image

Mambo ambayo hayafunguzi funga

Hii ni orodha ya mambo ambayo hayawezi kuharimu funga yako endapo utayafanya.

Yasiyobatilisha funga

Kuna baadhi ya mambo ambayo mtu aliyefunga akiyafanya, anaweza kujiona kuwa amefungua lakini bado hajafungua. Miongoni mwa mambo haya ni:

 


(i)Kula au Kunywa kwa Kusahau

 


Mtu akiwa amesahau kuwa amefunga akala au akanywa kiasi chochote, hata kiasi cha kushiba, bado atakuwa na swaumu kwa ushahidi wa Hadith zifuatazo:
Abu hurairah(r.a) amesema kuwa Mtume (s.a.w) amesema: “Anayefungua Ramadhani kwa kusahau hatalipa wala hatatoa kafara” (Daral Qutni, Bayhaqi na Hakim).
Abu Hurairah ameeleza kuwa Mtume wa Allah amesema: Yeyote yule atakayesahau akala au akanywa wakati amefunga, na amalizie funga yake kwa sababu Allah (s.w) amemlisha na kumnywesha ”. (Bukhari na Muslim).

 


Hali kadhalika, kama mtu atalishwa au kunyweshwa au kufuturishwa kwa namna yoyote ile kwa kutezwa nguvu, saumu yake haitabatilika:
Ibn Abbas (r.a) ameeleza kwamba Mtume (s.a.w) amesema: “Mwenyezi Mungu ameuondolea umati wangu (Jukumu la) kukosea, kusahau na waliotezwa nguvu.” (Ibn Majah, Ta bran na Hakim).

 


(ii)Kuoga wakati umefunga

 


Kuoga kwa kujimwagia maji au kujitumbukiza majini hakuharibu funga kwa maana imepokelewa kwamba Mtume (s.a.w) alikuwa akijimwagia maji kichwani kwa sababu ya kiu au joto, hali amefunga:

 


Mmoja wa Maswahaba ameeleza: Hakika nimemuona Mtume (s.a.w) akiwa Arji (bonde moja kati ya Makka na Madina) akijimwagilia maji kichwani mwake akiwa amefunga kwa sababu ya kiu au joto. (Malik, Abu Daud).

 

(iii)Kutokwa na Manii
Mtu akitokwa na manii kwa kuota au kwa namna ambayo hakukusudia, atakuwa hajafungua.

 


(iv)Kuamka na Janaba

 


Kuamka na janaba hakufunguzi kwani Mtume (s.a.w) wakati mwingine alikuwa anaamka na janaba na huku amefunga.
Aysha (r.a) ameeleza kuwa alfajiri iliingia wakati Mtume (s.a.w) yuko katika janaba. Kisha alioga na kuendelea na swaumu. (Bukhari na Muslim).
Hali kadhalika mwenye hedhi au nifasi, ambaye damu yake ilikoma kabla ya alfajiri, akiamka atafunga hata kama atakuwa hajaoga.
(v)Kubusiana na kukumbatiana Mume na Mke

 


Mtu kumbusu na kumkumbatia mkewe au mumewe wakati amefunga haiharibu funga iwapo kuna haja ya kufanya hivyo alimradi tu waweze kujizuia wasiendelee zaidi ya hapo. Hivi ndivyo tunavyojifunza katika Hadithi ifuatayo:
Aysha (r.a) ameeleza kuwa Mtume wa Allah alikuwa akimbusu na kumkumbatia wakati amefunga na alikuwa mw enye kumiliki matashi yake kuliko yeyote miongoni mw enu (Bukhari na Muslim).

 


Amehadithia baba wa Hisham kuwa: Aysha (r.a) amesema: “Mtume wa Allah alikuwa akiwabusu baadhi ya wake zake akiwa amefunga: na kisha akacheka. (Bukhari).
Miongoni mwa Masahaba walioruhusu hili la mtu kumbusu na kukumbatia mkewe wakati amefunga ni Sayyidna Umar (r.a), Ibn Abbas (r.a.), Abu-Hurairah (r.a) na Bibi Aysha (r.a). Kwa maoni ya Imam Abu Hanifa na Shafii, kumbusu na kumkumbatia wakati mtu amefunga ni makruhu iwapo kutaamsha matamanio. Vinginevyo si makruhu, lakini ni bora kuacha iwapo hapana haja ya lazima kufanya hivyo.

 


(vi)Kupiga Mswaki

 


Si vibaya kupiga mswaki wakati mtu amefunga kwani Mtume (s.a.w) alikuwa akipiga mswaki wakati amefunga kama tunavyofahamishwa katika Hadith zifuatazo:
Amr bin Rabiyah (r.a) ameeleza: Nilimuona mtume (s.a.w) Mara nyingi nisizoweza kuhesabu akipiga msw aki akiwa amefunga.(Tirmidh na Abu Da ud).

 

Amesimulia Abu Hurairah(r.a) kuwa Mtume (s.a.w) amesema: Si kwa kuw a ninahofia kuw a litakuw a jam bo zito kw a umm ati w angu, ningekuw a nimeshawaamrisha kutumia mswaki (kupiga mswaki) kila wakitawadha. (Bukh ari).

 


Hadith hii haikubagua mtu aliyefunga na asiyefunga. Bali tunapata fundisho kuwa kupiga mswaki ni kitendo kilichosisitizwa sana.
Bibi Aysha (r.a) ameeleza kuwa Mtume wa Allah amesema: “Mswaki hutakasa mdomo na ni njia ya kutakia Radhi za Allah (s.w). ” (Bukhari).

 


(vii)Kusukutua na kupandisha Maji Puani

 


Wakati mtu anatawadha anaruhusiwa kusukutua na kupandisha maji puani lakini asifanye sana mpaka maji yakaingia ndani kwani hilo amelikataza Mtume (s.a.w) katika Hadith iliyopokelewa na Abu Daud, Tirmidh, Ibn Majah na Nasai.

 


(viii)Kupaka Wanja na Dawa ya Machoni

 


Kupaka wanja kunaruhusiwa kwa mtu aliyefunga Mtume (s.a.w) ameruhusu hilo katika Hadith ifuatayo:
Anas(r.a) ameeleza kuwa mtu mmoja amekuja kwa Mtume (s.a.w) na akasema: “Ninaumwa macho. Ninaweza kupaka wanja wakati nimefunga? `Ndio’ Alijibu Mtume (s.a.w).”

 


Pia dawa ya macho iwe ya mafuta au ya maji inaruhusiwa kutumiwa wakati mtu amefunga kwa sababu hapana tundu la kuungana moja kwa moja na koo kama yalivyo matundu ya pua na masikio.

 


(ix)Kumeza usichoweza kujizuia nacho
Ukimeza vitu usivyoweza kujizuia kama vile mate, kohozi, vumbi la njiani, vumbi la unga, kumeza mdudu aliyeingia kwa ghafla hadi kooni, n.k. utakuwa hujafungua.

 


(x)Kujipaka mafuta au manukato
Kujipaka mafuta au manukato mwilini au nguoni, kunusa manukato, kujifukiza udi na ubani, n.k. hakuharibu funga.

 


(xi)Kuumika au kutoa Damu
Kuumika hakufunguzi kwani Mtume (s.a.w) amefanya hivyo wakati akiwa amefunga kama tunavyofahamishwa katika Hadith ifuatayo:
Amehadithia Ibn Abbas (r.a) kwamba Mtume (s.a.w) aliumikwa akiwa katika “Ihram” na pia akiwa amefunga. (Bukhari).

 

Hata hivyo, kama kuumika huko kutamfanya mtu awe dhaifu, basi itakuwa ni makruhu. Hali kadhalika mtu anaruhusiwa kutoa damu kwa ajili ya kuwasaidia wagonjwa (blood transfusion), akiwa amefunga.

 


(xii) Kupiga Sindano
Kupiga sindano ya dawa, iwe ya mshipa au chini ya ngozi, haifunguzi.





           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 1016


Sponsored links
👉1 Kitau cha Fiqh     👉2 Kitabu cha Afya     👉3 Madrasa kiganjani     👉4 kitabu cha Simulizi    

Post zifazofanana:-

Zijuwe funga za sunnah na jinsi ya kuzifunga
Post hii inakwenda kukufundisha kuhusu funga za sunnah na jinsi ya kuzigunga. Soma Zaidi...

Maana ya Swaumu na Lengo la kufunga
Soma Zaidi...

Kwa nini imefaradhishwa kufunga katika Mwezi wa ramadhani?
Soma Zaidi...

Nguzo za udhu ni sita
Post hii itakufundisha kuhusu nguzo kuu sita za udhu. Soma Zaidi...

Mifumo ya benki na kazi zake
Hapa utajifunza kazi za benki. Soma Zaidi...

Taratibu za kumiliki hisa na mali ya shirika
Katika Uislamu kuwa na hisa kwenye mali inaruhusiwa. Hapa utajifunza taratibu za kumiliki hisa. Soma Zaidi...

NAMNA YA KUSWALI SEHEMU YA KWANZA
Mtume (s. Soma Zaidi...

Usawa katika uchumi wa kiislamu
5. Soma Zaidi...

Utaratibu wa kuzika maiti ya kiislamu, hatua kwa hatua
Kuzika Kuzika ni kitendo cha nne cha faradh tunacho lazimika kumfanyia ndugu yetu aliyetutangulia kufa. Soma Zaidi...

Hizi ndio suna za swala kwa swala za faradhi na suna
Soma Zaidi...

Kumuandaa maiti punde baada ya kufariki dunia
Soma Zaidi...

Ni mambo gani haramu kwa mtu asiyekuwa na udhu?
Soma Zaidi...