image

Matibabu ya vidonda vya tumbo

Makala hii inakwenda kukufundisha kuhusu matibabu ya vidonda vyatumbo. Pia utajifunza kwa nini kunakuwa na vidonda vya tumbo sugu.

MATIBABU NA DAWA Z VIDONDA VYA TUMBO:

 

Nini vidonda vya tumbo, na zipi aina zake

Vidonda vya tumbo kitaalamu hufahamika kama ulcers, ni vidonda vinavyotokea kwenye tumbo. Vidonda hivi vimepewa majina mbalimbalu kulingana na aina zake. Vipo ambavyo huitwa gastric ulcers ambavyo ni vile avinavyotokea kwenye tumbo la chakula. Aina nyingine huitwa esophangeal ulcers hivi ni vile vinavyotokea kwenye sehemu inayojulikana kama esophagus, ni sehemu inayounganisha koo la chakula na tumbo la chakula. Na aina ya mwisho hujulikana kama duodenal ulcers hivi hutokea kwenye sehemu ya juu ya utumbo mdogo inayofahamika kama duodenum.

 

 

Kwa siku za mwanzo ni ngumu kugunduwa kama una vidonda vya tumbo. Vipimo vinahitajika kugundua kama una vidonda vya tumbo. Kwa kuwa vidonda vya tumbo vina sababu nyingi na hutokea kidogo kidogo, basi hata matibabu yake yanaweza kuchelewa. Endelea na makala hii hadi mwisho, nitakujuza vipimo vipi hutumika kutibu vidonda vya tumbo na ni matibabu gani yanahitajika kulingana na aina ya vidonda na sababu za kutokea kwake.

 

Vipimo vya vidonda vya tumbo:

Vipimo vya vidonda vya tumbo vimegawanyika katika makundi mengi. Na hata gharama za vipimo vyake zinatofautiana kulingana na kipimo kilichotumika. Hivyo kaama una dalili za vidonda na umepima huna badili aina nyingine ya kipimo. Aina hizo ni kama:-

 

  1. Aina ya kwanza ya kipimo ni ila ambayo lwngo lake kubwa ni kuchunguza kama ndani ya tumbo kuna bakteria aina ya H.pylori. Hawa ndio bakteria ambao wanasababisha vidonda vya tumbo kwa kiasi kikubwa. Vipimo hivi mara nyingi ni kwa njia ya kinyesi. Hata hivyo vinaweza kufanyika kwa njia ya pumzi (hewa) ama damu lakini njia hizi sio sahihi kuliko kwa kutumia kinyesi

 

  1. Kwa kutumia kifaa cha kuingiza tumboni kinachojulikana kama endoscope. Hiki hungizwa ndani ya tumbo kisha humulika kama katochi. Kwa msaada wa kifaa hiki vidonda vya tumbbo vinaweza kuonekana kwa macho

 

  1. Kwa kutumia x-ray hii ni x-ray aalimu kwa lengo la kuchunguza safu za juu za tumbo. Kipimo hiki pia hufahamika kwa jina la barium swallow.

 

Matibabu na dawa za vidonda vya tumbo:

Kama ulivyojifunza huko juu kuwa matibabu ya vidonda vya tumbo hutolewa kwa kulingana na aina ya vidonda na kulingana na sababu zake. Kama sababu ni bakteria mgonjwa atapewa dawa za kuuwa bakteria. Kama  sababu ni ongezeko la tindikali tumboni mgonjwa atapewa dawa ya kupunguza uzalishaji wa tindikali tumboni. Dawa za vidonda vya tumbo ni kama:-

 

  1. dawa za kuuwa bakteria wanaosababisha vidonda vya tumbo. Dawa hizo ni kama
  2. Amoxicillin (amoxil)
  3. Cacithromycin (Biaxin)
  4. Metronidazole (flagyl)
  5. Tinidazole (tindamax)
  6. Tetracycline (tetracycline HCL
  7. Levofloxacin (levaquin)

 

  1. dawa za kuzuia uzalishwaji wa tindikali za tumboni. Dawa hizo ni kama:-
  2. Omeprazole,
  3. lansoprazole,
  4. Rabeprazole
  5. Esomeprazole
  6. Pantoprazole

 

  1. Dawa za kupunguza uzalishwaji wa tindikali tumboni. Hiki ni kama
  2. Ranitidine
  3. Famotidine
  4. Cimetidine
  5. Nizatidine

 

  1. Dawa za kulinda ukuta laini wa tumbo hizi hujulikana kama cytoprotective agent. Dawa hizi ni kama sucralfate na misoprostol

 

Dawa mbadala za vidonda vya tumbo.

Tofauti na dawa hizo lakini pia vidonda vya tumbo viaweza kutibiwa na tiba mbadala. Kuwa makini sana na tiba hizi kwa sababu hazina vipimo maalumu. Tiba hizi mara nyingi hufanya kazi vyema kama sababu ya vidonda ni bakteria. Lakini kama sababu ni nyingine tiba hizi sio sahihi sana. Tiba hizi hujumuisha

  1. Karoti, kabichi na bamia (hizi unaweza kutengeneza juisi yake).
  2. Asali
  3. Kitunguu thaumu
  4. Shubiri

 

Athari za kutotibu vidonda vya tumbo:

Ugonjwa wowote unaweza kuwa na madhara zaidi endapo utachelewa kutibiwa. Hali hii pia ni kwa vidonda vya tumbo. Endapo havitatibiwa badi athari mbaya zaidi inaweza kutokea. Ni kawaida kwa vidonda vya tumbo kusababisha kifo ila kama havitatibiwa mwisho wake unawez akuwa kifo. Hebu tuone athari za kutotibu vidonda vya tumbo:-

 

  1. Kuvuja kwa damu ndani ya tumbo. Damu hii unaweza kuiona kwenye kinyesi ama kinyesi kuwa cheui sana amakuwa na damu. Hali kama hii inaweza kusababisha upungufu wa damu mwilini.

 

  1. Chakula kinaweza kupita bila ya kumeng’enywa. Kutokana na kuwepo vidonda kkwenye utumbo mdogo, chakula kinaweza kupita hata bila ya kumeng;enywa na kuingia kwenye damu kwa ajili ya kutumika mwilini. Endapo hali kama hii itatokea mtu anaweza kushiba kwa haraka sana na anaweza kupoteza uzitoto kutokana na kukosa virutubisho.

 

  1. Pia vidonda vya tumbo visipotibiwa vinaweza kusababisha maambukizi ya magonjwa mengine tumboni.
  2. Vinaweza kupelekea utumbo kukatwa. Yesendapo eneo la jeraha limekuwa kubwa na gumu kutibika tiba mbadala ni kuondoa kipande cha utumbo kilichoharibika.

 

Mambo hatari kwa mwenye vidonda vya tumbo:

  1. Kunywa pombe
  2. Kuvuta sigara
  3. Kula vyakula vyenye uchachu sana
  4. Kuwa na misongo ya mawazo
  5. Kukaa na njaa kwa muda mrefu
  6. Kula vyakula vyenye pilipili kwa wingi
  7. Kula vyakula vyenye chumvi sansa

 

Tukutane makala ijayo tuakapoangalia kuhusu dalili za minyoo na sababu zake.





           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 1430


Sponsored links
πŸ‘‰1 kitabu cha Simulizi     πŸ‘‰2 Kitau cha Fiqh     πŸ‘‰3 Kitabu cha Afya     πŸ‘‰4 Madrasa kiganjani    

Post zifazofanana:-

Dalili za ugonjwa wa kipindupindu
Post hii inahusu zaidi juu ya ugonjwa wa kipindupindu.Ni dalili zinzojitokeza kwa magonjwa wa kipindupindu. Soma Zaidi...

Habari nasumbuliwa na tumbo upande wakilia adi nikikojoa mkojo wa mwisho uwa wa kahawia tiba take nini?
Maumivu ya tumbo yanaweza kusababishwa na mambo mengi ikiwemo typhod, vidonda vya tumbo na shida nyingine kwenye mfumo wa chakula. Soma Zaidi...

Madhara ya kushindwa kupitisha mkojo.
Posti hii inahusu zaidi madhara ya kushindwa kupitisha mkojo, ni madhara makubwa yanayotokea kwa mtu iwapo akishindwa kupitisha mkojo. Soma Zaidi...

Visababishi vya ugonjwa wa Varicose vein
Posti hii inahusu zaidi visababishi mbalimbali vya ugonjwa wa vericose veini, ni visababishi mbalimbali ambavyo utokea kwenye mtindo wa maisha kama tutakavyoona. Soma Zaidi...

Ugonjwa wa Maambukizi ya mfumo wa mkojo kwa watoto chini ya miaka mitano (UTI)
posti hii inazungumzia kuhusiana na Maambukizi kwenye mfumo wa mkojo ambapo kitaalamu hujulikana Kama UTI(Urinary Tract Infection (UTI)) hufafanuliwa kuwa ni maambukizo ya mfumo wa uzazi ambayo yanahusisha urethra. UTI ni maambukizi ya mfumo wa mkojo, m Soma Zaidi...

Je kwa mfano mimi nmeupata ukimwi leo na sihitaji kwenda kupima yaaan uanza kujionyesha baada ya muda gani
Watu wengi wamekuwa wakijiuliza kuwa ukimwi huonekana baada ya muda gani toka kuathirika? Soma Zaidi...

SABABU ZINAZOPELEKEA KUJAA KWA MATE MDOMONI NA MATIBABU YAKE
Kutokwa na mate mengi mdomoni si ugojwa ni hali inayoweza kutokea kwa mtu yeyote. Mara nyingi hali hii haihitaji matibabu wa dawa, na huondoka yenyewe. Lakini hutokea baadhi ya nyakati ikawa mate yanatoka zaidi mdomoni. Je na wewe ni miongoni mwao? Makala Soma Zaidi...

Dalili za maambukizi kwenye tumbo na utumbo mdogo
Posti hii inahusu zaidi maambukizi kwenye tumbo na utumbo mdogo,ni dalili ambazo ujionesha kwa mtu akiwa na shida kwenye utumbo mdogo na tumbo la kawaida. Soma Zaidi...

MARADHI MENGINE 10 YANAYOTOKANA NA MBU ( matende, ngirimaji, homa ya manjano, n.k
Tofauti na maradhi yaliyotajwa hapo juu pia tafiti za kisayansi zimethibitisha kuwepo kwa maradhi mengine hatari yanayosambazwa na mbu, kama vile ngirimaji pamoja na matende. Soma Zaidi...

Dalili za Saratani ya utumbo mdogo.
Posti hii inaonyesha ishara na dalili za Saratani ya utumbo mdogo Soma Zaidi...

Dalili za kipindupindu na njia za kujilinda na kipindupindu.
Post hii inazungumzia zaidi kuhusiana na ugonjwa wa kipindupindu.kipindupindu ni ugonjwa unaosababishwa na mdudu ambaye kwa kitaalamu anaitwa vibrio cholera.mdudu huyu hushambulia utumbo mdogo na kusababisha madhara mengi. Soma Zaidi...

Njia za kupunguza ugonjwa wa zinaa
Posti hii inahusu zaidi njia ambazo zinaweza kutumika Ili kuweza kupunguza kuwepo kwa magonjwa ya zinaa Soma Zaidi...