SIOKOSA

Siokosa kwa mpenzi, kusoma tabia zako, Siokosa tangu enzi, nahayo yalikuweko, Siokosa saahizi, wala sionwe kituko, Siokosa nihalali, muache ajiridhishe, Siokosa kwa mkeo, kulijua chumo lako, Siokosa juwa leo, muambie namwenzako, Siokosa ndio cheo, anahaki hio kwako, Siokosa nihalali, muache ajiridhishe, Siokosa kwamchumba, kupima uwezo wako, Siokosa siushamba, vitabuni pia liko, Siokosa wala pumba, kuleta maswali kwako, Siokosa nihalali, muache ajiridhishe, Siokosa hilipia, kucheza na mkewako, Sikosa kukufanyia, japo madeko madeko, Sikosa akikwambia, apande mgongo wako, Siokosa nihalali, muache ajiridhishe, by.HD.Hassan