image

Mambo ya kuzingatia kwa mama ili apate huduma endelevu.

Posti hii inazungumzia kuhusiana na huduma kwa mama wajawazito na waliojifungua.

Mama mjamzito akiona Dalili zifuatazo awahi kituo Cha afya

1.kutokwa na Damu ukweni.

2.mtoto Kupunguza au kuacha kucheza tumboni.

3.maumivu makali ya tumbo.

4.maumivu makali ya kichwa.

5.kushindwa kuona vizuri.

6.kutokwa na majimaji ukweni.

7.Homa Kali.

 

Mambo ya kuzingatia kwa mama ili apate huduma endelevu.

1.Aanze kliniki ya ujauzito pale tu atakapojihisi ana mimba.

2.Ahudhurie mahudhurio ya kliniki yote nane.

3.ajifungulie katika kituo Cha huduma ya afya.

4.ahudhurie kliniki baada ya kujifungua Ndani ya siku tatu, baada ya siku ishirini na nane na baada ya siku Arobaini na mbili 42.

5.mama mjamzito anahitaji kula vyakula vyenye virutubisho vya kutosha ili aweze kukidhi mahitaji yake ya kilishe ya kila siku pamoja na Mtoto aliye tumboni.

6.anahitaji kula mlo kamili wenye mchanganyiko kutoka katika makundi matano vinavyopatikana katika jamii ya maziwa, matunda na mbogamboga, nyama,mayai,nafaka na jamii ya kunde.

7.mama anaye nyonyesha ana uhitaji mkubwa wa virutubisho kwaajili yake mwenyewe na kutengeneza maziwa kwa ajili ya mtoto, hivyo anapaswa kula Milo mingi kuliko Kawaida ili kukidhi ongezeko la mahitaji kwa ukuaji wa Mtoto.

8.mama mjamzito anapaswa kula Milo mitatu ya vyakula mchanganyiko na Milo miwili ya ziada kila siku ili kuimarisha Hali yake ya lishe na kuimarisha lishe ya mtoto anaye nyonya.

9.mama amnyonyeshe Mtoto Mara tu anapojifungua (Ndani ya saa moja)

10.mama asimpatie Mtoto chakula au kinywaji kingine chochote au maji mpaka atimize miezi sita

11.mama amwanzishie Mtoto vyakula vya nyongeza Mara anapotimiza miezi sita huku akiendelea kunyonya.           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2022/01/11/Tuesday - 12:13:18 am Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 992


Sponsored links
👉1 kitabu cha Simulizi     👉2 Kitau cha Fiqh     👉3 Madrasa kiganjani     👉4 Kitabu cha Afya    

Post zifazofanana:-

Nataka nijue siku ya kubeba mimba mwanamke
Soma Zaidi...

Dalili za kuharibika kwa mimba
Katika post hii utajifunza ishara na dalili ninazoonyesha kuwa mimba ipo hatarini kutoka ama inaweza kuwa imeshatoka. Soma Zaidi...

Sababu za mwanamke kukosa hamu ya kushiriki tendo la ndoa
Posti hii inazungumzia kuhusiana na sababu zinazosababisha kukosa hamu ya kushiriki tendo la ndoa. Soma Zaidi...

Je mwanamke anaweza kujijuwa ni mjamzito baada ya muda gani.
Mdau anauliza ni muda gani mwanamke anaweza kujijuwa kuwa amepata ujauzito. Soma Zaidi...

Sababu za kutoka mimba yenye miezi Saba na nane
Posti hii inahusu zaidi sababu za mtoto kuzaliwa akiwa na miezi Saba na nane kwa kawaida mtoto wa hivi anakuwa hajafikisha mda wake kwa hiyo uzaliwa akiwa na miezi saba na nane, kwa hiyo kuna sababu mbalimbali kama tutakavyoona Soma Zaidi...

Nimemaliza heddhi mwezi huu lkni najihisi tena dalili zakublidi wiki nzima hii kwann?
Soma Zaidi...

Mambo ya kuzingatia kwa Mama mwenye mimba
Posti hii inahusu zaidi mambo ya kuzingatia kwa Mama mwenye mimba, ni kipindi ambacho Mama uhitahi uangalizi wa karibu zaidi. Soma Zaidi...

dalili za uchungu kwa mama mjamzito
Makala hii itakwenda kukufundisha baadhi ya dalili za uchungu kwa mama mjamzito. Soma Zaidi...

Kwa mjamzito kuumia wakati wa tendo la ndoa tatizo linaweza kuwa ni nini?
Soma Zaidi...

SIKU HATARI ZA KUPATA UJAUZITO KWA MWENYE MZUNGURUKO WA SIKU KIDONGO AU NYUNGI
SIKU YA KUPATA UJAUZITO Kawaida wanawake walio wengi mzunguruko wa siku zao ni siku 28 lakini wapo ambao ni zaidi ya hapo na wapo ambao ni chini ya hapo. Soma Zaidi...

Imani potofu kwa mwanamke mwenye mimba
Posti hii inahusu zaidi imani potofu kwa mwanamke mwenye mimba, ni Imani ambazo zimekuwepo kwenye jamii kuhusu wanawake wenye mimba. Soma Zaidi...

Faida za uzazi wa mpango kwa watoto.
Posti hii inahusu zaidi umuhimu wa uzazi wa mpango kwa watoto, sio akina Mama peke yao wanaofaidika na uzazi wa mpango vile vile na watoto wanafaidika na uzazi wa mpango kama ifuatavyo. Soma Zaidi...