Mambo anayofanyiwa maiti baada ya kufa
Dhana ya faradh kwa muislamu (EDK form 2:dhana ya elimu ya uislamu)
Mambo anayofanyiwa mtu (maiti) mara tu baada ya kufa.
Baada ya mtu kufa inatuwajibikia tuseme: “Innalillah wainnailaihraaji’una”. Qur’an (2:156). Kisha kumfanyia maiti mambo yafuatayo:
- Kwa taratibu kurudishia mdomo wake usiwe wazi kwa kufunga kwa kitambaa kutoka kidevuni na kuzungushia kichwani.
- Kufunga macho ya marehemu na huku ukisema;
“Kwa jina la Allah na kwa kufuata mila ya Mjumbe wa Allah, Ewe Mola wetu mrahisishie mambo yake ya sasa na msahilishie mambo yake ya baadaye. Na jaalia anayokutanayo yawe bora kuliko aliyoyaacha.”
- Lainisha viungo vyake (miguu na mikono) kwa kukunja na kukunjua taratibu.
- Kama kuna ugumu maji ya uvuguvugu au mafuta yanaweza kutumika kulaisha na kunyoosha viungo hivyo.
- Baada ya kulainisha viungo, miguu na mikono inyooshwe na kulazwa uso ukielekezwa Qibla kwenye mkeka au kitanda kisicho na godoro.
- Maiti avuliwe nguo zote alizokufa nazo na kisha kufunikwa kwa shuka kubwa
- Ni vyema afunwe kitambaa tumboni au kuwekewa kitu kizito ili tumbo lisifutuke.
- Marashi na ubani vitumike kwa wingi ili kuzima harufu ya uvundo wa maiti.
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
👉1 Tafasiri ya Riyadh Swalihina 👉2 Bongolite - Game zone - Play free game 👉3 kitabu cha Simulizi 👉4 ai web app 👉5 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w) 👉6 web hosting
Post zinazofanana:
Dalili na ishara za jeraha kwenye ngozi
Posti hii inaonyesha dalili,sababu na mbinu za kutoa huduma ya kwanza kwa aliyepata jeraha kwenye ngozi kwa kuingiliwa na kitu Kama mwiba,Pini,sindano n.k
Soma Zaidi...Nafsi ya mwanadamu inavyothinitisha uwepo wa Allah
Mwanadamu ukifikiria vyema. Kuhusu nafsi yako, hakika utapatabfikra yabuwepp wa Mwenyezi Mungu
Soma Zaidi...Ushahidi juu ya kosa la Uzinifu
Ushahidi wa kuthibitisha kutendeka kwa kosa la uzinifu unapatikana kwa namna tatu zifuatzo: (i)Kushuhudia tendo hilo likifanyika kwa wakati mmoja watu wanne Mukalafu (Walio baleghe na wenye akili timamu), wakiwa ni Waislamu waadilifu.
Soma Zaidi...