SABABU YA NENO LAKO

Sababu ya neno lako, nasema nimesikia, Sababu ya neno lako, nasema hongera pia, Sababu ya neno lako, nishajua yakonia, Wasema afukuzwae, sihadi pasemwe toka, Sababu ya neno lako, maumivu yanijia, Sababu ya neno lako, nami leo nakwambia, Sababu ya neno lako, sitoweza kurudia, Ndege unae muinga, hujua pakukimbia, Sababu ya neno lako, sisiri nimeumia, Sababu ya neno lako, mengi sasa najutia, Sababu ya neno lako, najibadili tabia, Pilau bila viungo, pishi halijatimia, Sababu ya neno lako, sitoweza kukawia, Sababu ya neno lako, sasa nabadili nia, Sababu ya neno lako, nimesha kushitukia, Muwinda simba kwafimbo, maisha kayachukia, Sababu ya neno lako, nilitamani kulia, Sababu ya neno lako, sikuweza vumilia, Sababu ya neno lako, shairi nakutungia, Tamu ya ndimu sikula, hunoga haswa supuni, Sababu ya neno lako, jibu nimejipatia, Sababu ya neno lako, siwezi kun'gan'gania, Sababu ya neno lako, kwengine nita hamia, Baharia simkwezi, namkwezi sikwa mbizi, Sababu ya neno lako, ngazi nishaiachia, Sababu ya neno lako, waje wengine kungia, Sababu ya neno lako, haya nimedhamiria, Sitojali mambo yako, chochote sito kwambia. (inakuhusu) by HD.Hassan