Mapendekezo muhimu kwa wajawazito

Posti hii inahusu zaidi mapendekezo muhimu kwa wajawazito, haya ni mapendekezo yaliyotolewa na wataalamu wa afya ili wajawazito waweze kule mimba zao vizuri na kuweza kujifungua vizuri na kupata watoto wenye afya njema na makuzi mazuri pasipokuwepo na ule

Mapendekezo muhimu kwa wajawazito.

1.Kwanza kabisa wajawazito wanapaswa kuwa na mlo kamili na kupata chakula cha kutosha na pia akina mama wanapaswa kula vyakula vyenye wanga , protini, mafuta, mboga za majani, matunda na kunywa maji walau kwa siku glass nane na pia akina mama wajawazito wanapaswa kuachana na vyakula ambavyo havina faida yoyote mwilini kama vile kula pembe, Mawe na vitu vya aina hiyo na pia wanawake wajawazito wanapaswa kuachana na vileo vikali pamoja na uvutaji wa bangi kwa sababu ni hatari kwa afya ya mtoto.

 

2. Pia akina Mama wanapaswa kuangaliwa kila mwezi kwa Upande wa Mama anapaswa kuangaliwa kama anavimba miguu, ana damu ya kutosha,ana malaria au anaumwa ugonjwa wowote kama kina shida kati ya hayo anapaswa kwenda kupata matibabu Mara moja, na kwa upande wa mtoto aliyeko tumboni anapaswa kuangaliwa jinsi alivyolala tumboni,kama anapumua , kupima kimo cha mtoto na kutabiri tarehe na siku ambayo mtoto atazaliwa kwa kufanya hivyo kila mwezi kwa asilimia tisini na tano mtoto atazaliwa salama.

 

3.Kuzuia magonjwa nyemelezi kwa Mama na mtoto.

Kwa kuzuia magonjwa nyemelezi kama vile Malaria, kupungua kwa damu mwilini, kupima maambukizi ya virus vya ukimwi ni pendekezo la Muhimu sana ambalo homkinga mtoto na maradhi mbalimbali, kwa hiyo ili kupambana na magonjwa hayo kila baada ya mwezi Mama utumia vidonge vya sp, vidonge vya follic asidi kwa ajili ya kuongeza damu,kutumia dawa za minyoo pale anapoanza mahudhurio na pia Mama hupewa neti bure anapoanza mahudhurio kwa kufanya hivyo tunaweza kupambana na magonjwa nyemelezi kwa Mama na mtoto.

 

4.Uangalizi wa Mama baada ya kujifungua na uangalizi mkubwa pale ambapo mimba inaonekana kubwa na vikwazo vingi, katika kipindi hiki Mama ambaye ana matatizo wakati wa kujifungua anapaswa kuja hospitalini mapema anapofikisha miezi ile inayofikiliwa kubwa huwa anapata matatizo, mama huwa kwenye uangalizi wa manes na wataalamu wa afya walio na ujuzi ili likitokea jambo lolote awe tayari kupambana nalo na kumfanya Mama akifungua salama.



Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2022/02/08/Tuesday - 08:49:17 am     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 783


Download our Apps
👉1 Kitau cha Fiqh     👉2 Kitabu cha Afya     👉3 kitabu cha Simulizi     👉4 Madrasa kiganjani    

Post zifazofanana:-

Kazi ya metronidazole
Posti hii zaidi kazi ya Dawa ya metronidazole katika kutibu Minyoo, ni aina ya Dawa ambayo imetumiwa na watu wengi wakaweza kupona na kuepukana na minyoo. Zifuatazo ni baadhi ya kazi za metronidazole. Soma Zaidi...

Maandalizi ya mama mjamzito kwa ajili ya kujifungulia.
Postii inafundisha maandalizi ya mama kwa ajili ya kujifungulia hii Ni muhimu Sana kwa wale ambao hawajawahi kujingua Ni mara yao ya kwanza wanatakiwa kujua na kuelewa vifaa na mahitaji kujifungulia na kwa wale wanaohudhuria clinic huwa wanafundisha. Soma Zaidi...

Fahamu Mambo ya hatari yanayosababisha kuzaliwa kabla ya wakati (premature)
Kuzaliwa kabla ya wakati humpa mtoto muda mdogo wa kukua tumboni. Watoto waliozaliwa kabla ya wakati, hasa wale waliozaliwa mapema, mara nyingi huwa na matatizo magumu ya matibabu. Soma Zaidi...

Vipimo muhimu wakati wa ujauzito
Post hii inahusu zaidi vipimo muhimu wakati wa ujauzito ni vipimo ambavyo vinapaswa kupimwa na Mama ili kuangalia mambo mbalimbali katika damu au sehemu yoyote, pia vipimo hivi umsaidia sana Mama kujua afya yake. Soma Zaidi...

Mambo yanayopelekea ugumba.
Post huu inahusu zaidi mambo yanayopelekea ugumba kwa wanaume, ni mambo ambayo uchangia au upelekea mwanaume kukosa uzazi. Soma Zaidi...

Sababu za kuongezeka uzito wa wajawazito.
Posti hii inahusu zaidi sababu za kuongezeka uzito kwa wajawazito, Mara nyingi Mama akibeba mimba uongezeka uzito kutoka wiki ya Kwanza mpaka wiki ya mwisho ya kujifungua. Soma Zaidi...

Siku za kupata mimba
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu siku za kupata mimba Soma Zaidi...

Mabadiliko ya mzunguko wa damu kwa wajawazito.
Posti hii inahusu zaidi mabadiliko ya mzunguko wa damu kwa wajawazito, tunajua wazi kuwa wajawazito pindi ujauzito ukiingia tu, kila kitu kwenye mwili ubadilika vile vile na mzunguko wa damu ubadilika. Soma Zaidi...

Kondomu za kike
Posti hii inaonyesha Faida na hasara za Kondomu za kike Soma Zaidi...

Faida na hasara za Kufunga kizazi kwa Wanaume
Posti hii inazungumzia Faida, hasara, na madhara ya Kufunga kizazi kwa Wanaume. Soma Zaidi...

Mapendekezo muhimu kwa wajawazito
Posti hii inahusu zaidi mapendekezo muhimu kwa wajawazito, haya ni mapendekezo yaliyotolewa na wataalamu wa afya ili wajawazito waweze kule mimba zao vizuri na kuweza kujifungua vizuri na kupata watoto wenye afya njema na makuzi mazuri pasipokuwepo na ule Soma Zaidi...

Je, mwanamke anapataje Ugonjwa wa Maambukizi ya mfumo wa Uzazi PID?
Posti hii inaelezea namna mwanamke anavyoweza kupata Ugonjwa wa Maambukizi ya mfumo wa Uzazi. Soma Zaidi...