Mambo ya kuangalia kwa mtoto mdogo

Posti hii inahusu zaidi mambo ya kuangalia kwa mtoto mdogo chini ya umri wa miaka mitano ili kuweza kuweka afya yake kwenye njia safi.

Mambo ya kuangalia kwa mtoto mdogo chini ya umri wa miaka mitano.

1.Kwa kawaida tunajua wazi kubwa watoto wadogo chini ya miaka mitano ushambuliwa sana na Magonjwa mbalimbali na tiba mbalimbali zimeshatolewa kwa watoto hao kwa kupitia sehemu mbalimbali.yafuatayo ni mambo ya kuangalia kwa mtoto ili kuweza kupunguza Magonjwa kwa watoto kwa hiyo tunapaswa kuangalia yafuatayo.

 

2. Tunapaswa kuangalia Dalili za hatari kwa mtoto kama mtoto anakula au ananyonya, kuangalia kwa mtoto anatapika kila kitu , pia kuangalia kama mtoto anaanguka kifafa na kufanya kumtibu mara moja.

 

3. Pia tunapaswa kuangalia Dalili za Magonjwa kama vile kukohoa, kupumua kwa shida, kuharisha,homa na Dalili nyingine za Maambukizi kwenye sikio.

 

4. Pia tunapaswa kuangalia Magonjwa mbalimbali kama vile Surua, kuishiwa na damu na kuwa na mlo ambao hauridhishi kwa mtoto.

 

5. Pia tunapaswa kuangalia kama mtoto amepata chanjo zote ambazo zinapaswa kupewa kwa mtoto kama vile chanjo ya Surua, kifua kikuu, kifadulo, Dondakoo, polio na chanjo zote anazopaswa kupewa mtoto.

 

6. Pia Maambukizi kwa mtoto yanapaswa kuangaliwa kama vile Maambukizi ya madonda mkononi, Maambukizi ya virus vya ukimwi na Magonjwa mbalimbali.

 

7.kwa hiyo tunaona wazi kuwa mtoto chini ya miaka mitano wanahitaji uangalizi zaidi kwa hiyo hata mtoto akipata homa ni lazima apelekwe hospitali kwa uangalizi zaidiJe! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2022/02/18/Friday - 11:02:48 pm     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 897

Post zifazofanana:-