Masharti ya kukubaliwa kwa dua
Post hii itakwenda kukugundisha masharti yanayofungamana na kukubaliwa kwa dua.
MASHART YA KUKUBALIWA KWA DUA.
1.kuchunga adabu za dua kama zilivyotajwa hapo juu.
2.Kuwa twahara nje na ndani. Yaani kujiepusha na mambo maovu na machafu ya siri na yasiyo ya siri. Amesema Mtume صلّي الله عليه وسلّم “hakika Allah ni mzuri na anapenda (vitu) vizuri.…”. (amepekea Bukhari na Muslim) Hivyo mtu anatakiwa ahakikishe ni mzuri ndani na nje.
3.kujiweka mbali na yaliyo haramu yote, na kujiepusha kula na kunywa bya haramu au kuvaa vilivyo haramu. Amesema Mtume صلّي الله عليه وسلّم “ukitaka dua maombi yako basi kifanye kizuri chakula chako (kisiwe cha haramu) “ (amepekea Bukhari na Muslim). Na pia katika hadithi ndefu iliyo sahihi katika kuwa mtume anashangaa mtu ambaye chakula chake haramu, kinywaji chake haramu, a mavazi yake haramu. Isitoshe mtu huyu amechafuka na manywele yapo timtim. Vipi atajibiwa dua yake mtu huyu. (amepekea Bukhari na Muslim). 4.Kuzingatia nyakati ambazo dua hujibiwa. Tutaziona hapo mbele.
5.Sifa ya dua yenyewe. Tutaona dua zenye sifa ya kujibiwa.
6.Hali inayozunguruka dua. Tutaona hali ambazo dua hujibiwa
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
👉1 Bongolite - Game zone - Play free game 👉2 Simulizi za Hadithi Audio 👉3 web hosting 👉4 Tafasiri ya Riyadh Swalihina 👉5 ai web app 👉6 Kitabu cha Afya
Post zinazofanana:
Dua za kumuomba Allah wakati wa shida na tabu ama matatizo
Post hii inakwenda kukufundisha dua ambazo ni muhimu kuzisoma wakayi wa shida na taabu.
Soma Zaidi...Dua ambazo hutumiwa katika swala
Post hii inakwenda kukugundisha dua ambazo itazitumia katika swala yako.
Soma Zaidi...Maswali juu ya Sunnah na hadithi
Sunnah na hadithi (EDK form 3: dhana ya elimu ya uislamu)
Soma Zaidi...dua ya kuomba jambo ufanikiwe
hii ni damna ya kuomba dua ukubaliwe, dua ya kuomba jambo ufanikiwe
Soma Zaidi...