Maswali kuhusu hali ya bara arabu zama za jahiliyyah
Bara arabu zama za jahiliyyah (EDK form 2 dhana ya elimu ya uislamu)
Zoezi la 7.
- (a) Nini maana ya ‘zama za Jahiliyyah’?
(b) Bainisha baadhi ya mambo aliyoyakuta Mtume (s.a.w) katika jamii ya waarabu wa Makkah zama za Jahiliyyah.
- Mji wa Makkah ni mji mkongwe na mtukufu tangu zama za Nabii Ibrahim (a.s). Thibitisha kauli hii kwa kutoa sababu ya utukufu wa mji wa Makkah.
- (a) Bainisha sababu zilizopelekea Muhammad (s.a.w) alipokuwa mdogo kwenda kulelewa nje ya mji wa Makkah.
- Taja baadhi ya sifa au tabia za Mtume (s.a.w) alizokuwa nazo tangu utotoni zilizokuwa kama ishara ya kuandaliwa kuwa Mtume wa Allah.
- (a) Bainisha maandalizi ya Mtume (s.a.w) kabla ya kupewa Utume (mafunzo ya Ki-Ilhamu).
(b) Ni yapi mafunzo yatokanayo na Maandalizi ya Mtume (s.a.w) ya Ki-Ilhamu?
- Mtume (s.a.w) alianza kupewa mafunzo ya Ki-wahyi mara tu baada ya kuanza kumshukia sura tatu za mwanzo, (96:1-5), (73:1-10) na (74:1-7).
Kutokana na aya hizi ainisha mafunzo yatokanayo.
- (a) Ni sababu zipi za msingi ziliwafanya Maquraish wa Makkah kuupinga Ujumbe wa Qur’an?
- Ainisha njia na mbinu walizotumia Maquraish katika kuupinga na kuuzuia ujumbe wa Uislamu kuenea katika jamii na mafunzo yatokanayo.
- Changanua njia alizotumia Mtume (s.a.w) katika kuandaa ummah wa Kiislamu Makkah kwa kutumia mikataba ya ‘Aqabah.
- Katika kuendesha harakati za kuusimamisha Uislamu, hatuna budi kuwa na mikakati madhubuti. Kwa kurejea historia ya Mtume (s.a.w) onyesha jinsi alivyotumia stretejia madhubuti wakati wa kuhama kwenda Madinah.
- ‘Hijra katika Uislamu si sawa na Ukimbizi, bali na stretejia za kuunganisha nguvu ya kuusimamisha Uislamu’.
Kwa kutumia Hijra ya Mtume (s.a.w), mambo gani waislamu wa leo tunajifunza katika hatua za kuupigania Uislamu.
**********************************************
Wabillah Tawfiiq
**********************************
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
π1 Kitabu cha Afya π2 Kitau cha Fiqh π3 ai web app π4 Madrasa kiganjani π5 Dua za Mitume na Manabii π6 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)
Post zinazofanana:
Nani alikuwa ni Sahaba wa kwanza kufariki akiwa Shahidi
Sahaba wa kwanz akufariki akiwa shahidi, alifariki kwa sababu ya mateso aliyoyapata kutoka kwa Makafiri wa ki Quraysh
Soma Zaidi...Kuendeshwa kwa dola ya kiislamu, Uchumi, ulinzi, haki na sheria, siasa na vikao vya shura
Uendeshaji wa Dola ya Kiislamu Madinah.
Soma Zaidi...Kuanzishwa kwa dola ya kiislamu madinah
Dola ya kiislamu madinah (EDK form 3: dhana ya elimu ya uislamu)
Soma Zaidi...Watu waliovunja amri ya kuheshimu siku ya Jumamosi.
Katika zama za kale Mayahudi walikatazwa kufanya kazi siku ya Jumamosi.
Soma Zaidi...Kujengwa upya al Kabah baada ya kuwa na mipasuko.
Sira na historia ya Mtume Muhammad s.a.w sehemu ya 18. Hapa utajifunza kuhusu tukio la kujengwa upya kwa al kaaba Γ°ΕΈβ’βΉ
Soma Zaidi...