image

mambo ambayo utaulizwa mama mjamzito ukifika kituo cha afya unatakiwa utoe majibu sahihi.

Posti hii inahusu zaidi mambo ambayo Mama mjamzito anaweza kuulizwa pindi anapokuja kwenye kliniki ya uzazi ,ni mambo muhimu na ya lazima yanayopaswa kuongea na Mama mjamzito ili kuweza kuona maendeleo yake kama ifuatavyo.

Mambo muhimu ya kuongea na Mama mjamzito.

1. Maelezo kwa ujumla kuhusu Mama.

Maelezo kwa ujumla kuhusu mama kama vile kuna la mama, mme wake, sehemu anapoishi, miaka yake, kazi yake, kazi ya mwanaume, umri wa mwanaume ,jina mwenyekiti wa kijiji na number ya simu hayo yote uulizwa na mwanamke ili kuweza kujua wazi hali yake ingawa kama kitu chochote kimetokea iwe rahisi kumpata au kuna wanawake wengine ambao huwa wanaacha makusudi kwenye mahudhurio kwa kutumia maelezo kwa ujumla ni rahisi kumpata Mama huyo na kuweza kumpatia huduma za muhimu kwa hiyo ni kuhakikisha kujua hali halisi ya Mama.

 

2.Kujua juu ya mimba za Mama.

Kwa mama mjamzito akija kwenye mahudhurio ni lazima kujua hali ya mimba zake kwa ujumla kwa mfano mimba aliyonayo ni ya ngapi, amezaa watoto wangapi, je walio hai ni wangapi, ambao wamekufa ni wa ngapi au ni mimba ngapi zimetoka kwa kufanya hivyo tunaweza kuja matatizo aliyo nayo Mama katika kujifungua, kwa mfano kama mimba zimetoka tunaweza kujua chanzo cha kutoka kwa mimba na kupata tiba au kama watoto wanafariki kwa mda fulani tunaweza kujua sababu kwa hiyo kwa watoa huduma wanapaswa kuuliza mama kuhusu mimba zake zikoje na kama kuna tatizo liweze kutatuliwa.

 

3. Kuhakikisha kuwa Mama anajua miezi ya mimba yake na kujua tarehe ya kujifungua.

Mama akija kwenye mahudhurio anapaswa kujua wazi  siku ya kujifungua ambapo mhudumu wa afya ambaye ana ujuzi anaweza kumwesabia  Mama kuanzia siku ya kwanza ya  mwezi wa mwisho wa kuona siku za ke za mwezi na Mama akishaambiwa siku ya matarajio ya kujifungua anaanza kujiandaa taratibu na akisikia mabadiliko anaweza kwenda hospitali au kituo cha afya, na pia Mama anapaswa kujua wazi mda wa mimba yake ambapo kazi hiyo usaidiwa na mhudumu wa afya kuhakikisha kuwa Mama anajua wazi mda wa mimba yake.

 

4. Mzio au aleji yoyote kwa dawa na chakula.

Mama anapaswa kuongea na mhudumu wa afya kuhusu mzio wowote wa dawa na vyakula kwa sababu kila mahudhurio mama anapaswa kupewa dawa za minyoo,  dawa za kumzuia mtoto hasipatwe na Malaria kwa kitaalamu dawa hizo huitwa sp na pia Mama anapaswa kupewa dawa za kuongeza damu ili akija kujifungua awe na damu ya kutosha , kwa kupewa dawa hizo Mama anapaswa kuwa wazi kama kuna dawa yoyote inayoletea mzio au aleji na kuweza kuibadilisha kwa hiyo tuwe makini kwa kujua mizio ya kila Mama.

 

5. Kumuuliza Mama kama anatumia vileo na Mambo mengine kama hayo.

Kitu kingine ni kumuuliza  kuhusu matumizi ya pombe kali, madawa ya kulevya, na vitu vingine ambavyo utumiwa na wanawake wajawazito ambavyo kwa kitaalamu huitwa PICA vitu hivyo ni kama pembe, kula udongo,kula mkaa na vitu kwa ujumla ambavyo si vyakula vitu hivyo huwa havina faida yoyote kwenye mwili na pia Mama wajawazito wanapaswa kuelewa wazi madhara ya madawa ya kulevya, pombe na sigara kwa watoto na kuachana navyo wakati wa ujauzito.

 

6. Pia Mama anapaswa kuhimizwa kuhusu chanjo na milo anayoitumia kila siku.

Kwa kawaida tunajua kuwa wajawazito wanapaswa kupata chanjo mbalimbali kama vile Tetunus na vitamini A hizi chanjo umkinga mototo kutokana na magonjwa na pia vitamini A uepusha upofu wa mtoto kwa hiyo Mama anapaswa kupata chanjo ambazo ni za lazima na pia Mama mjamzito anapaswa kula na kushiba vizuri anapaswa kula milo mitano kwa siku kama ifuatavyo, kifungua kinywa cha asubuhi, saa nne au tano anapaswa kupata chochote, chakula cha mchana, saa kumi apate chochote na jioni mlo wa usiku.            

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2022/01/10/Monday - 11:25:03 pm     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 1085


Download our Apps
👉1 Kitau cha Fiqh     👉2 kitabu cha Simulizi     👉3 Madrasa kiganjani     👉4 Kitabu cha Afya    

Post zifazofanana:-

kunauwezekano wa darri ya kchefuchefu ictokee kabsa kwa mjauzito
Kichefuchefu ni moja katika dalili za mimba za mapema, Lucinda je upo uwezekano kwa mwanamke kuwa na ujauzito bila hata ya kuwa na kichefuchefu? Soma Zaidi...

Je endapo mama atafanya tendo la ndoa wiki moja kabla ya kuingia hedhi anaweza kupata ujauzito?
Zipo siku maalumu ambazo mwanamke hupata mimba. Siku hizi huzoeleka kwa jina la siku hatari. Je ungependa kufahamu mengi kuhusu siku hatari, endelea na makala hii. Soma Zaidi...

Umuhimu wa uzazi wa mpango kwa Mama
Posti hii inahusu zaidi faida za uzazi wa mpango kwa akina Mama, tunajua wazi kubwa kuna faida kubwa za uzazi wa mpango kwa akina Mama pindi watumiapo njia hizi kwa uhakika zaidi. Soma Zaidi...

Maambukizi kwenye kitovu cha mtoto.
Posti hii inahusu zaidi Maambukizi kwenye kitovu cha mtoto, ni Maambukizi ambayo yanaweza kutokea kwenye kitovu cha mtoto pale ambapo mtoto amezaliwa inawezekana ni kwa sababu ya hali ya mtoto au huduma kuanzia kwa wakunga na wale wanaotumia mtoto. Soma Zaidi...

Dalili ninazoziona kwangu chuchu zinauma na sjapata period mwezi huu na nlishiriki tarehe 19 mwezi wa tisa
Nini humaanisha kama chuchu zinauma na hupati period mwanaidi mrefu. Soma Zaidi...

Dalili za mimba kuanzia siku 7 Hadi 14
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu dalili za mimba kuanzia siku 7 Hadi 14 Soma Zaidi...

Dalili za mimba changa
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu dalili za mimba changa Soma Zaidi...

Umuhimu wa kunyonyesha kwa Mama
Posti hii inahusu zaidi umuhimu wa kunyonyesha kwa akina Mama, kunyonyesha ni kitendo ambacho Mama utumia maziwa yake na kumlisha mtoto pindi tu anapozaliwa mpaka wakati anapoachishwa titi, kunyonyesha huwa na faida kubwa kwa wote yaani Mama na mtoto, zif Soma Zaidi...

Umuhimu wa kumpeleka mtoto kliniki
Posti hii inahusu zaidi umuhimu wa kumpeleka mtoto kliniki, kliniki nisehemu ambayo mtoto hupelekwa Ili kujua maendeleo ya mtoto akiwa chini ya umri wa miaka mitano Soma Zaidi...

Maumivu ya uume baada ya tendo la ndoa
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu maumivu ya uume baada ya tendo la ndoa Soma Zaidi...

Je bado unasumbuliwa na nguvu za kiume?
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu njia za kuondoa tatizo la nguvu za kiume Soma Zaidi...

Je matiti kujaa na chuchu kuuma inakua ni dalili za hedhi?
Kuunda na kujaa kwa matiti ni miongoni mwa dalili za ujauzito lakini pia ni dalili za kukaribia hedhi kwa baadhi ya wanawake. Posti hii itakwenda kufafanuabutofauti wa dalili hizi na kipi ni sahihibkatibya hedhi ama ujauzito. Soma Zaidi...