image

Mambo yanayohitajika kabla ya kuanza upasuaji

Posti hii inahusu zaidi mambo yanayohitajika kabla ya kuanza upasuaji ni mambo muhimu ambayo yanapaswa kufanyika kwanza na baadaye upasuaji unaweza kuendelea.

Mambo yanayopaswa kufanyika kabla ya kuanza upasuaji.

1.Kwanza kabisa mazingira yanapaswa kuandaliwa.

Kuhakikisha kuwa chumba kimeandaliwa vizuri na kumfanya mgonjwa ajisikie huru, kuhakikisha kubwa hakuna alama yoyote ya kuwepo kwa maambukizi na kuwepo usalama katika chumba hicho na kuhakikisha kwamba kila mgonjwa anakuwa na utofauti na mwingine katika maandalizi hii inategemea na hali ya mgonjwa na Ugonjwa alio nao.

 

2.Kuandaa vifaa vyote vinavyohitajika wakati wa upasuaji.

Hivi vifaa vinaandaliwa na mhudumu maalumu ambaye amechaguliwa kuandaa vifaa hivyo na kuhakikisha kubwa vifaa vinaandaliwa kadri ya  ugonjwa alionao au kadri ya hali ya mgonjwa kwa hiyo kila hospitali inapaswa kuwa na vifaa vya kutosha ambapo akitoka mgonjwa huyu anaingia mwingine na seti za vifaa vinavyotumika ni tofauti tofauti ili kuweza kuepuka Maambukizi.

 

3. Kumwandaa mgonjwa.

Hii ni hatua ya msingi sana ambapo wahudumu wanapaswa kumwandaa mgonjwa na kumhakikishia kuwa upasuaji utaenda vizuri na kumwambia kwa nini wanafanya upasuaji na kuhakikisha kuwa mgonjwa anasaini fomu maalumu kwa ajili ya kukubali kuwa upasuaji ufanyike na kupima vipimo vyote kama vile mapigo ya moyo, upumuaji, msukumo wa damu na joto la mwili kabla ya kufanyika upasuaji wowote ule.

 

4.Maandalizi ya wahudumu.

Na wahudumu wenyewe wanapaswa kujiandaa kwa kila mtu na kazi yake kuhakikisha kuwa dawa zinazohitajika zimepatiwa kwa mgonjwa , kuhakikisha kuwa fomu imesainiwa na kuandaa mavazi na kujua historia ya mgonjwa kama upasuaji ni wa kwanza au vipi na kuandaa dawa kwa ajili ya kumpatia dawa kadri ya uchaguzi wa mgonjwa au ushauri wa wahudumu.





           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 741


Sponsored links
👉1 kitabu cha Simulizi     👉2 Kitau cha Fiqh     👉3 Kitabu cha Afya     👉4 Madrasa kiganjani    

Post zifazofanana:-

Umuhimu wa kuvaa nguo za upasuaji.
Posti hii inahusu zaidi umuhimu wa nguo za upasuaji, tunajua wazi kuwa, wakati wa upasuaji tunapaswa kusafisha chumba na mazingira yake lengo ni kuhakikisha kuwa tunazuia wadudu wasisambae au kuingia kwenye mwili wa binadamu. Soma Zaidi...

MARADHI YASABABISHWAYO NA HALI ZA MAISHA
Pata elimu juu ya afya hapa ukiwa na vitabu vyetu bila ya malipo yoyote Soma Zaidi...

darasa la lishe
Jifunze mengi kuhusu afya na lishe, ujuwe utaratibu wa lishe Soma Zaidi...

AINA ZA VYAKULA
Pata elimu juu ya afya hapa ukiwa na vitabu vyetu bila ya malipo yoyote Soma Zaidi...

Umoja wa mataifa unazungumziaje afya
Somo Hili linakwenda kukueleza kuhusu Mambo ya kiafya yanayozungumzwa na umoja wa mataifa Soma Zaidi...

AFYA NA MAGONJWA
Pata elimu juu ya afya hapa ukiwa na vitabu vyetu bila ya malipo yoyote Soma Zaidi...

Umuhimu wa kupiga push up kiafya
Posti hii inahusu zaidi umuhimu wa kupiga push up kiafya, ni mambo au faida zipatikanazo ki afya kwa wapigaji wa push up kama ifuatavyo. Soma Zaidi...

madhara ya tezi dume
Endapo tezi dume haitatibiwa ama itachlewa kutibiwa basi mtu anaweza kupata madhara. katika post hii utakwenda kuyajuwa madhara ya tezi dume kwenye Mwili Soma Zaidi...

DARASA LA AFYA NA AFYA YA UZAZI
Jifunze mengi kuhusu Afya, kuwa nasi kwenye makala hii hadi mwisho. Soma Zaidi...

Habari za uzima,nimesoma makala yako tumbo linaniuma upande wa kulia Ila sisikii Sana yenyewe Ila nikibonyeza na mkono ndio inauma yaani ni Kama nimegongwa sehem flani alafu Kuna maumivu lakini ni mpaka upaguse ndio una experience maumivu Kama Kuna namna
Kama unasumbuliwana tumbo upande wa kulia, kushoto, kitomvuni ama kuoande wa kuliavkwachini, basi muulizaji huyu atakupa uelewa. Soma Zaidi...

TAHADHARI KWENYE VYAKULA ILI KULINDA AFYA YAKO
Pata elimu juu ya afya hapa ukiwa na vitabu vyetu bila ya malipo yoyote Soma Zaidi...

YANAYOATHIRI AFYA TABIA
Pata elimu juu ya afya hapa ukiwa na vitabu vyetu bila ya malipo yoyote Soma Zaidi...