Maswali juu ya Nguzo za uislamu

Maswali juu ya Nguzo za uislamu

Nguzo za uislamu (EDK form 3: dhana ya elimu ya uislamu)

Zoezi la 4.

(a)  Ni upi mtazamo wa Uislamu juu ya maada ya ibada?

(b)  Ni lipi malengo ya ibada maalumu?

(a)  Swala katika Uislamu ina umuhimu gani?

(b)  Kwa ushahidi wa aya ainisha lengo kuu la swala.

(c)  Bainisha jinsi lengo la swala linavofikiwa kwa mwenye kuswali.

(a)  Dhihirisha matunda ya kusimamisha ibada ya swala kikamilifu.

(b)  Tofautisha baina ya kuswali na kusiamamisha swala.

Kwa hakika swala ikiswaliwa vilivyo humuepusha mwenye kuswali na mambo machafu na maovu (29:45).

Toa sababu tano ni kwa nini waislamu pamoja na kuswali kwao mara tano kwa siku hawajapata matunda ya swala zao?

 

(a)  Eleza maana ya zakat kilugha na kisheria.

(b)  Bainisha nafasi ya Zakat katika Uislamu.

(c)  Fafanua lengo la Zakat na jinsi linavyofikiwa.

Pamoja na waislamu wachache kutoa Zakat, lakini matunda yake hayaonekani katika jamii.  

Bainisha sababu zinazopelekea kukosekana matunda ya Zakat ndani ya jamii.

(a)  Eleza maana ya swaumu kilugha na kisheria.

(b)  Ni upi umuhimu na nafasi ya funga kwa muislamu?

Kwa ushahidi wa aya, bainisha lengo la funga na onesha jinsi linavyofikiwa na mfungaji.

(a)  Onesha zinazopatikana kutokana na funga ya mwezi wa Ramadha.

(b) Mmefaradhishiwa kufunga kama walivyofaradhishiwa wale waliokuwa kabla yenu (2:183).

Toa sababu zinazoonyesha funga ya mwezi wa Ramadhan kufaradhishwa katika mwezi huo.

 

Wengi wafungao mwezi wa Ramadhan hawafikii malengo ya fungo zao. Unafikiri ni kwa nini?

 

(a)  Ni ipi maana ya Hijja kilugha na kisheria.

(b)  Hijja ni ibada ya muda maalumu. Fafanua miezi ya Hijjah na tarehe ambayo ibada za Hijja huanza rasmi huko Makkah.

 

Toa mafunzo yatokanayo na vitendo vya ibada ya Hijjah vifuatavyo:

  (i)  Tawafu   (ii)  Sai  (iii)  Kisimamo cha Arafa  (iv)  Kupiga kambi Mina 

  (v)  Kutupa mawe  (vi)  Kuchinja mnyama.

 

(a) Ni lipi lengo kuu la ibada ya Hijjah au Umrah?

(b) Bainisha sababu tano, pamoja na waislamu kukusanyika mamilioni kila mwaka katika mji wa Makkah kwa ajili ya Hijjah, bado matunda yake hayaonekani katika jamii.

Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

       
Author: Rajabu Rajabu
Tarehe: 2024-05-10 14:53:23 Topic: Fiqh Main: Post File: Download PDF Views: 3397

Share On:

Share follows: 0 | Unique share links followed: 0
Sponsored links
👉1 Kitau cha Fiqh     👉2 Bongolite - Game zone - Play free game     👉3 ai web app     👉4 kitabu cha Simulizi     👉5 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)     👉6 Madrasa kiganjani    

Post zinazofanana:

Uislamu unavyokemea tabia ya ombaomba

Uislamu umekataza tabia ya kuombaomba kama ndio njia ya kuendesha maisha. Pia ukaweka suluhisho la kukomesha tabia hiyo

Soma Zaidi...
Mambo muhimu ya kuzingatia katika kujenga uchumi wa kiislamu

Nazingatio muhimu katika uchumi unaofuata sheria za kiislamu.

Soma Zaidi...
Jukumu la serikali katika kuzuia dhuluma

Serikali ina nafasi kubwa katika kuzuia dhulma na kufanya uchumibuwe huru kuyokana na dhulma.

Soma Zaidi...
Dua ya kuzuru makaburi, na utaratibu wa kuzuru makaburi

Kuzuru makaburi ni katika matendo ya sunah yaani unapata thawabu kwa kwenda klizuru kaburi.

Soma Zaidi...