Mambo yanayodhaniwa kuwa yanaharibu funga lakini hayaharibu
Nguzo za uislamu (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu)
- Mambo yanayodhaniwa yanaharibu funga lakini hayaharibu.
- Kula au kunywa bila kukusudia – kwa kusahau au kutwezwa nguvu.
- Kuoga wakati umefunga.
- Kutokwa na manii bila kukusudia – kwa kuota ndoto au namna nyingine.
- Kuamka na Janaba, Damu ya Hedhi au Nifasi ukiwa umefunga.
- Kubusiana na kukumbatiana mume na mke wakiwa wamefunga.
- Kupiga mswaki, kusukutua au kupandisha maji puani.
- Kupaka wanja, manukato, mafuta, kuvukiza ubani au dawa ya macho.
- Kumeza usichoweza kujizuia nacho kama mate, kikohozi, kuingiwa na mdudu (kitu) ghafla hadi kooni, vumbi, n.k.
- Kupiga sindano isiyoongeza chakula mwilini kama itahitajika.
- Kuumika au kutoa damu kwa mujibu wa Hadith;
“Amehadithia Ibn Abbas (r.a) kwamba Mtume (s.a.w) aliumikwa akiwa katika ‘Ihram’ na pia akiwa amefunga.”
(Ameipokea Bukhari)
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
Share follows: 0 |
Unique share links followed: 0
Sponsored links
👉1 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w) 👉2 Madrasa kiganjani 👉3 Tafasiri ya Riyadh Swalihina 👉4 ai web app 👉5 Simulizi za Hadithi Audio 👉6 web hosting
👉1 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w) 👉2 Madrasa kiganjani 👉3 Tafasiri ya Riyadh Swalihina 👉4 ai web app 👉5 Simulizi za Hadithi Audio 👉6 web hosting
Post zinazofanana:
Mali zinazojuzu kutolewa zaka, nisaab yake na viwango vyake
Nguzo za uislamu (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu)
Soma Zaidi...Hukumu ya talaka iliyotolewa kabla ya tendo la ndoa
Endapo mtu atamuacha mke wake kabla hata ya kukutana kimwili, basi talaka hii itahukumiwa kwa namna hii.
Soma Zaidi...