image

Mambo ya kuangalia kwa mtu aliyepoteza fahamu

Posti hii inahusu zaidi mambo ya kuangalia kwa mtu aliyepoteza fahamu, kama mtu amepoteza fahamu Kuna mambo muhimu yanapaswa kuangaliwa kwa makini kama ifuayavyo.

Mambo ya kuangalia kwa aliyepoteza fahamu.

1. Kwanza kuangalia kama mgonjwa anapumua.

Kitu Cha kwanza kuangalia kama mtu amepoteza fahamu ni kuangalia kama mgonjwa anapumua, kama hapumui unaangalia mdomoni kama Kuna kitu labda kimeziba mdomoni pia angalia puani labda Kuna michanga imeziba hasa kwa waliopata ajali, ukikuta Kuna kitu chochote unapaswa kukitoa Ila uwe mwangalifu unapotoa vitu mdomoni usije ukavisukuma kwenye mfumo wa hewa, kwa hiyo hakikisha mgonjwa wako anapumua ndipo uendelee na mambo mengine.

 

2. Kuangalia kiwango Cha damu kinachotoka , kwa hiyo mgonjwa kama anatokwa na damu nyingi zinapaswa kuzuia kwa kufunga sehemu ambapo damu zinatokea, kama damu zinaendelea kutoka mgonjwa anapaswa kumpelekwa hospitalini haraka ipasavyo Ili kuongeza kiwango Cha damu. Kama ni kidogo mgonjwa anaweza akafungwa na huduma nyingine zinaweza kuendelea.

 

3. Kuangalia chanzo Cha kupoteza fahamu.

Baada ya kufanya hayo yote tunapaswa kujua chanzo Cha kupoteza fahamu ni nini? Kama ni mshutuko wa Moyo au kama ni kushuka kwa sukari au kama ni tatizo la moyo na mambo mengine ambayo usababisha kupoteza fahamu, ukisha tambua chanzo Cha kupoteza fahamu unaanzia kutibu kadri ya chanzo, mfano kama ni kushuka kwa sukari mpe mgonjwa vitu vya sukari au kama ni kuishiwa maji mwilini mgonjwa anapaswa kuongezewa maji na mengineyo.

 

4. Kama unaona hali ya mgonjwa haiwezekani kutibiwa kwa kutumia huduma ya kwanza mpeleke mgonjwa haraka sana hospitalini Ili aweze kupatiwa matibabu zaidi.kwa hiyo tunapaswa kujua kuwa ugonjwa wa kupoteza fahamu upo na sababu nyingine zinaweza kutibiwa kwa kutumia huduma ya kwanza lakini hali ya mgonjwa isipobadilika mgonjwa anapaswa kumpelekwa hospitalini haraka Ili apatiwe matibabu zaidi.





           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 771


Sponsored links
👉1 Madrasa kiganjani     👉2 Kitau cha Fiqh     👉3 Kitabu cha Afya     👉4 kitabu cha Simulizi    

Post zifazofanana:-

Jinsi mimba inavyotungwa mpaka mtoto kuingia kwenye mfuko wa uzazi
Post hii inahusu zaidi namna mimba inavyotungwa mpaka mtoto kuingia kwenye mfuko wa uzazi, mimba kutungwa ni kitendo ambapo mbegu za kiume kuungana na yai la kike na kutengeneza zygote. Soma Zaidi...

Ratiba ya chanjo ya polio
Posti hii inahusu zaidi namna chanjo ya polio inavyotolewa na ratiba zake yaani kuanzia siku ya kwanza mpaka pale mtoto anapomaliza chanjo hii kwa hiyo tuone ratiba ya chanjo ya polio. Soma Zaidi...

Njia za kukabiliana na presha ya kupanda/hypertension
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu njia za kukabiliana na presha ya kupanda Soma Zaidi...

Aina mbalimbali za maumivu ya mwili.
Posti hii inahusu zaidi aina mbalimbali ya maumivu ya mwili, Maumivu ya mwili utokea kwa aina mbalimbali kama ifuatavyo. Soma Zaidi...

Jinsi macho yanavyoweza kuzungumza kuhusu afya yako ya kimwili na kiakili
Soma Zaidi...

Kushiriki ngono na mtu aliye na vvu na ukimwi
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu kushiriki-ngono-na-mtu-aliye-na-vvu-na-ukimwi Soma Zaidi...

Sababu za kumwosha Mgonjwa mwili mzima.
Posti hii inahusu zaidi sababu za kumwosha Mgonjwa mwili mzima,ni sababu ambazo umsaidie mgonjwa ili aweze kupata nafuu mapema na kumsaidia kama tutakavyoona hapo chini Soma Zaidi...

Huduma kwa watu wanaoishi na virusi vya Ukimwi
Posti hii inahusu zaidi huduma ambazo wagonjwa wanaoishi na maambukizi ya virus vya ukimwi wanaweza kupata, huduma hii utolewa hasa kwa wale ambao wamejitokeza kupima afya zao na kujua wazi hali zao na kwa wale wanaofatilia huduma hii wanaweza kuishi vizu Soma Zaidi...

Dalili za unyanyasaji wa kimwili
Unyanyasaji wa kimwili. Unyanyasaji wa watoto kimwili hutokea wakati mtoto amejeruhiwa kimwili kimakusudi. Unyanyasaji wa kijinsia. Unyanyasaji wa watoto kingono ni shughuli yoyote ya kingono na mtoto, kama vile kumpapasa, kushikana mdomo na sehemu Soma Zaidi...

Njia za kuingiza chanjo mwilini
Posti hii inahusu njia mbalimbali ambazo utumika kupitisha chanjo, njia hizo utegemea na kazi ya chanjo kama ifuatavyo. Soma Zaidi...

Njia za kuzuia damu isiendelee kuvuja
Posti hii inahusu zaidi njia za kuzuia damu isiendelee kuvuja, ni njia ambazo utumika ikiwa kuna damu inavuja kwenye sehemu yoyote ya mwili,kwa hiyo tunaweza kutumia njia hizi ili kuepuka kuendelea kuvuja kwa damu. Soma Zaidi...

HUDUMA YA KWANZA KWA ALIYENG’ATWA NA NYUKI
Kung’atwa na nyuki kunaweza kukahitaji huduma ya kwanza kwa haraka kama mgonjwa ana aleji na nyuki. Soma Zaidi...