Mambo ya kuzingatia kabla ya kugawa mirathi
Haya ni mamno muhimu yanayozingatiwa kabla ya kuanza zoezi la kugawa mirathi ya marehemu.
Mambo ya kuzingatia kabla ya kugawanya urithi
Kabla mali ya marehemu haijagawanywa kwa warihi wake, hapana budi kuzingatia yafuatayo:
(a)Haki zilizofungana na mali ya urithi:
Mali ya marehemu haitakuwa halali kwa warithi wake mpaka zitolewe haki zifuatazo:
(i)Madeni.
(ii)Zakat.
(iii)Gharama za makazi ya mkewe katika kipindi cha eda.
(iv)Usia ambao hauzidi theluthi moja (1/3) ya mali yote iliyobakia.
(b)Sharti Ia kurithi:
Kurithi kuna sharti tatu:
(i)Kufa yule mwenye kurithiwa (Si halali kurithi mali ya mtu aliye hai).
(ii)Kuwepo hai mrithi wakati akifa mrithiwa. Kwa mfano, kama wawili wanaorithiana mathalani baba na mtoto wote wamekufa. Aliyekufa nyuma (au aliyeshuhudia kifo cha mwenzie) atakuwa mrithi wa yule aliyetangulia kufa.
(iii)Kukosekana mambo yenye kumzuilia mtu kurithi.
(c)Mambo yanayomzuilia mtu kurithi
Mrithi huzuilika kurithi itakapopatikana na moja kati ya sababu zifuatazo:
(i)Kumuua amrithiye: Yaani mtu hatamrithi aliyemuua ijapokuwa kwa bahati mbaya.
Abu Hurairah (r.a) ameeleza kuwa Mtume wa Allah amesema Mwenye kuua hapati chochote katika mirathi. (Tirmidh, Ibn Majah).
(ii)Kuhitalifiana katika dini:
Muislamu hamrithi kafiri, mshirikina, mkristo au myahudi na wala kafiri, mshirikina, mkristo au myahudi hatamrithi Muislamu hata akiwa karibu naye kiasi gani katika nasaba.
Usama bin Zaid (r.a)ameeleza kuwa mtume wa Allah amesema: Muislamu hamrithi mshirikina wala mshirikina hamrithi Muislamu. (Bukhari na Muslim)
Pia Mtume (s.a.w) amesema katika Hadithi iliyosimuliwa na Abdullah bin Amri(r.a) kuwa: Watu wa dini mbili tofauti hawatarithiana. (Abu Dauwd, Ibn Majah, Tirmidh).
(iii)Mtoto aliyezaliwa nje ya ndoa hana haki ya kumrithi baba aliyemzaa na baba hana haki katika mirathi yake, kama tunavyojifunza katika Hadith ifuatayo:
Amri bin Shuab(r.a) ameeleza kutoka kwa baba yake naye kutoka kwa babu yake kuwa Mtume wa Allah amesema: "Atakayezini na mwanamke muungwana au na mjakazi, mtoto atakayepatikana humo hana haki naye. Hatomrithi na wala hatarithiwa naye ". (Tirmidh)
(d)Sababu za Kurithi:
Mtu hurithi kwa sababu moja katika hizi:
(i)Kuwa na nasaba na marehemu (baba, mama, mtoto, ndugu, n.k.). (ii)Kuoana kwa ndoa halali (yaani mume humrithi mke na mke humrithi mumewe).
(iii)Kuacha huru, yaani mwenye kumpa uhuru mtumwa humrithi huru wake.
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
👉1 kitabu cha Simulizi 👉2 web hosting 👉3 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w) 👉4 Kitau cha Fiqh 👉5 Kitabu cha Afya 👉6 Bongolite - Game zone - Play free game
Post zinazofanana:
Aina za twahara na aina za najisi
Katika post hii utakwenda kuzijuwa aina za twahara katika uislamu. Utaviona vigawanyo vya twahara kulingana na maulamaa wa Fiqh
Soma Zaidi...Sanda ya mwanamke na namna ya kumkafini
Mambo ya faradh kwa maiti ya muislamu (EDK form 2: Dhana ya elimu ya uislamu)
Soma Zaidi...Jinsi ya kumuosha maiti wa kiislami mwanaume au mwanamke
Post hii inakwenda kukufundisha hatuwa kwa hatuwa jinsi ya kumuosha maiti wa kiislamu
Soma Zaidi...Jinsi ya kushona sanda ya maiti na kumvisha yaani kumkafini
Hapa utajifunza taratibu za kumkafini maiti wa kiislamu. Yaani kushona sanda yake na kumvisha.
Soma Zaidi...Taratibi za malezi ya watoto wadogo baada ya talaka katika uislamu
Endapo mke na mume wameachana na hali ya kuwa mke ana watoto wachanga. Je uislamu unasemaje kuhusu taratibu za malezi?
Soma Zaidi...