Matamshi ambayo ukimwambia Allah kwenye dua yako basi hujibiwa kwa haraka dua hiyo

Post hii inakwenda kukufundisha matamshi ambayo mtu akiyatamka Allah hujibu dua hiyo kwa urahisi.


SIFA ZA (MANENO NA MATAMSHI YA) DUA YENYE KUJIBIWA.
Hapa tutaona dua iliyo katika sura ambayo Allah ataijibu. Dua zenye kujibia wakati mwingine zina sura yake na sifa zake katika maneno na matamshi. Hebu tuone sifa hizo.

1.Dua ya nabii Yunusi. Mwenye kuomba dua na akatumia maneno aliyoyasema nabii Yunusi (amani ishuke juu yake) dua hii ni yenye kujibiwa. Amesema mtume ' ' ' ' “dua ya nabii Yunus pindi alipokuwa kwenye tumbo la samaki (aliseme) ‘LAA LILAAHA ILLAA ANTA, SUBHAANAKA INII KUNTU MINADHWALIMIINA’ hakika hataomba mtu muislamu dua kwa kutumia maneno haya kitu chochote isipokuwa atajibiwa na Allah”. (amepokea tirmidh).

2.Kuomba dua kwa kutumia jina la Allah lililo kubwa. Allah ana majina mengi na mazuri. Lakini katika majina hayo lipo ambalo ni kubwa na ukiomba dua kwalo lakina utajibiwa. Kwa ufupi ni kuwa jina hili limefichwa na hakina yeyote anayelijuwa. Ila mtume ametowa ishara ya kuonesha wapi linapatikana na maneno gani mtu atumie kulipata jina hilo.

Amesema mtume ' ' ' ' “jina kubwa la Allah lipo kwenye aya sita za mwisho za surat hashri. (amepokea Dilamy kutoka kwa Ibn ‘Abas). Pia katika mapokezi mengine ya Tabrany kutoka kwa Ibn ‘Abas kuwa mtume amesema jina kubwa lipo kwenye aya ya 20 ya surat al-imran. Na pia zipo hadithi nyingi sana zinazoashiri wapi jina hilo lipo. Nitaleta chache tuu.

i) Aisha ' ' aliomba dua hii “ ALLAHUMMA INII AD’UKA LLAHA WA-AD’UKAR-RAHMANA, WA-AD’UKAL-BARRAR-RAHIIMA, WA-AD’UKA BIASMAAIKAL-HUSNAA KULLIHAA MAA ‘ALIMTU WAMAA LAM A’ALAM AN TAGHFIRA LII WATARHAMNII” Mtume akacheka kisha akasema “hakika jina kubwa lipo ndani ya dua hii. (amepokea Ibn Maajah kutoka kwa ‘Aisha) hadithi hii ni ndefu nimeikatisha na kuchukua hiyo dyua tu.

ii)hadithi ya Anas' 'kuwa” ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ‏.‏ ' ' ' ' ' ' ‏ "‏ ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ‏"amesimulia Anas ' ' kuwa alikuwa amekaa na mtume ' ' ' ' wamekaa msikitini na kulikuwa na mtu mmoja anaswali kisha akaomba dua kwa kusema “ ALLAHUMMA ANNII AS-ALUKA BIANNALAKAL-HAMDA, LAA ILAAHA ILLA ANTAL-MANNAANU BADI’US-SAMAAWATI WAL-ARDH YAA DHALJALALI WAL-IKRAM YAA HAYYU YAA QAYYUUM” akasema Mtume ' ' ' ' umemuomba Allah kwa jina lake kubwa ambalo anapoombwa kwalo atajibu”. (amepokea tirmidh kwa isnad gharib).

iii)amesimulia Abdillah Ibn Buraydah ' ' kutoka kwa baba yake kuwa Mtume ' ' ' ' alimsikia mtu mmoja akisema “ALLAHUMMA INNIASALUKA BIAN-ASHHADU ANNAKA ANTALLAHU LAA ILAAHA ILLA ANTA. AL-AHADUS-SWAMADUL-LADHII LAMYALID WALAM YUULAD, WALAM YAKUN LAHU KUFWAN AHAD” akasema Mtume ' ' ' ' hakika umemuomba Allah kwa jina lake kubwa ambalo akiombwa hutoa na akiombwa dua hujibu. (amesimulia Abuu Daud,tirmidh,Ibn Maajah na Ibn Hiban).

Iv). Mtume amesema ' ' ' ' ' ' ‏{' ' ' ' ' ' ' ' '}‏ ' ' ' ' ‏"‏Jina kubwa la Allah linapatikana kwenye aya hizi‘ waillahukum ilahu wahidu laa ilaaha illa huwar-rahmanir-rahiim’ na mwanzoni mwa surat al ‘Imran

3.dua ya Mtume ' ' ' ' ni yenye kujibiwa. "‏ ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ‏"‏ Katika hadithisahihi mtume amesema Nabii yeyote ameomba dua yake na akajibiwa. Na nikaifanya dua yangu mimi ni shifaa kwa umati wangu sikku ya qiama. (amepokea Bukhari, Muslim na tirmidh kutoka kwa Anas).

4.Dua wakati wa raha hujibiwa wakati wa shida. Hii ni sifa ya dua yenye kujibiwa mbayo watu wengi hatujui. Nikuwa pindi unapopata neema na raha hapo ndipo pa kumuomba Allah na Allah atakujibu wakati unapopata matatizo kwa kukufariji na kukuondlea matatizo. Amesimulia Abuuhurairah ' ' kuwa mtume ' ' ' ' amesema "‏ ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ‏" ‏ “mwenye kutaka kujibiwa dua yake wakati akiwa na shida basi azidishe kumuomba Allah wakati wa raha”. (amepokea Tirmidh kwa isnad gharib).

Na katika mapokezi mengine amesema Mtume ' ' ' ' "‏ ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ‏" “Mwenye kupenda kujibiwa dua zake wakati wa shida na taabu basi na azidishe dua wakati wa raha” (amepokea tirmidh)


 



Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2022/08/12/Friday - 06:10:56 pm     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 1682


Download our Apps
👉1 Kitau cha Fiqh     👉2 kitabu cha Simulizi     👉3 Kitabu cha Afya     👉4 Madrasa kiganjani    

Post zifazofanana:-

Adhkari unazoweza kuomba kila siku
Hapa nitakuletea baadhi tu ya adhkari ambazo ni muhimu kwa muislamu Soma Zaidi...

Matamshi ambayo ukimwambia Allah kwenye dua yako basi hujibiwa kwa haraka dua hiyo
Post hii inakwenda kukufundisha matamshi ambayo mtu akiyatamka Allah hujibu dua hiyo kwa urahisi. Soma Zaidi...

Dua ambazo hutumiwa katika swala
Post hii inakwenda kukugundisha dua ambazo itazitumia katika swala yako. Soma Zaidi...

Hukumu ya kukusanyika kwenye dua na umuhimu wa dua ya watu wengi
Post hii inakwenda kukufundisha kuhusu umuhimu wa kukusanyika katika kuomba dua. Soma Zaidi...

Dua za kuondoa wasiwasi, woga na kujikinga na uchawi, na mashetani
Post hii itakufundisha dua za kuomba wakati wa woga, wasiwasi na kujikinga na wachawi na mashetani Soma Zaidi...

Masharti ya kukubaliwa kwa dua
Post hii itakwenda kukugundisha masharti yanayofungamana na kukubaliwa kwa dua. Soma Zaidi...

Utofauti wa dua ya kafiri na dua ya muislamu katika kujibiwa
Posti hii inakwenda kukufundisha ni kwa nini dua ya kafiri inawwza kujibiwa wakati ya muumini haijibiwi. Soma Zaidi...

Dua za kumuomba Allah wakati wa shida na tabu ama matatizo
Post hii inakwenda kukufundisha dua ambazo ni muhimu kuzisoma wakayi wa shida na taabu. Soma Zaidi...

Namna ambazo Allah hujibu dua ya mwenye kuomba.
Post hii inakwenda kukufundisha namna ama staili ambazo Allah hujibu dua za watu. Soma Zaidi...

Dua 10 ambazo ni muhimu kuziomba kwa kila siku.
Posti hii inakwenda kukupa orodha ya dua 10 ambazo unaweza kuziomba kila siku. Soma Zaidi...

Zijuwe nyakati ambazo ukiomba dua hujibiwa kwa urahisi
Post hii inakwenda kukugundisha ni nyakati zipi ambazo Allah hukubali dua kwa urahisi. Soma Zaidi...

Halo ambazo akiwa nazo mwenye kuomba dua dua yake hujibiwa
Post hii inakwenda kukifundisha nibhali zipi ukiwa nazo, basi dua yako kuhubaliwa kwa urahisi. Soma Zaidi...