Mambo yanayobatilisha funga au yanayoharibu swaumu.

Hapa utajifunza mambo ambayo akiyafanya mtu aliyefunga, basi funga yake itaharibika.

Yanayobatilisha Funga

Mtu aliyefunga analazimika kujizuilia na vitendo mbalimbali ambavyo hubatilisha funga yake. Mfungaji akifanya moja wapo katika yafuatayo swaum yake itabatilika.

 

(i)Kula na Kunywa
Ukila au ukinywa chochote kile kwa kudhamiria hata ikiwa ni dawa utakuwa umefungulia. Vile vile ukivuta sigara au chochote kile au ukivuta dawa ya mafua kwa pua utakuwa umefungua. Pia kupitisha chochote puani au masikioni kwa kudhamiria, hata ikiwa dawa utakuwa umefu n gu a.

 


Ikumbukwe kuwa kujifunguza makusudi katika mwezi wa Ramadhani kwa kula na kunywa bila ya udhuru wowote wa kisharia ni kosa kubwa sana mbele ya Allah(s.w) kwa kiasi ambacho hata kama mtu atafunga umri wake wote hataweza kuilipia hiyo siku moja aliyojifunguza makusudi kama tunavyojifunza katika Hadith ifuatayo:

 


Abu Hurairah(r.a) ameeleza kuwa Mtume (s.a.w) amesema: Yule anayefungua siku moja ya Ramadhani bila kuwa mgonjwa au kuwa na udhuru mwingine wa kisheria, hata akifunga maisha yake yote hataweza kuilipia funga hiyo. (Ahmad, Tirmidh, Abu Daud, Ibn Majah, Darimi).

 


Hadith hii inatuasa tusifanyie mas-khara amri za Allah (s.w). Hivyo mtu akijifunguza makusudi ajue wazi kuwa amefanya kosa kubwa ambalo halitasameheka kwa kuilipia tu siku hiyo bali ni lazima pia arejee kwa Mola wake kwa toba ya kweli.

 


(ii)Kujitapisha Makusudi
Mtu akijitapisha makusudi funga yake itavunjika kutokana na Hadith ifuatayo:
Abu Hurairah(r.a) ameeleza kuwa Mtume wa Allah amesema: Anayeshindwa kuzuia matapishi halipi. Lakini anayejitapisha makusudi, na alipe. (Tirmidh, Abu Daud, Ib Majah).
Kutokana na Hadith hii kutapika kwa ugonjwa hakufunguzi.

 


(iii)Kupatwa na Hedhi au Nifasi
Mwanamke akipatwa na hedhi au nifasi hata kama imempata nyakati za mwisho kabla ya jua kuchwa, atakuwa amefungua na atalazimika kuilipia siku hiyo baada ya Ramadhani.

 


(iv)Kujitoa Manii Makusudi Ukijitoa manii kwa mkono au kwa kubusiana na kukumbatiana mume na mke, au kwa njia nyingine yoyote ile utakuwa umefungua.Kutokwa na manii kwa kuota au kwa njia nyingine isiyokuwa ya makusudi, hakufunguzi.

 


(v) Kunuia Kula na hali umefunga
Ukinuia kula hata kama hukula swaumu yako itakuwa imebatilika kwa kuwa utakuwa umevunja nguzo moja ya funga - nia.

 

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2022/08/16/Tuesday - 06:50:20 pm     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 895

Post zifazofanana:-

Jinsi ya kutekeleza funga za sunnah
Hapa utajifunza muda wa kutia jia katika funga za sunnah. Pia utajifunza kuhusu uhuru ulio nao Soma Zaidi...

Je ni kwa nini lengo la finga halifikiwi kwa wafungaji
Lengo la funga ni kuwa mchamungu sasa ni kwa nini wafungaji hawalifikii lengo hili na kuwa wachamungu. Soma Zaidi...

Nguzo za swaumu (kufinga)
Hapa utajifunza nguzo kuu za swaumu. Kama hazitatimia nguzo hizi basi swaumu itakuwa ni batili. Soma Zaidi...

Zijuwe funga za sunnah na jinsi ya kuzifunga
Post hii inakwenda kukufundisha kuhusu funga za sunnah na jinsi ya kuzigunga. Soma Zaidi...

Mambo ambayo hayafunguzi funga
Hii ni orodha ya mambo ambayo hayawezi kuharimu funga yako endapo utayafanya. Soma Zaidi...

Tarstibu za kulipa swaumu ya Ramadhani
Hapa utajifunza namna ambayo utatakiwa kulipa funga ya Ramadhani kwa siku ambazo hukufunga Soma Zaidi...

Vipi utapata uchamungu kupitia funga
Vipi lengo la funga litafikiwa na kumfanya mfungaji awe mchamungu. Soma Zaidi...

Jinsi ya kukaa itiqaf na taratibu zake
Hapa utajifunza kuhusu taratibu za ibada ya itiqaf yaani kukaa msikitini kwa ajili ya ibada. Soma Zaidi...

Ufafanuzi kuhudu mgogoro wa mwezi ni muda gani mtu aanze kufunga.
Je inapoonekana sehemu moja tufunge duania nzima ama tufunge kwa kuangalia mwandamo katika maenro tunayoishi. Soma Zaidi...

Je kukosa hedhi kwa mwanmke anayenyonyesha ni dalili ya mimba
Kipimo cha mimba cha mkojo hakiwezi kyonyesha mimva changa sana. Hivyo kama ni mimba baada ya wikibpima tena itaweza kuonekana. Dalili hizobulizotaja pekee haziashirii mimba tu huwenda ni homoni zimebadilika kidogo, ama una uti. Soma Zaidi...

Jinsi ya kutoa zakat al fitiri na umuhimu wa zakat al fitri kwa waislamu
Hapa utajifunza kuhusu zakat al fitiri, kiwango chake, watu wanaostahili kupewa na kutoa, pia umuhimu wake katika jamii. Soma Zaidi...

Fadhila za usiku waalylat al qadir
Zijuwe fadhila za usiku wenye cheo kuliko nyusiku ya miezi 1000. Soma Zaidi...