Posti hii inahusu zaidi malengo ya kutibu ukoma, ni malengo ambayo yamewekwa na wizara ya afya ili kuweza kutokomeza ukoma kwenye jamii
Malengo ya kutibu ugonjwa wa ukoma.
1.Tunajua kabisa ukoma ni Ugonjwa ambao ushambulia sehemu mbalimbali za mwili kama vile kwenye miguu na mikono na mara nyingi uondoa vidole vya kwenye miguu na mikono na mgonjwa huyo anakuwa hasikii maumivu ila uona kidole kinaondoka kwa sababu wadudu wanaharibu mfumo wa Neva system na kumfanya mgonjwa hasisikie maumivu wakati vidole vinapokuwa vinadondoka, kwa hiyo malengo ni kama ifuatavyo.
2.Kuzuia kuaribika kwa nevu na tisu nyingine kwenye mwili wa binadamu, kwa sababu ya kuwepo kwa bakteria kwenye mwili usababisha nevu kuaribika na kuaribika kwa tishu kwa hiyo dawa mbalimbali zimeweza kupatikana na kuweza kupunguza ugonjwa huu kwa sasa ni Watu wachache ambao wanapatwa na ugonjwa kama huu kwa sababu ya kuwepo kwa dawa.
3. Kuzuia ugonjwa huu kusambaa kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine.
Tunajua kubwa ugonjwa huu una tabia ya kusambaa kwa hiyo ikiwa kwenye familia amepata mtu mmoja na kama haujatibiwa anaweza kumwambikiza mtu mwingine na kusababisha kuwepo kwenye familia na kwa jamii ambazo zina imani potovu wanaweza kusema kuwa ni Ugonjwa wa familia kumbe ni kwa sababu ya kutotibu ugonjwa huu kwa hiyo jamii inapaswa kujua na kutibu ugonjwa huu mapema kabla haujaanza kusambaa.
4.Kutokomeza kabisa ugonjwa huu.
Lengo kuu la afya ni kuhakikisha kwamba ugonjwa huu inatokomezwa kwanza kwa kutambua mazingira ambapo Ugonjwa huu upo kwa kiasi kikubwa, kutoa elimu hasa vijijini ili kutowatenga na kuwafukuza majumbani mwao wagonjwa wa ukoma, kuihakikishia jamii kuwa ugonjwa huu unatibika na pia kutibu ugonjwa huu kwa dawa zilizopendekezwa, kwa kufanya hivyo ugonjwa huu utapungua.
5.Kws hiyo mpaka sasa kwenye jamii ugonjwa huu umepungua kwa kiwango kikubwa mno kwa hiyo elimu inapaswa kuendelea kutolewa ili kuweza kutokomeza kabisa ugonjwa huu na inawezekana ukatokomezwa kwa hiyo tujue kuwa ugonjwa huu upo na unatibika na dawa zipo na wengi wamepona
Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetuUmeionaje Makala hii.. ?
Maumivu ya shingo ni malalamiko ya kawaida. Misuli ya shingo inaweza kuchujwa kutokana na mkao mbaya - iwe inaegemea kwenye kompyuta yako kazini au kuwinda benchi yako ya kazi nyumbani.
Soma Zaidi...Somo hili linakwenda kukueleza jinsi ya kumfanyia huduma ya Kwanza kwa mtu aloanguka kifafa
Soma Zaidi...Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu huduma ya Kwanza kwa mtu anayetokwa na damu ya pua
Soma Zaidi...Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu namna ambavyo mwili unapambana na maradhi
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi namna ya kutunza nywele za mgonjwa hasa kwa wagonjwa mahututi na wale wasiojiweza tunafanya hivyo ili tuweze kuwatoa kwenye hali ya usafi.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi namna ya kuchoma chanjo, ni njia ambazo utumika kutoa chanjo kwa watoto na watu wazima kwa utaratibu uliowekwa.
Soma Zaidi...Post hii inahusu zaidi mambo yanayochangia Ili dawa iingie vizuri kwenye damu, na mambo yanayoweza kusababisha dawa kuingia au kutoingia vizuri kwenye damu.
Soma Zaidi...Hii ni hali inayotokea ambapo wili unakuwa na joto la juu sana tofauti na kawaida.
Soma Zaidi...Post hii inahusu zaidi namna ya kuwasaidia wagonjwa wa vidonda vya tumbo, ni njia ya kuwasaidia wagonjwa waliopata madonda ya tumbo
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi imani potofu waliyonayo Watu kuhusu ugonjwa wa kifua kikuu, hizi ni imani ambazo uwepo kwenye jamii na pengine uweza kuaminika lakini si za ukweli.
Soma Zaidi...