mitume na Manabii 👉5 Bongolite - Game zone - Play free game 👉6 Kitabu cha Afya
Post zinazofanana:
Huduma kwa mama mwenye mimba Inayotishia kutoka.
Post hii inahusu zaidi huduma ambayo Mama anapaswa kutolewa pindi mimba inapotishia kutoka huduma hii utolewa kulingana na Dalili tulizoziona zinazohusiana na mimba kutishia kutoka.
Soma Zaidi...Mwezi juzi niliingia tarhe 21 ila mwez uloisha nmeingia tarh 25 maana mzunguko wangu umekuwa mrefu nikahs naujauzito kumbe mzunguko umebadilika hapo tatz n nn
Posti hii utakwenda kutoa sababu kuu za kuvurugika kwa mzunguko wa hedhi. Kama na wewe numiongini mwaka endelea kusoma
Soma Zaidi...Mimba changa: Dalili za hatari unazotakiwa kuzijua.
Miezi mitatu ya kwanza ya ujauzito (trimester ya kwanza) ni kipindi nyeti sana kwa ukuaji wa mtoto na mabadiliko ya mwili wa mama. Ingawa ni kawaida kuhisi uchovu au kichefuchefu kidogo, kuna baadhi ya dalili ambazo si za kawaida na zinaashiria dharura ya kitabibu. Makala hii inaangazia ishara za hatari unazopaswa kuzitilia maanani ili kulinda afya yako na ya kiumbe ulichobeba.
Soma Zaidi...Jinsi ya kuacha kupiga punyeto.
Post hii inakwenda kukupa njia za kukusaidia kuacha punyeto.
Soma Zaidi...Uzazi wa mpango
Uzazi wa Mpango hutoa chaguo kwa familia kuwa na idadi ya watoto wanaotaka katika muda maalum, wanahisi na mbinu iliyoamuliwa. Uzazi wa mpango una faida kadhaa kwa mama wa mtoto, wanandoa na jamii Ujuzi wa mzunguko wa hedhi humwezesha mtoa huduma kumshaur
Soma Zaidi...Njia za kuondoa fangasi sehemu za siri
Makala hii itakujuza baadhi ya njia utakaoweza kuzifuata ili kukabiliana na fangasi sehemu za siri kwa wanaume
Soma Zaidi...