picha

Maradhi ya macho

Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu maradhi ya macho,dalili na matibabu yake

MARADHI YA MACHO

Matatizo ya macho yapo mengi katika jamii, lakini mara nyingi matatizo ya macho yanatibika iwapo mgonjwa ataonana na daktari mara atakapoona dalili. Miongoni mwa matatizo ya macho ni kupoteza uwezo wa kuona.

 

1.Kutoona karibu (long sightedness)Tatizo hili mara nyingi huwatokea watu wenye umri wa miaka 40 na kuendelea.

 

DaliliA.Katika mazingira ya kawaida anaona sawa sawaB.Kushindwa kusoma herufi ndogo ndogoC.Kushindwa kufanya kazi za sehemu ndogo ndogo mfano kutunga sindano.

 

Matibabu: Kutumia miwani ya kusomea.

2.Kutoona Mbali (short sightedness)A.Hayana umri maalumB.Myopia – haoni mbali vizuriC.Hyperopia – haoni mbali na kichwa kinauma akikosa kuvaa miwani yenye namba ndogo kusaidia lense.

 

NB: Mgonjwa anasoma karibu bila miwaniMatibabu: Kutumia miwani ya kuonea mbali

 

3.Mtoto wa Jicho (cataract)DaliliA.Kidoto cheupe katikati ya kioo cheusi cha jicho (kinafunika mboni ya jicho)B.Kidoto cheupe kisichobadilika kwa mwangazaC.Kupunguza nuru ya macho

 

NB - Mtu anaweza kuzaliwa nacho au kupata ukubwani, inaweza kuwa kwenye jicho moja au yote. Mgonjwa huona mchanganyiko wa rangi anapoangalia mwangaza kama taa za umeme au gari.

 

MatibabuMtoto wa Jicho huwa anatibika kwa upasuaji mdogo na kumuwezesha mgonjwa kuona tena.

 

4.Presha ya macho (glaucoma)Tatizo hili husababishwa na kuongezeka presha ya jicho (intraocular pressure) kutokana na kukosekana uwiano wa mzunguko wa majimaji ndani ya jicho (aqueous fluid) kinachotoka kidogo kuliko kinachoingia.

 

MatokeoGlaucoma hukandamiza na kuuharibu mshipa wa fahamu ya jicho na kusababisha kupungua kwa nuru na baadae kupoteza nuru ya macho.

 

Matibabu: Kuonana na daktari kwa ushauri na dawa

 

5.Macho tongoHutokea ama kwa mtu mmoja mmoja, makundi au kwa msimu.

 

Sababu:Vimelea ambavyo huzaliwa kwenye sehemu za uchafu Wakati wa msimu huambukiza kwa kukosa elimu ya afya, kwa mfano kutokuosha mikono baada ya kuamkiana na mgonjwa mwenye maradhi haya au kutumia vifaa vya macho kwa zaidi ya mtu mmoja kama vile miwani.

 

DaliliA.Kuhisi kama kuna mchanga ndani ya jichoB.Kuvimba mifuniko ya macho bila kupoteza nuru.C.Macho kuwa mekundu sana (conjuctivitis)D.Kutoka tongo kila mara

 

MatibabuMgonjwa atumie dawa alizoandikiwa na daktari tu, kwani dawa za matone za macho ni nyingi na zina kazi tofauti.

 

6.Matatizo ya sehemu nyeusi ya jicho (cornea)Kuna matatizo manne makubwa1. Kovu - kidoto/kibaka cheupe2. Kidonda - kidoto kijivujivu3. Kuingiwa na kitu - kemikali,mdudu, vumbi n.k4. Kutoboka na kutoa maji.Indhari: hali ya pili mpaka ya nne zikitokea mgonjwa akimbizwehospital wakati jicho limefunikwa baada ya huduma ya kwanza

 

DaliliKOVU1.Haina maumivu2.Jicho haliwi jekundu3.Jicho halivimbi4.kupungua nuru jicho

 

KIDONDAA.Kinayo maumivuB.Jicho lililoathirika huwaC.jekunduD.Jicho kupunguka nuruE.Kuuma jicho kwenyeF.mwangazaG.Kutoka machoziH.Jicho kuvimba

 

Kidonda kinaweza kusababishwa na bakteria, fangas, ukosefu wa vitamin A au kwa kuumia mfano; kujichoma na kitu chenye ncha au kitu kigumu, kuingiwa na kitu jichoni, kuungua au kuingia kemikali jichon.

 

Indhari: Iwapo jicho litaumia lifunike jicho lisipate mwangaza kisha mpeleke mgonjwa hospitali.

 

7. Kemikali na kuunguaKama mgonjwa ameingia kemikali kama vile acid, alkali, saruji, chokaa mtie maji ya mchuruziko kwa takriban dakika 15 mfululizo na baadae mpeleke hospitali

 

8.Macho kuwasha na kutokwa na machozi (conjuctivitis)Huwakumba zaidi watoto wa umri kati ya miaka 5 -15 ambao hupendelea kucheza sehemu za vumbi au kwenye muangaza mkali (pwani yenye mchanga mweupe sana)

 

Watu wazima wenye kufanya kazi kwenye viwanda vinavozalisha vumbi, na wenye pumu ya muda mrefu.

 

DaliliA.Macho kuwasha (Nuru ya macho haipungui)B.Macho kubadilika rangi (kahawia)C.Kutokwa na machozi mengi (sana)D.Kushindwa kuangalia kwenye muangaza mkali

 

MatibabuKusafisha macho mara kwa mara kwa maji safi.Kutumia dawa kwa maelekezo ya daktari

 

9.Kinundu katika mfuniko wa juu au chini wa jicho

 

DALILIA.Kinundu kisichoumaB.Mara nyingi hupona wenyewe au unaweza kukikanda kwa maji ya uvuguvugu.C.Kisipopona au kitakapokuwa kikubwa huhitaji upasuaji mdogo.

 

10.Uvimbe katika mfuniko wa jicho (cellulitis)

 

A.uvimbe kwenye mifuniko ya jichoB.inaweza kuzuwia jicho kucheza (kutembea tembea)C.mara nyingi hutokea baada ya kusambaa kwa maambukizoD.ya socket ya jicho kutoka pembezoni kwa saines (sinusitis) za puaE.husababisha kupoteza nuru za macho

 

Matibabu: Mpeleke mgonjwa kwa daktari wa masikio, pua na koo (ENT)

Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

       
Author: Rajabu image Tarehe: 2024-05-10 14:53:23 Topic: magonjwa Main: Post File: Download PDF Views 3793

Share On:

Share follows: 0 | Unique share links followed: 0
Sponsored links
πŸ‘‰1 ai web app     πŸ‘‰2 Tafasiri ya Riyadh Swalihina     πŸ‘‰3 Bongolite - Game zone - Play free game     πŸ‘‰4 Kitabu cha Afya     πŸ‘‰5 Kitau cha Fiqh     πŸ‘‰6 web hosting    

Post zinazofanana:

Polio (Kilema cha utotoni): Dalili na umuhimu wa chanjo.

Ugonjwa wa Polio, unaojulikana kitaalamu kama Poliomyelitis, ni ugonjwa hatari wa kuambukiza unaosababishwa na virusi vya Polio (Poliovirus). Ugonjwa huu huathiri mfumo wa neva na unaweza kusababisha ulemavu wa kudumu au kifo ndani ya saa chache. Licha ya juhudi kubwa za kimataifa kutokomeza ugonjwa huu, bado ni tishio katika maeneo machache duniani. Makala hii inachunguza kwa kina biolojia ya ugonjwa, dalili zake, athari za muda mrefu, na umuhimu wa chanjo kama nyenzo pekee ya kuzuia maambukizi.

Soma Zaidi...
Dalili za mimba wakati wa ovulation

​Kipindi cha baada ya yai kuachiliwa (ovulation) hadi kufikia tarehe ya hedhi inayofuata hujulikana kama Luteal Phase. Hapa ndipo wanawake wengi wanaotafuta ujauzito huanza kuchunguza mabadiliko ya miili yao. Makala haya yanajadili dalili za mapema za mimba zinazoweza kujitokeza siku chache baada ya ufertilishaji, jinsi ya kutofautisha dalili hizi na zile za hedhi ya kawaida (PMS), na ukweli wa kitaalamu kuhusu lini unapaswa kupima mimba.

Soma Zaidi...
Dalili za mtu aliyegongwa na nyoka

Post hii inahusu zaidi dalili za mtu aliyegongwa na nyoka, nyoka ni kiumbe ambacho Kina sumu kali na sumu ikiingia mwilini mtu huwa na dalili mbalimbali

Soma Zaidi...
Vipimo vya VVU

Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu vipimo mbalimbali vinavyotumika kupima VVU

Soma Zaidi...
Je utaweza kuambukiza HIV ukiwa unatumia PrEP?

Swali hili limeulizwa na mdau mmoja. Kuwa endapo mtu atafanya ngono zembe na akapata virusi je ataweza kuambukiza.

Soma Zaidi...
Njia za kupambana na fangasi

Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu njia za kupambana na fangasi

Soma Zaidi...